Aina Tano (05) Za Ujuzi Unazohitaji Ili Kuwa Milionea Kwenye Ulimwengu Wa Leo


Kwenye makala niliyotuma kwa watu wa nguvu ambao huwa wanapokea makala zangu kwa njia ya email jana. Niliandika kwamba zama zimebadilika na wewe unapaswa kubadilika. Kama hujajiunga na mfumo wetu wa kupokea makala kwa njia ya barua pepe nina hakika huo ujumbe hukuuona,  hivyo, leo nimelazimika kuuweka huo ujumbe kwenye blogu yetu hapa ili na wewe uweze kuuona na kikubwa zaidi ni kwamba uweze kunufaika nao. Hivyo unaweza kuusoma kwa kubonyeza hapa rafiki yangu.

Sasa baada ya jana kukwambia kwamba zama zimebadilika, basi leo nataka nikwambie aina saba za ujuzi unaopaswa kuwa ili uweze kutoboa kwenye ulimwengu wa leo ambao umebadilika sana.

SOMA ZAIDI: Vitu Viwili Ambavyo Havitapitwa na wakati kwenye zama hizi

Unashangaa ee!

Usishangae! Unapaswa kuzoea kitu hiki, kwa sababu ulimwengu wa leo umebadilika sana. Kwenye uliwengu wa leo umilionea ni neno ambalo unapaswa kulitumia sana, na hata wewe unapaswa kupambana sana kuhakikisha kwamba unaufikia walau umilionea kama siyo ubilionea.

Sasa ujuzi huu ndiyo utakufanya wewe utobe.

1. Ujuzi wa kuongea mbele ya watu wa  kuwasilisha mada au kitu unachofikiria

kuna watu wengi wana vitu vizuri sana ndani yao. ila vitu wanashindwa kuvifikisha kwa watu kutokana na kukosa ujuzi sahihi wa kuwasilisha kile walichonacho. Naomba unisikilize mimi kwenye hili. Kwenye uliwengu wa leo unahitaji sana ujuzi wa kuongea mbele ya watu.

Hata kama umeajiriwa. huu ujuzi ni muhimu kwako, maana ujuzi huu pekee tu unaweza kukufikisha kwenye umilionea. Dunia ya leo bado inawapenda sana watu ambao wanaweza kusimama mbele ya watu na kuwasilisha mada kwa namna ambayo inaeleweka.

Naamini, wewe ni kama mimi huwa hupendi mtu anayesimama mbele ya watu kuongea na kuanza kumung’unya maneno. Au mtu anayesimama na kuwasilisha mada kama vile anaogopa dunia itammeza.

Huwa siwapendi watu wa aina hii. Ila ukifuatilia wengi ambao huwa wanaoongea mbele ya watu, huwa wanaongea kwa namna ya kipumbavu kama hii.

Rafiki yangu, unahitaji kujitofautisha. Kuanzia leo hii anza kujenga ujuzi wa kusimama mbele ya watu na kuongea. Uongee na watu wawe na shauku ya kukusikiliza wewe ukiongea. Siyo unaongea mpaka unaboa watu wanaanza kutafuta simu zao ziko wapi ili wachati.

huu ni ujuzi ambao haufundishwi shuleni, ila ni ujuzi ambao unahitaji kujifunza ili uweze kula mema yanchi. Nakwambia rafiki yangu, kamwe, usije ukafanya kosa la kuishi bila ya huu ujuzi.

anza leo kujifunza ujuzi huu baada ya kusoma hapa. Kuna kozi kibao mtandao ambazo unaweza kusoma na zikakusaidia kupata ujuzi huu. Ukweli ni kwambaa kama kuna ukomo ambao utakuzia, basi utakuwa ni ukomo ambao umejiwekea mwenyewe.

2. ujuzi wa kuanzisha na kusimamia na kukuza biashara

Huu ni ujuzi ambao unauhitaji rafiki yangu. kwenye ulimwengu wa leo kuwa na biashara ni moja ya hitaji la muhimu sana.

Najua unaweza kuwa unasema kwamba ajira peke yake inanitosheleza.

Ninachotaka kukwambia ni kwamba kama unataka kufikia kiwango cha  kuwa na fedha ambacho kitakupa uhuru. Basi kuwa na biashara ni lazima.

Ni kweli ajira inakupa kipato. Ila nina  uhakika kipato chako hakiwezi kuwa kikubwa sana kiasi cha kukufanya uweze kufurahia mambo mengine matamu yaliyo kwenye hii dunia.

Lakini pia kipato cha ajira pekee, nina hakika hakitoshi kukufanya wewe uweze kuwekeza na kufanya mambo mengine ya kipekee.

Kwa Tanzania, asilimia kubwa ya wafanyakazi wanalipwa chini ya milioni moja kwa mwezi. Hiki kiasi kinaweza kukutosha tu kula, kunywa na kufanya mambo mengine ya kawaida. Ila hakiwezi kukutosha wewe kufanyia kazi ndoto zako mpaka kuweza kuzifikia. Na hapa ndiyo maana, unahitaji kuwa na biashara

Ubora wa biashara ni kwamba inaweza kukupa kipato kisicho kuwa na kikomo.

