Watanzania Tujenge Utaratibu Wa Kukubali Vitu Vyetu.


Juzi nilikuwa kwenye daladala nasoma Kitabu cha  JINSI YA KUTOKA UMASIKINI MPAKA MAFANIKIO cha Erick Shigongo. Mara alijitokeza jamaa ambaye alikuja kukaa pembeni mwangu. Baada ya kuwa amekaa na kutulia, jamaa akawa ameona Kitabu nilichokuwa nasoma. Akaniomba akione. Sikuwa mchoyo, nikampa. Baada ya muda akanirudishia Kitabu changu.  Nikakawa nasikiliza kwa umakini ili nisikie atakachosema. Ila jamaa alikaa kimya.

Baadae nilimuuliza ili nijue kitu gani kilimvutia kuniomba Kitabu na pia nilitaka kujua kama huwa anasoma Vitabu. Nilichokisikia ni mshangao mtupu!

Jamaa: “mimi huwa nasoma ila sisomi vitabu vya kitanzania”!
Mimi: “Eh kwa nini”? Niliuliza kwa mshangao!

Jamaa: “Kwa sababu watanzania wengi wanakopi na hawajui kuandika”

Nilicheka kimoyomoyo. Nikamuuliza ebu niambie Vivtabu gani vya kiingereza ambavyo umewahi kusoma! Jamaa akaanza kujing’atang’ata. Alikuwa hata haelewi Kitabu gani. Baada ya muda akawa kama amekumbuka kitu. Akasema “kitabu cha Ben Carson ila sikumbuki kichwa chake”. Alisema.

Kwa upande wangu sikushangaa kumsikia mtu huyu anasema kwamba watanzania hawajui kuandika. Sikushangaa kabisaaa! Maana ni kawaida ya watanzania wengi kuvikataa vitu vyetu ambavyo tunavyo.

Sikushangaa maana hata kuna asilimia kubwa sana ya watanzania wanaikataa ligi kuu ya Tanzania kwa kisingizio kwamba wanapenda ligi ya ulaya.
Sikushangaa pia kwa sababu kuna watanzania wanasema wapo bongo kwa bahati mbaya.
Sikushangaa kwa sababu kuna watanzania wanasema bora wangezaliwa kama mbwa ulaya.
Sikushangaa maana kuna watanzania wanakataa kununua bidhaa zilizozalishwa Tanzania na kukimbilia za nchi nyijgine

Kwa hiyo nilijua kwa hakika huyu naye ni mmoja kati ya hao watu.

Nipende tu kusema kwamba watanzania tujenge utaratibu wa kupenda vitu vyetu. Binafsi kwa upande wa vitabu ninapenda zaidi vitabu vya kitanzania kuliko vitabu vilivyoandikwa na mtu wa nchi nyingine.

Nipende tu kusema kwamba watanzania tujenge utaratibu wa kupenda vitu vyetu.

Tupende tulipozaliwa maana kuna kusudi maalumu la sisi kuzaliwa tulupozaliwa leo.

Wahenga wanasema mtu kwao.  Tafadhali sana, jijengee utaratibu huu.

Nakushukuru sana kwa kuweza kusoma andiko hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri

Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391




One response to “Watanzania Tujenge Utaratibu Wa Kukubali Vitu Vyetu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X