Mfuko wa FAIDA (FAIDA FUND): Unawekeza au Huwekezi?


Watumishi Housing Investment (WHI) wameanzisha mfuko wa uwekezaji wa pamoja ambao wanauita MFUKO WA FAIDA au kama unaielewa vizuri lugha ya kigeni basi unasema FAIDA FUND. Mfuko wao ni mfuko ulio wazi (open-endend). Kama bado hujasoma kitabu changu cha maajabu ya kuwekeza kwenye hisa, hatifunagni na vipande lazima tu utakuwa unajiuliza mfuko ulio wazi maana yake ni nini?

Mfuko ulio wazi ni mfuko ambao pale unapotaka kununua vipande meneja wa mfuko anakutengenezea vipande vyako. Na pale unapotaka kuuza vipande meneja wa mfuko ananunua vipande vyako.

Yaani, tuchukilie mfano, mimi naanzisha mfuko wa uwekezaji wa pamoja. Na watu mnakusanyika kununua vipande, labda kipande kimoja ni shilingi mia moja. na watu wa kwanza, mnanunua vipande elfu moja (1000). Mfuko hapo hapo utakuwa na vipande elfu moja. Labda baada ya siku kumi za kununua vipande anatokea mmoja ambaye anataka kuuza vipande vyake 200. Anauza vipande na mimi meneja wa mfuko nanunua hivyo vipande na kumpa hela yake. Mfuko unabaki na vipande 800. Wakati kesho yake anatokea mwingine ambaye anataka kunununua vipande mia tano. Na huyo anaunua vipande na hivyo vipande vya mfuko sasa vinakuwa 1300/-.

Kwa hiyo, mfuko ulio wazi huwa una sifa ya kuongezeka kwa vipande pale wanunuaji wanaponunua na kupungua kwa bei pale wauzaji wanapouza.

Mfuko ulio wazi (open ended) ni tofauti kabisa na mfuko uliofungwa (closed ended) ambao wenyewe huwa una idadi ya kamili ya vipande, na idadi hiyo huwa haiongezeki wala kupungua. Kama mfuko una vipande 1000. Vinabaki kuwa hivyo hivyo tu miaka yote. Ili ununue vipande kwenye mfuko uliofungwa, lazima awepo mtu anayeuza. Na ili uuze, lazime kuwepo anayenunua. Utagundua kitu hiki ni tofauti na mfuko ulio wazi ambao meneja wa mfuko ndiye ananunua au kukuuzia vipande. Kama huelewi, hakikisha unapata kitabu changu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE kwa 20,000 tu, nakala ngumu, na 10,000 tu nakala laini (softcopy).  Kipate kitabu hiki kwa ajili ya kuongeza maarifa zaidi pia kuhusu eneo hili la uwekezaji.

Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy0
Kitabu hiki kinapatikana kwa 20,000/- tu

Mimi niache niendelee mbele kuuongelea mfuko wa FAIDA ulioanzishwa na WHC.

Mfuko upo chini ya WHI ambao wamesajiliwa na kisheria chini ya soko la mitaji (CMSA).

Madhumuni ya mfuko

•   Mfuko huu   ni    mpango    ulio    wazi unaotoa fursa nyingine ya uwekezaji kwa Watanzania hasa wa kipato cha kati na cha chini kupitia uwekezaji katika vipande ili kupata mapato shindani kupitia ukuaji wa mitaji.

• Kuwajengea watanzania utamaduni wa kuwekeza katika Masoko ya Fedha na Mitaji na kuweka akiba.

Anayestahili kuwekeza kwenye huu mfuko

Mfuko huu unatoa mwanaya wa mtu yeyote, (ambaye ni mtanzania au wa nje ya nchi) kuwekeza kwenye mfuko huu. Lakini pia taasisi kama benki, mifuko ya pension, taasisi za kiserikali,  taasisi zisizo za kiserikali, taasisi za kijeshi, makampuni n.k.

