Hiki kitu kimoja tu kinaweza kukufanya ulipwe zaidi ya unavyolipwa Sasa


Rafiki yangu, najua Mara kwa mara huwa nakwambia njia mbalimbali za kukusaidia KUONGEZA kipato chako.

Nafanya hivyo kwa sababu nakupenda. Najua wazi kuwa haupaswi kutegemea chanzo kimoja cha kipato. Lakini pia najua wazi kuwa kama chanzo chako kimoja ni ajira Basi maana yake unapaswa kuhakikisha kwamba umepanbana na kuongeza vingie zaidi zaidi ili vitakavyokuingizia kipato bila Kokomo.

Nadhani, kama Kuna mchezo ambao kila mmoja anapaswa kuufurahia hapa duniani Basi ni mchezo wa kuhakikisha kwamba   anaongeza kipato chake Mara kwa mara. Na hili linawezekana vizuri sana. Na ndio maana nimekuwa nasukumwa kukwambia njia mbalimbali za kuongeza kipato chako, na hata nimeandika vitabu kadha wa kadha vya kukusaidia kwenye hili Kama kitabu cha

MAAJABU YA KUWEKA AKIBA
JINSI YA KUONGEZA THAMANI YAKO na
MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE.

Sasa siku ya leo nataka nikwambie kitu kimoja ambacho kitakufanya wewe uweze kulipwa zaidi ya unavyolipwa sasa. Kitu hiki siyo kingine bali ni uhakika wa kutegemewa kufanya jambo na ukalifanya.

Yaani, kwamba mtu anaweza kujiamini kwamba utafanya Jambo fulani, na kweli Hilo jambo ukalifanya bila shida yoyote.

Hili ni jambo ambalo unapaswa kujijengea.
Moja ya kitu ambacho kimekuwa kinanishangaza ni kuwa vijana wengi huwa wanaandika kwenye CV zao kuwa ni wachapakazi na wanaweza kufanya kazi hata kwenye msukumo mkubwa. Utakuta MTU ameandika kwenye CV yake kuwa “I can work under pressure”. Lakini Sasa njoo kwenye uhalisia. Huyo mtu hawezi kufanya hata za kawaida tu.

Ulimwachia kazi na ukaondoka huyo mtu anakuwa siyo wa kutegemewa. Ni mpaka uwepo ndipo anaweza kufanya kazi. Kama haupo hawezi kufanya kazi.

Ukiwa na tabia ya Aina hii huwezi kutegemea kulipwa zaidi kama ambaye anategemea kufanya kitu na anahakikisha kwamba amekifanya.

Hivyo, Kuanzia siku ya leo nataka uwe mtu wa kutegemewa.
Kutegemewa kufanya kazi na ukalifanya.
Kutegemewa utawahi na ukawahi
Kutegemewa kufanikisha kitu au vitu fulani na ukaweza kuvifanikisha.

Rafiki yangu, inawezekana na ninakitakia kila la kheri.


3 responses to “Hiki kitu kimoja tu kinaweza kukufanya ulipwe zaidi ya unavyolipwa Sasa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X