KAMA HAWAHESHIMU MUDA WAKO, HAWAKUHESHIMU


 

 

Najua. Ndiyo najua. Kuna siku umewahi kupanga kukutana na mtu fulani sehemu ambayo unaifahamu wewe na ukawa umejiandaa siku nzima kwa ajili ya hilo tukio halafu mtu huyo akawa amekwambia dakika za mwisho kuwa hatakuja au la hakuonekana kabisa na hakukuwa na taarifa yoyote ile aliyokupa.

Pengine wewe mwenyewe umekuwa ukiwafanyia watu wengine hivi. Ninachopenda kukwambia ni kuwa watu hao hawakuja kwa sababu waliona kwamba hakukuwa na kitu kikubwa wanaenda kupata kwako. laiti kama wangekuwa wanajua wakija kukutana na wewe tu wataondoka na milioni moja mkononi wasingehairisha kuja. Uongo ukweli? hata kama ingekuwa ni laki moja, bado wangekuja.

 

Kumbe hawakuona thamani yoyote kwako. au kama wewe ni ulihairisha kwenda kuonana na mtu dakika za mwisho ni wazi kuwa hukuona thamani yoyote ile ambayo unaenda kupata. Hivyo, uliona uende sehemu nyingine ambayo utapata thamani kubwa au uutumie muda wako kwa mambo mengine ya maana. Hivyo, hukuheshimu muda wa watu ambao wameupoteza kwa ajili yako. Kulikuwa na mambo mengi ambayo wangeweza kufanya ila hawakuyafanya, wameamua kuyaacha kwa ajili yako.

 

Kwahiyo kama hukuheshimu muda wao hukuwaheshimu na wao pia. Mtu yeyote ambaye unamheshimu utajihidi kuhakikisha kwamba unatokea kwa wakati na hata kuwahi mapema sana kabla ya yeye kufika. Ila kama humweshimu unachukulia vyoyote tu. umewahi, umechelewa kwako ni sawa. Ebu tafakari hii kauli ninayokupa leo. Kama huheshimu muda wa watu wengine, basi watu hao huwaheshimu.

 

Soma zaidi kanuni ya dakika 15 kutoka Lombardi


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X