Hivi Ndivyo Unavyopishana Na Gari La Mshahara Kwenye Zama Hizi Za Taarifa


Rafiki yangu bila shaka siku ya leo ni siku njema sana kwako. karibu sana kwenye makala ya siku hii ya kipekee na leo kuna vitu viwili vikubwa. Kwanza nitekueleza kidogo historia ya binadamu alivyopitia kwenye zama mbalimbai na jinsi ambavyo kila zama ilikuwa na madhara yake.

Pili nitaeleza kiundani kuhusu zama tulizomo sasa  hivi na jinsi ambavyo umekuwa unapishana na gari la mshahara?

Najua shuleni umejifunza kuhusu historia ya binadamu. Umejifunza kuwa binadamu alipitia kwenye vipindi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na zama za mawe, zama za chuma, baadae zama za viwanda. Je, sasa hivi nikiuuliza tupo zama gani unaweza kunijibu?

Karibu sasa iili tuweze kuendeea rafiki yangu.

 

Ni kweli dunia imepitia kwenye zama mbalimbali. Na kila zama ilikuwa na nyezo yake muhimu ambayo ilikuwa inaitofautisha na zama nyingine.

Kwenye zama za mawe, kitu kikubwa ambacho binadamu alikuwa anatumia kilikuwa ni JIWE. Mtu yeyote ambaye alikuwa na jiwe,huyo ndiye alikuwa ana uwezo wa kupata chakula kwa wakati na chakula cha kutosha. Naweza kusema kuwa wajasiliamali wa zama za mawe walikuwa ni wale ambao wanamiliki mawe. Na kama mtu alikuwa na jiwe lilichongoka zaidi basi huyo alikuwa amefikia hatua kubwa zaidi.

 

Kwenye zama za chuma, kitu kikubwa kenye zama hizi hapa kilikuwa ni CHUMA. Mtu yeyote ambaye alikuwa anamiliki chuma, alikuwa ana uwezo wa kupata chakula kwa wakati. Na hata kama ingekuwa ni kulima basi kwake kulima kwake kulikuwa ni rahisi sana, kwa sababu alikuwa na chuma. Mwenye chuma alikuwa anafanya uwindaji kwa uzuri zaidi, mwenye chuma alikuwa ana uwezo wa kujilinda na adui na kufanya shughuli nyinginezo. Naweza kusema kuwa wajasiliamali wa zama za chuma ni wale ambao walikuwa wanamiliki vyuma

 

Baada ya hapo, dunia ilipitia kwenye zama za viwanda. Viwanda vilikuja na mageuzi makubwa. viwanda viliwatengeneza matajiri. Na kwa mara ya kwanza kwenye historia ya binadamu, viwanda vilianzisha mfumo wa kazi, ambao ndio unatumika mpaka sasa hivi. Mfumo ambao unamfanyia kazi mtu na huyo mtu anakulipa mshahara  mwisho wa mwezi au mwisho wa wiki/siku. Haya yote yalijitokeza kwenye zama za viwanda.

 

Kitu kikubwa zaidi kwenye zama za viwanda ni kwamba mtu yeyote ambaye alikuwa na kiwanda, huyo ndiye alikuwa na uwezo wa kutegeneza utajiri mkubwa. Na kwenye zama hizi hapa ambapo dunia imewashuhudia watu kama Rockefeller, Andrew Carnegie,akina Schwab na wanamapinduzi wengine wa viwanda wengi wa wakati huo.

Kipindi hiki watu walitengeza fedha kwa viwango vikubwa, kwa kutumia viwanda. Hata hivyo kulinganisha na zama nyingine, zama hizi zilikuwa na changamoto kwa mtu mmoja mmmoja ambaye  alipenda kumiliki kiwanda.

Ilikuwa ni gharama kubwa kutengeneza nakuanzisha kiwanda. Hivyo wachache tu ndio waliweza kutengenea viwanda na kuviendesha

 

Hata hivyo kila chenye mwanzo huwa hakikosi kuwa na mwisho. Zama za viwanda  zilifikia mwisho na kuja zama za taarifa ambazo ndizo tulizo nazo sasa hivi.

Zama za taarifa zimepitia katika vipindi viwili mpaka sasa hivi. Hata hivyo, kwa leo nitajikita zaidi kwenye kipindi cha pili ambacho kinatuhusu zaidi, ambacho ni kipindi ambapo sisi kwa pamoja tunaishi.

 

Rafiki yangu, kama unavyoona zama zimebadilka. Maisha nayo yamebadilika. Hivyo ni juu yako kubadilika mara moja ili kuweza kuendana na hali hii ya  mabadiliko.

