Unapaswa Kuwa Na Uwezo Wa kutenganisha Kitu Hiki Na Biashara Yako


Rafiki yangu, hongera sana kwa nafasi nyingine ya kuishi. Leo hii ni siku ya kipekee sana.
Swali la kwanza unalopaswa kujiuliza siku ya leo?
Nimepewa uhai tena ili nifanye nini?

Swali la pili je, nitafanya nini leo kitakachoongeza thamani kwa watu, ndani ya siku ya leo?

Kumbuka kwamba kila siku ni siku yako wewe kukua na kuhakikisha unasonga mbele.

Kitabu Cha Kabla Ya Kuanzisha Biashara Kipo Kwa Ajili Yako
Tsh.5000/

Sasa leo napenda ujue kitu kimoja ambacho unapaswa kukitofautisha  na biashara yako.

Ukiweza kutofautisha kitu, hiki utakuwa umejua vizuri namna ya kuishi na utaweza kusonga mbele zaidi.

Kitu hiki sio kingine bali ni kujitofautisha wewe hapo pamoja na biashara yako. Yaani wewe ni wewe na biashara ni biashara.
Hiki ni kitu muhimu sana ambacho napenda ukifahamu.
Na vitu hivi, havina uhusiano.

Soma Zaidi: Jambo Moja Litakaloikuza Biashara Yako Bila Ukomo

Ukiweza kufanya hivi maana yake hata kwenye biashara yako hutatoa tu pesa ili mradi umetoa, kama mmiliki. Badala yake utafuata taratibu.

Ukifanya hivi utaweza kuishi pia maisha na familia yako vizuri. Maana tatizo la watu wengi ni kwamba wanapenda kuonekana ni wakurugenzi hadi kwenye familia.
Wakati watu hawa kwenye familia zao  ni baba, ni mama, ni mke au ni mme.

Usipotofautisha vitu hivi viwili, utaishi kama mkurugenzi nyumbani na watoto pamoja na familia haitakuelewa.

Kwa hiyo mimi nakuomba ufanye yafuatayo.
Mosi, muda wa kazi uache uwe muda wa kazi. Hapa hakikisha unafanya kazi za kiofisi na biashara zako.

Pili muda wa familia uache uwe muda wa familia, hapa usilete ukurugenzi wala unani nani?

Tatu, weka mfumo unaoeleweka ambao haukuruhusu wewe kuchukua pesa moja kwa moja kutoka kwenye biashara. Sio kwa sababu wewe ni mmiliki basi unatoa tu pesa kwenye biashara na kutumia utakavyo. Kuwa na mfumo.

Kumbuka biashara ni biashara na wewe ni wewe.

Nne, weka mfumo unaoeleweka wa maamuzi kwenye biashara. Maamuzi haya yahusishe watu  unaofanya nao biashara.

Rafiki yangu,  kuanzia leo, unapaswa kujitenganisha wewe na biashara yako.

Soma Zaidi: NYUMA YA USHINDI

Asante sana

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X