Vitabu Vitano Vifupi Ambavyo Mtu Anayeanza Usomaji Wa Vitabu Anaweza Kuanza Navyo


 

Kama kuna tabia moja muhimu ambayo unpaswa kuijenga, basi ni tabia ya kusoma vitabu. Hata hivyo, usomaji wa vitabu unaweza kuonekana ni mgumu hasa kwa mtu ambaye anaanza kutokana na vitabu vingi kuwa vikubwa. kama unaanza kujenga tabia ya kusoma vitabu ni vizuri kuanza kusoma vitabu vifupi ila vyenye ujumbe mzito huku wakati huohuo ukiendelea kutanua wigo na kusoma vitabu vikubwa vikubwa.

 

Sasa leo hii nimekuandalia orodha ya vitabu vitano vifupi ambavyo wewe unaweza kuanza kusoma ili kujenga tabia ya kusoma vitabu,

1. 50 COMMON MISTAKES PEOPLE MAKE ABOUT MONE

Hiki ni kitabu kifupi ambacho kimeandikwa na Olumde Emmanuel kuhusu fedha. Katika kurasa za kitabu hiki hapa utajifunza mengi kusu fedha na unaweza kuchukua hatua hapohapo. Ukisikia kwamba kuna vitabu ambavyo vimeeleza mambo makubwa kwa ufupi na kwa lugha inayoeleweka basi ni hiki kitabu. Kimeeleza kila kitu kuhusu fedha kwa ufupi na kwa lugha ambavyo inaeleweka. Kichukue ukisome ili uweze kujionea mwenyewe.

 

2. WHO WILL CRY WHEN YOU DIE

Hiki ni kitabu cha Robin Sharma chenye mambo 101 kuhusu uongozi na mafanikio. Hiki ni kitabu kingine ambacho ni kidogo ila chenye mambo makubwa ndani yake. Ukisoma kitabu hiki hapa utajifunza mambo makubwa ndani yake ambayo unaweza kuanza kufanyia kazi ndani ya muda kidogo.

 

3. THE PROPHET

Hiki ni kitabu kingine kifupi chenye mambo makubwa ndani yake. Kimeandikwa na Khalil Gibran. Kitabu hiki  kimezungumziamambo mengi ndani yake. Kimezungumzia kuhusu uongozi, mahusiano, ndoa, watoto, wachungaji, kazi na mambo mengine mengi. Kila mada imeongelewa kwa ufupi huku ikikupa mwanya wa wewe msomaji kupata kitu cha kufanyia kazi na kuchukua hatua.

Hiki ni kitabu kingine kifupi ambacho kama msomaji unaweza kukichukua na kukifanyia kazi mara moja

 

4. NYUMA YA USHINDI KUNA KUSHINDWA, KUSHINDWA, KUSHINDWA.

Nyuma ya ushindi kuna kuhindwa ni kitabu kingine kidogo ila chenye mambo makubwa sana nadani yake. Kitabu hiki kimeeleza mchakato mzito ulio  nyuma ya ushindi ambao watu huwa hawapandi kuusikia. Mwandishi wa kitabu hiki  anasema kwamba Nyuma ya ushindi kuna kushindwa, kushindwa, kushindwa. Utajifunza mengi kuhusiana na ushindi na dhana ambazo watu wengine wamejenga kuhusiana na ushindi kwenye maisha. Pengine kati ya vitabu vifupi ambavyo tumeongelea mpaka sasa hivi hiki ndicho kitabu kifupi kuliko vyote ila chenye mambo makubwa ndani yake.

Mawasiliano ya kupata kitabu hiki hapa Ni 0755848391

5. DIP cha Seth Godin

HIKI ni kitabu kingine kifupi ila chenye mambo makubwa pia ndani yake. Mwandishi wa kitabu hiki ameeleza safari ya mafanikio kwa ufupi na kwa nini watu wengi hushindwa kufikia mafankio makubwa maishani. 

Mwandishi anasema kwamba kabla ya kufikia mafanikio makubwa hapa katikati kuna bonde (dip) ambalo mtu anaenda kukutana nalo. Na hili bonde lazima tu utakutana nalo bila kujali umetokea kwenye hali gani au umekuwa mtu namna gani. Sasa kwa kuwa watu wengi huwa hawapendi kupitia katika shida na kuanguka basi huwa wanajikuta kwamba wanaogopa kuendelea kuchukua hatua na hivyo kuishia njiani huku wale ambao wako tayari kuchukua hatua na kupitia kwenye hilo bonde wakiwa ndio watu ambao mwisho wa siku huja kushinda kwa kishindo.

 

Hivyo, ndivyo vitabu vitano vifupi vyenye ujumbe mzito sana ndani yake. Pengine na wewe unaweza kuwa na orodha ya vitabu vyako vitano vifupi ila vyenye ujumbe mzito ambao mtu anaweza kuufanyia kazi. naomba kujua vitabu vyako vitano ni vipi?

Karibu ili uweze kuweka maoni yako.

 

 

 Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X