Fedha Inaondoa Matatizo? Au Matatizo Yanaondoa Fedha?


“ Tengua kauli, fedha inaondoa matatizo?, matatizo yanaondoa fedha”. Ilikuwa ni kauli ambayo ilisikika kutoka kutoka kwenye kikundi cha watu watano waliokuwa wakiongea na mtu mmoja aliyekuwa ng’ambo ya barabara. Ilikuwa jana jioni wakati nikienda kutuma vitabu pale stendi ya msamvu kuelekea Dodoma.

 

Muda huo nilikuwa na mtu mmoja ambaye nilikutana naye barabarani tukiongea. Kauli hiyo ilitufanya tusitishe mazungumzo yetu ghafla. Baada ya kutembea hatua kama kumi kutoka wale watu walipokuwa yule mtu aliniuliza wanaongea nini hawa mbona siwaelewi. Nikarudia tena kauli ambayo walikuwa wanasema, japo zamu hii niliiboresha kidogo ili rafiki yangu aweze kuilewa haraka. Wanasema hivi “fedha inaondoa matatizo au matatizo yanaondoa fedha”?

Akanijibu, “mbona haina maana yoyote ile?’.hapo ndipo nikarudia kauli kwa msisitizo mkubwa, wanasema hivi, “fedha inaondoa matatizo au matatizo yanaondoa fedha”?

Hapo ndipo aliponielewa na kuitafakari kauli hiyo kwa dakika moja hivi. Kisha akanijibu, “fedha inaondoa matatizo”. Kisha akaendelea kusema, “ukiwa unaumwa ukaenda hospitali kama hauna fedha basi huo ndio mwisho wako”. Moyoni mwangu nilirejea swali la wale watu taratibu, huku nikijiuliza. Hivi hapa ugonjwa sio tatizo ambalo limeondoa fedha. Au fedha ndio imeondoa tatizo.

 

Wakati naendelea kutafakari tulifika eneo ambalo lilikuwa na kiwanja. mbacho kilikuwa kimezungukwa na sheli upande wa kulia huku kikiwa kimezungukwa na hoteli nzuri upande wa kushoto. Yuke mtu alinyoosha kidole chake kuelekea kiwanja kile akasema, “unakiona hiki kiwanja, yaani mwenye kiwanja hiki siku akistuka. Utaona watu wanajenga kitu cha kipekee sana hapa”.

Nakumbuka niliitikia, japo sikumbuki niliitikia nini maana akili yangu ilikuwa tayari inatafakari juu ya fedha kuondoa matatizo au amtatizo kuondoa fedha. Muda huohuo alinyoosha kidole tena kuonesha ng’ambo ya pili. Kisha nikasikia akisema, “unaliona lile sheli”? nikajibu “ndio”. Akasea kuna kipindi kiwanja hicho hapo kilikuwa kichaka kikubwa na nyasi ndefundefu. Ila sasa hivi unaona kitu kilichopo kilivyo cha kipekee.

Niitikia kwa sauti ya kumtaka aendelee kutirika zaidi, ila akawa hajaongeza neno la ziada.

Nilipotafakari kuhusu kile kiwanja, na baadae kuhusu lile sheli ndipo nilipogundua kwamba mwenye sheli alitumia fedha kuleta huduma ya mafuta karibu na watu na hivyo kuondoa matatizo. Kwa hiyo FEDHA INAONDOA MATATIZO.

 

Kuna magari ambayo yalikuwa yanapita yakiwa yamepakiza watu, nilipoyaona yotehayo nikaona wazi kuwa fedha ilikuwa imeondoa matatizo. Maana bila hayo magari watu wangelazimika kusafiri umbali mrefu ila sasa kwa sababu fedha imetumika kununua hayo magari, sasa matatizo ya kusafiri yameondoka.

Fedha inaondoa mtatizo au matatizo yanaondoa fedha? Swali hili lilinijia tena kichwani mwangu wakati nikiwa naagana na yule mtu niliyekutana naye njiani huku nikiingia ndani ya stendi.

Niliendelea kutafakari kauli hiyo wakati huohuo nikawa ninaona watu mbali mbali waliokuwa wamepanga bidhaa mbalimbali. akilini mwangu nilijuwa hawa wajasiliamali wameona tatizo ambalo lilikuwepo na hivyo wamrtumia fedha hiyo kutatua hilo tatizo,na sasa watu wanafurahia huduma zao.

Hivyo mwisho wa siku nikawa nimeona kwamba fedha inaondoa matatizo ambayo watu wanayo badala ya matatizo kuondoa fedha.  Kinyume chake ni kuwa matatizo yanaleta fedha maana inaonekana fedha zinajificha nyuma ya matatizo.

 

Ebu subiri kwanza, wewe unasemaje? Fedha inaondoa matatizo au matatizo yanaondoa fedha?

 

jipatie nakala ya kitabu cha maajabu ya kuweka akiba kwa shilingi elfu nne tu. tuma fedha kwenda 0755848391 jina GODIUS RWEYONGEZA ili kupata kitabu hiki hapa. baada ya hapo nitumie ujumbe.



Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X