Kiwango cha chini cha kuwekeza kwenye mfuko huu

Kiwango cha chini cha kuwekeza kwenye huu mfuko ni elfu kumi, pale unapofungua akaunti mara ya kwanza. Baada ya kufungua akaunti, unaweza kuendelea kuwekeza zaidi kwenye huu mfuko kwa kuongeza kiwancho cha chini kabisa cha shilingi elfu tano.

Kiwango cha juu cha kuwekeza

Hakuna kiwango cha juu cha kuwekeza. Kwa hiyo, kama una mabilioni ya kuwekeza, unaweza kuyawekeza bila shida yoyote kwenye huu mfuko. Lakini bado kama huna mabilioni makubwa sana, unaweza kuendelea na utaratibu wako wa kuwekeza kwenye huu mfuko kadiri utakavyojiwekea, kwa kuweka kiwango cha chini kabisa cha elfu tano (5,000/-) kila utakapohitaji kuwekeza.

Gharama za kujiunga na mfuko (Entry load)

Kwa kawaida huwa ukitaka kununua hisa, huwa kuna gharama ambayo mtu unalipia ili kununua hisa. Na pale unapotaka kuuza hisa zako, kuna gharama ambazo unakatwa. Hizi gharama kwa Kiswahili tunaweza kuziita tozo za kiujiunga (entry load) au tozo za kujitoa (exit load).

Wakati wa kujiunga na mfuko huu au wakati wa kujitoa kwenye huu mfuko, hakuna gharama yoyote ile ya kujiunga au kujitoa.

Thamani ya kipande

Thamani ya mwanzo ya kipande ni Tsh 100/=. Hii itatumika wakati wa mauzo ya awali na baada ya hapo kipande kitauzwa kulingana na thamani halisi.

Ambapo kipande kitapanda au kushuka kulingana na mwenendo wa soko kwa wakati husika.

NB: Mpaka sasa hivi mfuko upo kwenye hatua za awali za kuuza vipande vyake. Hivy, kama unasoma ujumbe huu kabla ya tarehe 31 Disemba, unaweza kununua vipande kwa bei ya awali ya vipande.

Ukwasi

Uuzaji wa vipande utafanyika kila siku baada ya mienzi mitatu tangu kumalizika kipindi cha mauzo ya awali. Mfuko utatuma malipo ya mauzo ya vipande ndani ya siku tatu za kazi baada ya kupokea maombi katika Makao Makuu ya Watumishi Housing Investments. Fedha za mauzo zitatumwa moja kwa moja katika akaunti ya benki ya mwekezaji au simu ya mkononi iliyosajiliwa.

Sera za uwekezaji kwenye mfuko

Mfuko utawekeza katika masoko ya fedha kwa asilimia 100%. Kiwango cha uwekezaji katika masoko ya fedha na Dhamana kitalenga kupata mapato makubwa katika soko.

Muda wa kuendesha mfuko

Mfuko huu ni wa kudumu kwa mujibu wa Waraka wa Makubaliano.

Faida za kikodi

Kwa mujibu wa sheria za nchi,mgawanyo wa mapato ya Mfuko yamesamehewa kodi ya mapato kwa wawekezaji.

Hayo ni baadhi ya mambo ambayo nimekuandalia kuhusu  mfuko huu.

NB: 1. Kabla hujachukua hatua ya kuwekeza kwenye huu mfuko, nashauri uhakikishe umesoma kitabu changu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE ili uweze kuelewa zaidi dhana ya uwekezaji.

2. Mwandishi wa makala hii hauhusiki kwa vyovyote vile na faida au hasara utakayopata kutokana na uwekezaji utakaoufanya kwenye huu mfuko. Ni muhimu kuhakikisha kwamba umepata ushauri wa watalaam kabla ya kufanya uwekezaji.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.


6 responses to “Mfuko wa FAIDA (FAIDA FUND): Unawekeza au Huwekezi?”

  1. Thank you so much Bro huu ndio unaitwa uungwana hakika Roho ya kutoa ukiwa nayo lazima uzidi kubarikiwa nami nakuombea baraka lete mbele ya Mwenyezi Mungu kila utakachogusa kiwe ni baraka kwako na familia yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X