Haya Ndio Maajabu Ya Zama Tunazoishi


Habari ya siku hii ya kipekee rafiki yangu. Karibu sana kwenye makala hii ya kipekee sana. Leo hii tunaenda kujifunza maajabu ya zama hizi ambazo tunaishi. Na maajabu haya ni kuwa mteja anaweza kukuacha wewe hapo kwa kubonyeza mara moja tu na kwenda sehemu nyingine.

 

Ni wazi kuwa tupo kwenye zama ambazo biashara niyingi zipo mtandaoni. Kama wewe hujaweka biashara yako mtandaoni basi unapaswa kuanza siku ya leo kwa kuhakikisha kuwa una BLOGU.  Kitendo cha kuwa na biashara nyingi mtandaoni kinampa mteja mwanya wa kuwa na uhakika wa kuchagua biashara ambayo anataka yeye. Sio lazima biashara yako. Na kitu kimoja ambacho mteja anaweza kufanya ni kukukimmbia wewe kwa kubonyeza mara moja tu kwenye simu au kompyuta yake.

 

Hivyo unachopaswa kufanya kwenye zama hizi ni kuhakikish kwamba unakuwa na bidhaa bora na zenye uhakika kwa ajili ya mteja wako.

Usikubali mteja wako akimbie kutoka kwako kwa kubonyeza mara moja tu.

Jiulize kama wewe ungekuwa ni mteja wako wewe mwenyewe ni vitu gani ambavyo ungependa kupata kwenye hiyo biashara yako. Kisha fanya vitu hivyo kwa wateja wako.

 

Unawez pia ukawa na utaratibu wa kuongea na wateja wako kujua wanataka nini? na kitu gani ambacho hawataki. Kisha wape kile ambacho wanataka.

 

Mwisho kabisa unapaswa kufahamu kuwa kuna kipindi ambacho wateja wenyewe wanaweza kuwa hawajui wanataka nini. wewe hapo ukakaa, ukafikiria na kuona kitu ambacho wateja wako wanahitaji. Hivyo ukawa umekileta na bado kikwasaidia zaidi.

 

Rafiki yangu, epuka sana wateja kukukimbia kwenye zama hizi hapa kwa sababu tu kubonyeza mara moja kwenye simu au kompyyuta zao.

 

Asante sana, kila la kheri.

 

Ni, mimi Godius Rweyongeza

MOROGORO


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X