Ushauri Mzuri Ambao Nimewahi Kupokea Maishani Mwangu


Nakumbuka mwaka 2016 hivi wakati naendelea na masomo yangu ya chuo. Nilikuwa njia panda nikifikiria niache chuo niendelee na biashara na uandishi au nifanyeje?

Uamuzi wangu ulikuwa kuacha chuo…

Baadaye katika kuwashirikisha watu wangu wa karibu; mmoja wao aliniambia hivi;

Godius fanya vyote, endelea na kusoma, andika na fanya biashara. Ukifanikisha vyote vitatu utaonekana shujaa siku za mbeleni utaonekana shujaa mkubwa sana.

Leo hii sipo hapa kukwambia kwamba mimi ni shujaa kwa sababu nilifanya vyote. Ila tu kukushirikisha yafuatayo:

1. Kwenye maisha kuna watu ni wabobevu na wana ujuzi na uelewa mpana zaidi yako. Inapotokea ukawa njia panda basi usisite kuwasiliana nao ili wakusaidie kukupa ushauri.

2. Unapokuwa njia panda huelewi ufanye kitu gani, unapaswa kufikia uamuzi wa kufanya kitu. Kutokufanya uamuzi kabisa ni hatari. Chagua kitu kimoja na ukisimamie hicho.

3. Kama upo chuoni, usiache chuo. Leo hii nipo nafikiria hivi ningeacha chuo mwaka ule ingekuwaje sasa hivi. Sisemi hivyo labda eti kwa sababu labda nimeajiriwa. Sijaajiriwa na hata cheti changu cha chuo sijawahi kukitoa chuoni! Ila kwa sababu moja tu. Katika kuendelea kusoma nilikuja kujifunza kitu ambacho leo hii nimeamua kukifanyia kazi maisha yangu yote.

Kuna kozi nilikuwa bado sijajifunza kipindi nataka kuacha chuo. Sasa hivi nimefungua kampuni kufanyia kazi kile nilichojifunza kwenye hiyo kozi.

Rafiki yangu, huo ndio ushauri mzuri ambao nimewahi Kupokea maishani mwangu.

Wewe unakumbuka ushauri mzuri ambao umewahi kupokea ni upi?

Tushirikishe hapa chini

[mailerlite_form form_id=0]


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X