Ukisikia Fulani Ni Kiongozi, Basi Jua Anafanya Hivi


Hongera sana rafiki kwa siku hii njema sana ya leo.
Leo ni jumamosi ya tarehe 06 oktoba 2018.
Ni siku ya kipekee sana ambayo unapaswa kuitumia kuhakikisha unaweza kufikia ndoto zako.

Kwa sasa hivi nafundisha sana masomo ya uongozi, na makala zangu nyingi zijazo mbali na kwamba nitaongelea vitu vingine lakini suala la uongozi nitaliongelea kwa undani zaidi.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba watu wengi wanatafsiri vibaya neno uongozi.
Wapo wanaosema kwamba kuwa na cheo tu, inatosha kukufanya wewe kuwa kiongozi.

Lakini ninachoamini ni kwamba uongozi sio lazima uwe na cheo. Uongozi sio lazima uwe na madaraka.

Leo napenda nikwambie kwamba ukisikia watu wanasema fulani ni kiongozi, basi jua kwamba yeye ana uwezo wa kushawishi kupitia matendo, wala sio maneno au siasa.
Kiongozi ni yule mtu ambaye anaweza kutangulia mbele ya kundi la watu, nao wakawa tayari kumfuata nyuma yake. Huyu ndiye kiongozi.

Kwa hiyo bila kujali nafasi, cheo au madaraka yake, kiongozi ana uwezo wa kuwafanya watu wamfuate nyuma yake hata kama hana madaraka na vyeo vikubwa. Haya ndio maajabu ya uongozi. Kwa hiyo ukisikia watu wanasema kwamba fulani ni kiongozi, basi angali hizo sifa.

Jiangalie, pia na wewe. Je, unao udhubutu wa kutangulia na watu wakakufuata?
Kama jibu lako ni ndio basi upo kwenye kundi hili, sasa ni juu yako kujiendeleza na kujifunza zaidi kuhusu uongozi

Soma Zaidi: Kitu Hiki Ndicho Kinapaswa Kukusukuma Kuwa Kiongozi 

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA

,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X