Tumeona mpaka sasa hivi kuwa kwenye kila zama kuna kitu ambacho kilikuwa kinawafanya watu watu waishi maisha mazuri au kutengeneza fedha. Kwenye zama za mawe, jiwe ndilo liliwafanya watu waishi maisha mazuri

Kwenye zama za chuma, CHUMA ndicho kiliwafanya wale waliokuwa nacho waishi maisha mazuri na kutengeneza fedha

Kwenye zama za VIWANDA, kiwanda ndicho kiliwafaya watu waishi maisha mazuri na kutengeneza fedha. Sasa kwenye zama za taarifa, kinachowafanya watu waishi mazuri na kutengeneza FEDHA ni TAARIFA.

 

Unaweza kuwa unajiuliza hii ndio nini? Rafiki yangu, kama ambavyo unaona siku hizi jinsi mambo yalivyo. Mtu akiwa anahitaji kujua kitu chochote kile, hatua ya kwanza kabisa anayofaya ni kuingia kwenye mtandao wa GOOGLE na kutafuta hicho kitu. Huko analetewa majibu yake kulingana na swali ambalo ameuliza. Majibu yake yanaweza kuwa yameandaliwa kwa mufmo wa makala kama hii au kwa mfumo wa video kwenye mtandao wa YOUTUBE. Mtu akishajifunza na kupata jibu la swali lake, kinachofuata ni yeye kuchukua hatua ili kufanyia kazi kile alichojifunza. Au anachukua hatua kumtafuta aliyeandika hilo andiko ili aweze kupata msaada zaidi.

 

Tuseme mkulima wa MAHINDI ndiye ameingia mtandaoni akitafuta mbegu bora za mahindi na ambazo zinakomaa mapema. Anatafuta hiyo mbegu mtandaoni, na kukutana na blogu ya ambayo imeandika hicho kitu kiundani. Kwenye hiyo blogu anaelezwa aina mbalimbali za mahindi. Lakini humo humo kwenye aina hizo anakutana na aina moja ambayo ina sifa zilezile alizokuwa anataka yeye. Inakomaa mapema, inastahimili ukame na inatoa mahindi mawili yanayofa kwa ajili ya kuchoma au kusagwa unga.

Sasa kwa sababu mkulima ameikubali hii mbegu, kinachofuata ni kumtafuta mtu ambaye anauza hiyo mbegu.  Hivi unadhani ni mtu gani anaweza kuwa anajua mbegu hii inauzwa wapi? Bila shako lolote lile mtu huyu ni mwandishi wa andiko lile ambalo mkulima amesoma. Hivyo kitu ambacho mkulima atafanya ni kumtafuta mwandishi wa andiko hilo akitaka kujua zaidi kuhusu hiyo mbegu, na kujua wapi anawezakkupata mbegu zake kupanda. Sasa unadhani kama yule mwandishi wa andiko lile ana mbegu nini kitatokea? NI MAUZO TAYARI YAMEFANYIKA.

 

Hivi ndivyo biashara zinazofanywa kwenye zama hizi za TAARIFA. Tofauti na zama za viwanda ambapo umiliki wa viwanda ulikuwa ni wa watu wachache, kwenye zama za taarifa, hakuna mtu ambaye anaweza kukuzuia kupata taarifa unayotaka. Kila mtu ana taarifa sasa hivi. Kikkubwa uwe na simu au kompyuta.

Lakini si kila mwenye taarifa hiyo ananufaika nayo, kama ambavyo kila mwenye kiwanda alikuwa ananufaika nacho. Naweza kusema kuwa kuna sayansi ndogo tu ya kunufaika na hizo taarifa ulizonazo. Na sayansi hii inaanza kwa wewe kutentengeza BLOGU AU TOVUTI.

Ukiwa na BLOGU yako, utakuwa unaweka maandiko, picha, video au hata mafunzo ya sauti kwenye blogu hivyo utajenga jukwaa ambalo watu mbalimbali watakuwa wanakuja kujifunza na kuchukua hatua.

 

Kati ya hao watu ambao wanajifunza, ndio utakutana na watu ambao watapenda kujifunza zaidi. Kati ya hao wanaojifunza ndio utakutana na watu ambao watakukwa tayari kununua huduma zako kama vitabu, mafunzo au nyimbo zako za CD, utakutana na watu watakaohitaji ushauri zaidi wa mtu mmoja mmoja au kikundi.

 

Lakini ni ukweli kwamba watu hawa hawataweza kukupata wewe, kama hutaweka kitu chako mtandaoni ili siku wakikitafuta wakuone wewe. Na usispofanya hivyo, basi ni wazi kuwa utapishana na watu wanaoitafuta bidhaa zako.

 

KWA NINI BLOGU NA SIO UKURASA WA FACEBOOK AU INSTAGRAM?

Rafiki yangu, unaweza kuwa unajiuliza swali la aina hii hapa. ukasema kuwa mimi nikishakuwa na ukurasa wa Facebooka basi unanitosha.

Blogu ni bora  mara 1000 zaidi kuliko kurasa hizo. Kwa nini?

1. Kwa sababu mtu unapotafuta kitu google, anayependelewa na kuoneshwa akiwa wa kwanza ni mtu wa blogu na sio kurasa za facebook. kurasa zitaoneshwa mara ya kwanza kama hakuna mtu wa blogu ambaye ameandika kitu cha ainahiyo.