Kadiri utakavyoweka juhudi kubwa kwenye biashara yako ndivyo ambavyo utaweza kuongeza kipato chako zaidi.

Kwa hiyo nakushauri rafiki yangu uweze kuanzisha biashara. Hata kama ni kijibiashara kidogo, anza na hicho.

Kama umeajiriwa, tumia muda wako wa ziada baada ya kutoka kazini au kabla ya kwenda kazini kwa ajili ya kufanyia kazi biashara yako.

Rafiki, usiridhike na hayo maisha. Maisha yanabadilika kila kukicha. Hivyo, kwa vyovyote vile, pambana kuhakikisha kwamba unaanzisha hata kijibiasahra kidogo ambacho kitakupa kipato bila ukomo.

SOMA ZAIDI:

Tatu jifunze ujuzi ambao unaweza kukuingizia kipato cha milioni moja na zaidi

Kama nilivyoandika kwenye makala ya jana. Kuna aina fulani za ujuzi kwenye ulimwengu wa leo ambao ukiwa nao, unaweza kukuingizia kipato cha milioni  moja na zaidi. na hii syo kwa mwezi, siyo kila baada ya siku mbili au tatu. Bali ni kwa siku moja. aina hizi za ujuzi zipo rafiki yangu, chagua aina walau moja ya ujuzi wa aina hii kisha anza kuujenga.

Kabla sijakupa mifano ya aina  hii ya ujuzi nataka wewe mwenyewe uweze kutafakari kuhusu watu ambao unawafuatilia sana kwenye mitandao ya kijamii.

Hivi watu wa aina hii ni wapi? Wana kitu gani ambacho kinakufanya uwafuatilie. Ukifuatilia kwa umakini utagundua kuwa baadhi ya hawa watu wana huo ujuzi ndio maana hata wewe unawafuatilia. Inawezekana ni ujuzi wa kuongea mbele ya watu na kuwasilisha mada zao kwa ustadi wa hali ya juu sana, inawezekana ni ujuzi wa kuandika, inawezekana ni ujuzi wa kuuza, unaweza pia kuwa ni ujuzi kuunda timu sahihi ya watu, unaweza kuwa ni ujuzi wa kung’ang’ania kitu kimoja mpaka kieleweke au ujuzi wa kuburudisha.

Kwa vyovyote vile ebu na wewe chagua ujuzi wako ambao unataka kuwa nao maishani. Kisha anza kuujenga.

Tena unaweza kuwa aina mbli za ujuzi na kuziunganisha na kuwa kitu kimoja. Hiki kitu kitalaamu kinaitwa skill sexing au idea sexing. Unaweza kukisoma zaidi kwa kubonyeza hapa

SOMA ZAIDI: Kitu kimoja ambacho watu hawajui kuhusu uwekezaji

Nne, jifunze kusema hapana kadiri uwezavyo

Huu ni ujuzi ambao unapaswa kuwa nao pia. Maana kama utafuata mbinu ambazo nimekueleza hapa, muda siyo mrefu wewe utakuwa ni mtu wa viwango vingine. muda siyo mrefu kila mtu atakuwa anahitaji muda wa kuwa na wewe.

Sasa hapa, unahitaji kuwa bahili wa muda wako. Unakuwa bahiri siyo kwa ubaya bali kwa uzuri. Ili uweze kuwekeza muda wako kwenye kufanya kazi za maana kwako na kuachana na kazi ambazo hazikujengi wala kukuongezea kitu chochote.

Kwa hiyo, kama unataka kuujenga umilionea, jifunze kusema hapana nyingi kwa vitu ambavyo siyo vya muhimu kwako na vitu mbavyo havikusogezi wewe kwenye kufanikisha lengo lako. Badala yake wekeza muda wako huo kwenye kufanyia kazi malengo na ndoto zako mpaka uweze kuzikifia.

SOMA ZAIDI: Huyu Ni Mtu Ambaye Lazima Utamwambia Hapana

Tano ujuzi wa kuwekeza

Huu ni ujuzi mwingine ambao unauhitaji. Rafiki yangu unahitaji uwe na ujuzi wa kuwekeza ili uweze kutunza fedha zako unazopata kwa uzuri na kwa namna ambayo itakusaidia wewe kuendelea kukuza utajiri wako.

Nimeandika zaidi kuhusu uwekezaji na hasa uwekezaji kwenye hisa kwenye kitabu cha maajabu ya kuwekeza kwenye hisa, hatifungani na vipande. Unaweza kukipata hicho kitabu kwa kufuata maelekezo haya hapa

maelekezo ya kupata kitabu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE haya hapa

Au unaweza kuwasiliana moja kwa moja na +255 684 408 755 sasa.

SOMA ZAIDI: 

Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu. Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.

Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.

SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea

Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X