Ifahamu Kanuni Ya Kaizen Kutoka Kwa Wajapani


Japani ni miongoni mwa mataifa ambayo kiteknlojia limeendelea. Taifa hili kutoka mashariki kuna kipindi lilikuwa ni taifa la kawaida sana (masikini). Ila baadae uchumi wake ulianza kukua kwa kasi kiasi cha mataifa mengine kuogopa. Je, ni kitu gani kililifanya taifa la Japani kukua kwa kasi kiasi hicho?

Ni kanuni moja inayojulikana kama kaizen. Kanuni ya kaizeni inasema kwamba hakuna kitu kilichokamilika. Hivyo kila kitu kinapaswa kufanyiwa mabadiliko. Kanuni hii inaendelea kwa kuweka wazi kwamba mabadiliko hayatokei kimapinduzi bali hutokea kwa mfumo wa ukuaji kila siku. Hivyo kama kuna kitu chochote ambacho unafanya leo,  jitahidi ukifanye kwa ubora zaidi kila siku. Kila siku tafuta kitu kipya cha kuboresha na kufanya kwa ubora zaidi.

Kama kila siku utapata kitu kimoja tu cha kufanyia kazi basi mwishoni mwa mwaka utakuwa umefanya mabadiliko 365. Haya sio mabadiliko ya kimzaha mzaha.

Mabadiliko haya lazima yatakusogeza kwenye viwango vingine vya ubora.
Kwa hiyo hakikisha kila unapoenda kulala umekuwa bora zaidi ya ulivyokuwa ulipoamka asubuhi.  Kuwa bora zaidi kwenye maeneo ya kiuchumi, kwenye maeneo kimahusiano, kwenye uuzaji, kwenye ubunifu, kwenye pesa na mambo mengine.

Soma Zaidi; Hili Ni Jambo Ambalo Linaendelea Kukuweka Hapo Ulipo

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


One response to “Ifahamu Kanuni Ya Kaizen Kutoka Kwa Wajapani”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X