Hili hapa ndio wazo bora la Kibiashara Kwa Mwaka 2020. Fanyia Kazi Wazo Hili Hapa Tu, Utakuwa Na Mwaka Wenye Mafanikio Makubwa Sana


Kama mpaka sasa hivi umekuwa unajiuliza ni wazo gani bora la mwaka 2020 ambalo unaweza kufanyia  kazi na kupata mafanikio makubwa basi leo nimekuja na suluhisho. Na suluhisho iko wazi kabisa. yaani hadi mwenyewe utashanga kwa nini hukujua suluhisho hili mapema. Ila uhakika ni kwamba ukilifanyia kazi wazo hili ndani ya mwaka huu mmohja tu, basi nina uhakika  mwishoni mwa mwaka huu utakuwa tayari umekuwa mtu mwingine kabisa.
Kwa hiyo kama mwaka huu bado hujapatwa wazo bora la biashara basi wewe tulia tu maana leo nina suluhisho. Lakini hata kama bado una biashara, wazo hili linakufaa pia.


Wazo bora la mwaka 2020 ni LILE AMBALO UTAWEZA KULIFANYIA KAZI kila siku kwa siku 365. Hili ndilo wazo bora kabisa.
Ngoja mikwambie kitu. Wazo huwa haliwi zuri kabla ya kulifanyiwa kazi. Wazo huwa linakuwa bora wakati linafanyiwa kazi au baada ya kufanyiwa kazi.
Kuna siku Chinua Achebe aliulizwa, hivi ulikuwa unajua kuwa kitabu chako kitakuwa kitabu bora cha nyakati zote? alisema sikujua ila kwa wakati huo hicho ndicho kilikuwa kitu ambacho nilipaswa kufanya.
Mwaka 2008 Kelvi Kelly aliandika makala ambayo ilisambaa mtandaoni na kuwa maarufu sana. Baadae alikuja kuandika kitabu kutokana na hiyo makala kilichouza sana. Baadae alikuja kuulizwa, hivi ulijua kuwa andiko lako hilo lingekuwa andiko bora sana. Alisema, sikujua, ila kwa wakati huo hicho kilikuwa ni kitu cha kipekee ambacho ningeweza kufanya.
Kwa hiyo tunaweza kusema kwamba wazo bora huwa haliwi bora mpaka pale unapokuwa umelifanyia kazi na kulikamilisha. Ni wazi kwamba kitabu cha Chinua Achebe kisingekuwa maarufu kama asingekuwa ameweza kufanyia kazi wazo lake na kulikamilisha.
Hakuna aliyejua kwamba iPhone ingekuwa wazo bora. ila baada ya Steve Jobs kulifanyia kazi na kulikamilisha lilikuwa wazo bora. Hakuna aliyejua kuwa magari ya Tesla yatakuwa bora ila baada ya kufanyiwa kazi na kukamilishwa ndio yakawa maarufu.
Hakuna aliyejua kwamba google itakuwa kampuni  bora sana. ila wazo la Google lilipofanyiwa kazi likawa wazo bora sana.
Kwa hiyo kama unataka kujua wazo bora mwaka huu 2020 basi lifanyie kazi wazo lako hilo kazi kwa siku 365. Nina uhakika ndani ya kipiindi hiki tutakuwa tayari na uhakika wa kwamba wazo lako ni bora sana.
Nimeona niseme kitu hiki mapema leo, maana kuna watu wanakuwa na mawazo ya kuanzisha vitu vikubwa ila hawachukui hata hatua ya kwanza. Kuna watu wanakuwa na mawazo ya kuanzisba biashara kubwa kila siku wanasema kwamba ninataka nifanye kitu fulani ila bado hawachukui hatua. Na hata wewe unayesoma hapa, endapo hutafanyia kazi wazo ambalo unalo leo hii. Nina hakika mwakani tarehe kama hii uutakuwa bado hivyo hivyo ulivyo hapo. Ila ukiamua kulifanyia kazi leo hii, basi nina hakika kufikia mwakani tarehe kama hii utakuwa umeweza kufika hatua kubwa sana ambayo ulikuwa hujafikiria wewe mwenyewe.
Kwa hili nakubaliana na Dr. Myles Munroe ambaye aliwahi kusema kwamba, sehemu tajiri sana hapa duniani  sio kwenye machimbo ya dhahabu kule Afrika Kusini. Wala sio kwenye kwenye visima vya mafuta kwenye nchi za uarabu, na wala sio kwamba utajiri upo kwenye nchi zenye gesi. Ila utajiri mkubwa sana umelala makaburini. Huko ndiko kuna watu wengi ambao walikuwa na vipaji na mawazo makubwa ila hawakuyafanyia kazi. Huko ndipo kulikuwa na watu waliokuwa na mawazo mazuri ya muziki ila hawakuwahi kuimba, huko ndiko kulikuwa na watu ambao walikuwa na ndoto za kuwa viongozi wakubwa wa nchi ila hawakuwahi hata kuthubutu kuchukua fomu za kugombea. 
Sasa hiki ndicho kitu ambacho kitatokea kwako endapo hutafanyia kazi wazo lako mwaka huu. Endapo hutafanyia kazi wazo lako mwaka huu basi mwaka huu utaisha   na wewe bado utakuwa bado hivyo hivyo na utaendelea kuishi maisha yale yale uliyokuwa unaishai kila siku.
Je, una wazo gani ndani ya mwaka huu? Ebu nenda sasa hivi ukalifanyie kazi sasa hivi ninapoongea  na wewe ili uweze kunufaika na wazo hili hapa
Katika makala ijayo nitakueleza sababu za kwa nini unapaswa kufanyia kazi wazo lako mwaka huu na sio wakati mwingine.
Tafadhali, usikose kutembelea blogu ya songembele kwa ajili ya kujifunza kila siku.
Kama bado hujajiunga na kundi la think big for Africa unaaweza kunitumia ujumbe wasapu kwa nambari hii 0755848391 ili nikupe utaratibu wa kujiunga huku.

KAMA BADO HUJASUBSCRIBE UJAJIUNGA KWENYE CHANNEL YANGU YA YOU TUBE BONYEZA HAPA
https://www.youtube.com/channel/UCRGDR3d_Pt-TeRxSlF3ORzQ kisha USUBSCRIBE kwa ajili ya video mpya za kila siku.

SOMA ZAIDI:  TOO BUSY TO WATCH YOUR DREAM; Hatua Sita Za Kutana na Watu Maarufu,  Wafanyabiashara Wakubwa Na Wanamziki Nguri Bila Kutumia Nguvu Kubwa


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X