2. blogu ina mpangilio mzuri wa kutunza kumbukumbu zako. Hivyo hii inakusaidia hata kumwelekeza mtu aweze kusoma zaidi maandiko ya nyuma.

Tuseme kwamba wewe unafundisha watu kuhusu ufugaji wa samaki. Sasa, wakati unaanza mafunzo yako

·         Siku ya kwanza umeandika kuhusu ufugai wa samaki ni nini?

·         Siku ya pili umeandika kuhusu mambo ya kuzingatia kwenye ufugaji wa samaki

·         Siku ya tatu ukaandika kuhusu bwawa la samaki na vitu ambavyo unapaswa kuzingatia kwenye bwawa

·         Siku ya nne ukazungumzia makosa ambayo watu hufanya kwenye bwawa la samaki

·         Siku ya tano ukazungumzia sehemu ambapo unaweza kupata samaki wa kuweka kwenye bwawa lako

·         Siku ya sita ukazungumzia vyakula vitano muhimu kwa samaki anapokuwa bwawani

·         Siku ya saba ukazungumzia, matumizi ya dawa kwenye bwawa la samaki

·         Siku ya nane ukazungumzia umuhimu wa wataalamu kwenye ufugaji wa samaki

·         Siku ya tisa ukazungumzia, mambo ya kuzingatia kwenye samaki wanapoanza kukomaa

·         Siku ya kumi ukazungumzia kuhusu soko la samaki na jinsi ambavyo unaweza kulifikia kirahisi

Sasa unaweza kuona hapa. inawezekana wewe upo siku ya kumi unaandika kuhusu masuala ya SOKO LA samaki mtu ambaye alikuwa hajakujua akaja na kuuliza swali linaoendanana na somo la siku ya kwanza. Ukiwa na blogu ni rahisi sana kumpatia kiunzi na kumfanya asome hapo kisha atakupa mrejesho.

 

3. ukiwa na blogu unaweza kuweka kiunzi cha somo la awali kwenye somo linaloendelea sasa hivi. Kitu hiki hakiwezekani kwenye kurasa za mitandao mingine.

Kwa mfano wetu hapo juu wa ufugaji wa samaki. Tuseme siku ya saba  wakati unazungumzia juu ya matumizi ya dawa kwenye bwawa la samaki ukakumbuka kuwa kuna kitu cha muhimu ambacho mtu anaweza kusoma kwenye somo la TATU na kikamsaidia, unaweza kumwelekeza mtu huko akasome andiko la somo la tatu.

 

4. blogu inakunfanya ufanye vitu kitaalamu, na hata watu wanaokutafuta wanakutafuta kama mtaalamu. Ebu turudi kwenye mfano wetu wa mfugaji huyo wa samaki. Nadhani baada ya kusoma masomo yake hayo 10 hata kama unampgia simu, huwezi kumpgia simu kama mtu wa kawaida. Lazima utamtafuta kama mtaalamu ili aweze kukusaidia kwenye ufugaji wa samaki.

 

 

Rafiki yangu, unaweza kuona wazi jinsi ambavyo blogu inafanya kazi na kwa mfumo huu unaaweza kuona wazi ni kwa jinsi gani unaweza kuiweka biashara yako mtandaoni. Ni wazi kwamba mtandao intaneti unazidi kuwa na watumiaji zaidi kila siku. Na hapa Tanzania takwimu zinaonesha, watumiaji wa mtandao wa intaneti wanaongezeka.

 

Sasa ni juu yako kuhakikisha kwamba unaweza biashara yako, ujuzi wako, kipaji chako, na elimu yako mtandaoni. Ili hata kama watu wanakutafuta basi wasianze kukutafuta kama wanavyomtafuta mbuzi (samahani). Wakutafute kwa njia ya kidigitali. Hahah!

Ikitokea mtu anatafuta mtaalamu wa kilimo basi wewe unakuwa mtandaoni na ni rahisi kwake kukuona na kuchukuka mawasiliano yako mkafanya kazi.

Kama mtu anatafuta hadithi nzuri, basi akiingia google hadithi yako itokee aione na aweze kuichukua.

 

Rafiki yangu, kuna mengi sana ninaweza kuongelea kuhusu mabadiliko ya intaneti. Nitaendelea kukujuza mara kwa mara. Kwa leo tu ningependa uchukue hatua moja muhimu sana. ANZISHA BLOGU LEO. Basi

Kwa kufanya hivi utakuwa umefanya kitu cha kishujaa sana kwenye zama hizi za taarifa.

Kama utapenda nikusaidie kutengeneza blogu ya kitaalamu, basi unaweza kuwasiliana nami, kwa kupiga 0755848391. Nitakutengenezea blogu ya kitaalamu kwa elfu 30 tu za kitanzania.

RAFIKI YANGU, WEKA HISTORIA LEO. Anzisha blogu na ingia kwenye mtandao rasmi. Kila la kheri

,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X