Njia 7 Rahisi Za Kujenga Tabia Zitakazodumu


Katika familia au maeneo yaliyo mengi muda wa kupata kifungua kinywa, chakula cha mchana au cha jioni unajulikana, muda huo ukifika unakuta majukumu yaliyokuwa yanafanyika yanahairishwa kwa ajili tu ya kukamilisha jukumu la kupata chakula kwa wakati husika.

Ukifika muda wa chakula hakuna mtu  anayejiuliza mara mbili tatu kwamba aende kula muda huo au la aache. Ila badala yake muda ukifika mtu anaenda kula tu. Sasa kitu kama hiki ndicho kinakosekana kwa watu wanaotaka kujenga tabia mpya.

1.
Kama unataka kujenga tabia, tenga muda maalumu utakapokuwa unafanyaia kazi tabia hiyo. Ukishaweka muda pembeni kinachokuwa kimebaki Ni wewe kuonekana eneo la tukio ndani ya huo muda.

Kwa mfano kama unataka kujenga tabia ya kuandika. Tenga muda wa kuandika, labda saa 11 asubuhi mpaka saa 12 asubuhi.

Ukifika muda huo, onekana kwenye eneo la tukio. Fungua kompyuta kama unatumia kompyuta na Anza kuandika.
Inakuwa rahisi kwako kujenga tabia yako kihivyo. Na ndani ya huo muda haupaswi kamwe kufanya kitu kingine tofauti na kile ulichodhamiria. Kama ni kuandika basi utapaswa kuandika hata kama hujisikii.

USISEME kwamba ngoja niutumie muda huu kufanya kitu kingine halafu baadaye nitaandika. Amua muda huo kwamba nitaandika au la sitafanya kitu kingine.
Ni bora ndani ya muda huo ukae ukiwa unaingalia kompyuta yako bila kuandika kukiko kwenda kufanya kitu kingine, kitu ambacho najua huwezi.

Hivyo, utajikuta unalazimika kuandika kitu tu. Wewe andika kitu tu, hata Kama kitu hicho siyo bora ila andika. Muda wako ukiisha, achana na hicho kitu nenda kafanya mambo mengine

2.
Kitu cha pili kitakachokusaidia wewe kujenga tabia yako ni mazingira. Yaweke mazingira yako ili yaendane na tabia yako mpya unayotaka.
Kama unataka kusoma vitabu, Basi tenga eneo maalumu la kusomea vitabu.  Kisha lizungushe eneo hili na vitabu.

Uliwahi kufanyika utafiti kwenye chuo kimoja Marekani. Kwenye utafiti huo, waliongeza maeneo maji yalipokuwa yanapatikana kwenye mgahawa. Mwanzoni kulikuwa na maeneo mawili  yenye maji. Hata hivyo, baada ya huu utaratibu mpya maeneo yaliongezeka kutoka mawili.

Yaani, karibia kwenye kila kona ya mgahawa ilikuwa na maji. Kila ulipokaa uliona maji

Kilichotokea ni kwamba kulikuwa na ongezeko kubwa la watu kunywa maji kuliko ilivyokuwa mwanzo.

Mwanzoni watu walikuwa wanakunywa soda kwa wingi ila sasa zamu hii unywaji wa maji ukawa umeongezeka.

Kwa hiyo ikawa imegundulika kwamba ukibadili mazingira unaweza kubadili mengi. Kama unataka kujenga tabia ya kusoma vitabu, zungusha mazingira yako na vitabu vya kutosha. Hii njia unaweza pia kuitumia kuwajengea wanao au familia yako tabia ya kusoma vitabu.

Badala ya kuwa unanunua movie nyingi, jitoe kununua vitabu vya kutosha, Kisha hakikisha vitabu hivi vipo kwenye maeneo yanayoonekana kwenye familia yako. Hili litawafanya wanze kusoma kidogo kidogo.

3.
Njia ya tatu ya kujenga tabia kirahisi Ni kutofautisha vifaa vyako. Hapa unapaswa kuamua kuwa kifaa fulani Ni kwa ajili ya kazi fulani. Kwa mfano, Kama una simu mbili unaweza kuzitenganisha. Moja ikawa maalumu kwa ajili ya kusoma vitabu na kuandika na nyingine ikawa maalumu kwa ajili ya mawasiliano.
Kwa hiyo inakuwa inajulikana kwamba ukishika simu fulani, hapo moja kwa moja kifuatacho ni kusoma au kuandika tu.
Ukishika simu nyingine kazi yake ni kuchati na mawasiliano mengine

4.
Njia ya nne Ni kuwajulisha watu wako wa karibu juu ya tabia yako mpya. Wambie wajue kabisa kuwa ukikaa kwenye meza fulani hutaki usumbufu. Ndani ya muda huo mambo mengine yaendelee kama ambavyo ungekuwa ofisini au safarini. Usisumbukiwe na mtu yeyote unapokuwa meza au chumba fulani.

5.
Njia ya tano ya kujenga tabia mpya kirahisi ni kuwaambia watu ambao watakushirikiria. Unawaambia watu kuwa nitafanya kitu fulani na hivyo kwako inakuwa ni rahisi kutekeleza kile ulichopanga  maana unakuwa unajua kwamva endapo sitafanyia kazi hiki Kitu, Kuna watu watanishikiria.

6

Njia ya sita ni ya kutumia zawadi na adhabu. Hapa unaamua kuwa nikifanya na kukamilisha kitu fulani nitajipongeza na nisipofanya nitajiadhibu. Kwa mfano, unaweza kujiwekea utaratibu kuwa kila siku baada ya kukimbia kilomita moja nitakuwa nakunywa glass moja ya juisi fresh. Siku ambayo hujakimbia hakuna kunywa. Hiki Kitu kinaweza kukupa hamasa maana utakuwa unajua kwamba mara tu baada ya kukimbia kilomita moja kuna juisi fresh. Kama nakuona unavyojilamba!!!

7
Njia saba ni kutafuta mtu ambaye kazi yake ni kukushikilia wewe. Kwa mfano, unaweza kusema kwamba kila siku nitawapigia wateja 10 kuongea nao kuhusu biashara au bidhaa zilizo kwenye biashara yangu. Ukamshirikisha mtu kitu hiki, na kumwambia endapo sitafanya hivyo nitakulipa kiasi fulani. Hapa kinapaswa kuwa kiasi ambacho kitakuuma wewe kiasi kwamba utajisukuma kufanya hivyo la sivyo usipofanya hivyo utapaswa kulipa faini.

Niendelee au nisiendelee……

Mengine utayakuta kwenye kitabu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA. Unaweza kusapoti ukamilishwaji kwa kitabu hiki kilicho jikoni kwa kununua ebook hiyo hapo chini kwa elfu 2 tu
BONYEZA hapo chini kununua au wasiliana nami sasa kwa 0755848391 ili nikutumie.

Upendo utawale

Imeandikwa na GODIUS RWEYONGEZA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X