USHAURI: Kwa Nini Maskini Wanapendelea Kuwa Maskini


Habari yangu ni njema sana.

Kuna uhusiano mkubwa sana Tena sana Kati ya kuzaliwa kwenye familia masikini na kuendelea kuwa maskini maisha yako yote.

Kwanza unapozaliwa kwenye familia masikini unachoona ni umaskini. Nahata stori zinazopigwa ni kimasikini. Wakiongelea matajiri wanaongelewa kama watu wabaya, watu ambao hawana huruma, watu ambao wanawaonea wengine. Watu ambao wameupata utajiri wao Kwa ubaya na siyo Kwa uzuri.

Sasa hiki kitu kinaanza kujengeka kwenye Akili yako kiasi kwamba unaanza kuuchukia utajiri.

Na ukweli ni kwamba ukiuchukia utajiri huwezi kuupata. Huwezi kupata kitu ambacho hupendi.

Chukulia mfano wa MARAFIKI, wenza au watu wa karibu. Kama mtu unamchukia huwezi kuwa naye karibu. Hii rahisi sana kueleweka. Na kwenye utajiri Iko hivyohivyo, kama huupendi utajiri huwezi kuupata hata kidogo.

Ili kuondokana kwenye huu mtego unapaswa kuanza kuuona utajiri kama kitu ambacho kinawezekana na ambacho unastahili kupata kwenye maisha yako. Ona utajiri kama haki yako ya kuzaliwa na mara zote jiambie kwamba Mimi ni tajiri na utajiri ni kitu kizuri.

Pili, unapozaliwa unakuwa na watu ambao hawana tabia za matajiri. Na kama unavyojua ndege wa aina Moja huruka pamoja.
Ili uwe tajiri unapaswa kuwa umezungukwa na matajiri au watu ambao wanaamini kwenye utajiri. Ukizungukwa na watu ambao maskini Kwa kanuni ya wastani ni kuwa na wewe unaenda kuwa maskini mwingine.
Ili kujinasua kwenye hili unapaswa kuanza kujihusisha na watu waliofanikiwa, matajiri na watu wenye maono makubwa sana

Hao ndio wawe MARAFIKI zako.

Kitu kingine na muhimu sana ni kwamba maskini wanapenda sana kupata utajiri Kwa haraka (shortcut). Nadhani Kwa sababu wapo KWENYE umaskini basi wanataka watoke Kwa haraka na kuingia KWENYE utajiri. Hiki kitu kinawafanya waendelee kuwa maskini zaidi.

Unajua Kwa Nini? Njia yoyote ya mkato Huwa inafanya maisha kuwa magumu zaidi. Na ndio maana maskini wengi wanatapeliwa, wanaingizwa KWENYE fursa feki na vitu vingine kama hivyo.

Ili kuondokana na hili unapaswa kuchagua fursa au biashara Moja, Kisha kuamua kufanya biashara hii na kuachana na fursa nyingine hata kama ni nzuri kiasi gani. Ukweli ni kwamba kila siku Kuna fursa mpya nzuri Kwa ajili Yako. Huwezi kufanya kufanyia KAZI kila fursa na siyo kila fursa inakufaa wewe.

Lakini pia Kuna tabia Fulani ambazo matajiri wanazo. Tabia kama kuweka akiba, kuwekeza, kujifunza n.k hivi vitu masikini hawana. Familia za kimaskini hazina hivi vitu.

Unahitaji nguvu ya ziada kuanza kufanya hivi vitu unapokuwa hujazoea kuvifanya. Na ili ujenge tabia hizi utahitaji kuweka nguvu ya ziada ambayo usipokuwa na nidhamu itakushinda.

Kiufupi, ni kama Newton alivyosema kwenye Sheria zake. Newton anasema kwamba kitu chochote ambacho kimetulia kitaendelea kukaa kwenye hali hiyo ya utulivu mpaka NGUVU YA ZIADA itakapotokea na kukitoa hicho kitu hapo na kupeleka kwenye HATUA ya ziada.

Hivyohivyo, kitu chochote ambacho kipo kwenye mwendo kitaendelea kukaa kwenye mwendo mpaka NGUVU YA ZIADA itakapotokea.

Na umaskini uko hivyohivyo, utaendelea kuwa maskini mpaka utakapoamua kuweka NGUVU YA ZIADA kujinasua.

Asante
Naamini jibu hili limekuwa lenye manufaa kwako

,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X