ZAMA ZIMEBADILIKA-3


Mwaka 1982 Buckminster Fuller alianzisha kitu kinachojulikana kama  Knowledge Doubling Curve. Katika mchoro huo Buckminster alionesha kwamba mpaka mwaka 1900 maarifa yalikuwa yanaongezeka mara dufu kila baada ya miaka 100.

Ila ndani ya miaka 45 kufikia mwaka 1945 maarifa yalikuwa yanabadilika kila baada ya miaka hamsini.

Sasa tumefikia kiwango ambapo maarifa yanabadilika kila baada ya miezi 12 tu. Siku si nyingi yatakuwa yanabadilika kila baada ya saa kadhaa.

Hii ndio kusema kwamba maarifa ambayo siku za nyuma kidogo ungeweza kuyasoma/ kujifunza na ukayatumia mwaka mzima, siku si  nyingi utakuwa unayasoma yanatumika kwa saa chache sana kabla ya kupoteza thamani yake.

Hii ni kutokana na ugunduzi mkubwa sana ambao unatokea kwenye sekta ya sayansi na teknolojia, matibabu, kilimo n.k
Yaani hakuna sekta ambayo imelala. Na kwa sasa wastani Wa mabadiliko katika kila sekta ni miezi 13. Yaani kwamba ukijifunza kitu kwenye sekta fulani baada ya miezi 13 basi tayari kinakuwa kimepitwa na wakati!

Ukitaka kujua hili anza kufuatilia mfumo wa mabadiliko ya simu na magari. Simu ambayo ilikuwa inaonekana ni ya kisasa/kijanja mwaka 2016, njoo nayo leo afu uanze kujidai kwamba ndio simu bora, watu watakucheka sana! Hii ni kutokana na ukweli kwamba sasa hivi kuna simu bora zaidi ya hizo ambazo zimegunduliwa.

Napenda sana maneno aliyosema Alvin Toffler, katika kitabu chake  cha The Future Shock (1970), anasema, “mjinga wa karne ya 21 sio yule ambaye hajui kusoma na kuandika, bali yule ambaye hawezi kujifunza, kuachana na mambo ya zamani na kujifunza mambo mapya”. Kwa hakika ZAMA ZIMEBADILIKA.

Kinachoendelea kwenye zama hizi ni kwamba maarifa yanaongezeka kwa kiwango kikubwa sana (knowledge is doubling exponentially) wakati kiwango cha matumizi yake pia kinashuka kwa kasi. Kwa hiyo sasa kikubwa kwenye zama hizi ni wewe kuwa mtu wa kutafuta maarifa muda wote. Maana kwenye zama hizi hauchelewi kuzeeka, kupitwa na wakati na kuwa mtu ambaye hana thamani kama utaacha kutafuta maarifa mapya kila siku.
🔥Tafuta maarifa kupitia vitabu,
🔥Tafuta maarifa kupitia semina,
🔥Tafuta maarifa kupitia watu unaokutana nao au kuongea nao.

Yaani hakikisha unatafuta maarifa na kutafuta maarifa kwelikweli.

Inaendelea…..

Siku si nyingi sana kuna mtu ambaye alihitimu na akawa anahudhuria semina nyingi, anasoma tafiti na kusoma vitabu. Mtu huyu alikuwa tayari kulipia semina hata kama ingekuwa ni gharama kiasi gani. Yeye usemi wake ulikuwa ni kwamba, kama ninalipia kiasi kikubwa ila ninajifunza kwa mtu mwenye ujuzi mkubwa sana, sijapoteza. Mtu huyu alikuwa daktari. Hivyo alizunguka nchi nyingi sana akitumia kila senti ya mshahara wake kujifunza. Kila aliposikia kwamba kuna ugunduzi umefanyika sehemu hakuwa mtu ambaye alipenda kuachwa nyuma na ugunduzi huu, badala yake alitaka kujua ni nini kinaendelea…

Siku moja alihudhuria semina na kujifunza kitu kidogo sana kwenye matibabu ya macho. Kitu hiki kilibadili maisha yake yote. Alikuja kuwa mtaalamu mkubwa sana. Watu kutoka kila kona ya nchi walikuja kwake kutibiwa macho. Ilifikia hatua ambapo matibabu ya macho yakawa yanahusishwa na jina la daktari yule. Yaani kama ungeumwa jicho ukawa hujatibiwa na daktari yule basi wewe ulikuwa bado hujapona. Kitu hiki kitufunze  kubadilika kadri zama zinavyobadilika.

Sasa ebu tuone hadithi ya tofauti kidogo.
Mtu ambaye amejifunza kompyuta miaka ya 1970 na tokea hapo hataki kujifunza mambo mapya, hivi unafikiri mtu huyu yuko wapi sasa hivi.
Je, bado ana ustadi wa kazi wa kuendana na zama za sasa?

Kwa hakika,
ZAMA ZIMEBADILIKA, MAISHA YAMEBADILIKA, ajira hatarini. Ebu na wewe badilika.

Kwa hakika ZAMA ZIMEBADILIKA
Maisha nayo pia yamebadilika

Sasa ni wakati wako kubadilika.

Imeandikwa na
GODIUS RWEYONGEZA
0755848391
www.songambeleblog.blogspot.com

*RASMI SASA:* kitabu cha ZAMA ZIMEBADILIKA, kitazinduliwa rasmi tarehe 15/4/2019 asubuhi na mapema sana!

Kitabu kitaanza kupatikana kwa soft copy kwanza.

Bei itatolewa baadae


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X