UCHAMBUZI WA KITABU: THE WEALTH OF NATIONS Utajiri Wa Mataifa


Ukurasa 17-27

Habari ya siku hii njema rafiki yangu.  Kuna nyakati huwa zinakufanya unakuwa na maswali mengi sana na pengine hupati kabisa majibu ya maswali haya.
Mimi ni miongoni mwa watu wenye maswali mengi sana ambayo huwa najiuliza ila kadri ninavyosoma vitabu ninapata majibu na kunufaika na majibu hayo.
Mfano baada ya kukua na kuona jinsi watu wa rika langu wanavyooa na kuolewa, ila wanaachana ndani ya miaka michache na wengine ndani ya miezi michache. Nilianza kujiuliza kwa nini ndoa nyingi hazidumu? Kwa nini watu wengi wanaingia kwenye mahusiano kwa furaha ila wanakuja kuachana kwa vilio vikuu? Je, inawezekana mtu kutengeneza mahusiano yakadumu milele?

Soma Zaidi: UCHAMBUZI WA KITABU CHA THE ALCHEMIST

Katika kutafuta majibu ya hayo maswali niliwauliza wazazi, ndugu jamaa na marafiki ila sikupata jibu la uhakika. Ndipo katika kusoma vitabu nilikutana na kitabu vha WHY MEN WANT SEX AND WOMEN NEED LOVE (kwa nini wanaume wanapenda ngono na wanawake wanahitaji upendo). Hapa nilipata zaidi ya majibu niliyokuwa najiuliza.

Sio hilo tu, kuna kipindi nilikuwa najiuliza inakuwaje watu wanatengeneza pesa mtandaoni. Je, kwa nini baadhi ya watu ni matajiri na wengine masikini? Je, kwa nini baadhi ya watu wanafurahia maisha na wengine wanalia japo wapo kwenye eneo moja? Nilishangaa sana, ila katika kutafuta mtandaoni nilikutana na blogu ya AMKA MTANZANIA ambayo ilijibu asilimia kubwa sana ya maswali yangu. Nikakutana pia na vitabu vingi sana ambavyo vimenipa majibu na ninayafanyia kazi. Kama wewe pia una maswali kama haya, tayari nimekuandalia kitabu, kinachojulikana kwa kichwa; *”KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI.”*

Hata hivyo bado nina maswali mengine bado sijapata majibu yake ya kunitosheleza na hivyo wewe ukiweza kunisaidia kupata majibu au kupata vitabu vyenye majibu, nitafurahi sana.  Miongoni mwa maswali hayo ni
Kwa nini watu wanakunywa pombe? Kuna nini katika pombe kinachowafanya watu waendelee kunywa bila kuacha? Je, ni kitu gani kinaweza kunishawishi mimi kunywa pombe? Na maswali mengine ya namna hiyo. Je, unayo majibu? Tuwasiliane.

Sasa kitabu cha WEALTH of NATIONS ndio nimeanza kukisoma ila kwa utangulizi niliouona, naona kabisa kwamba kinaenda kujibu swali langu ambalo nimekuwa najiuliza, JE, NI KITU GANI KINAFANYA MATAIFA KUWA TAJIRI NA MENGINE MASIKINI? Japo kila mtu anaweza kuwa na majibu yake kulingana na uelewa wake kwa wakati husika, basi sasa tuone mwandishi ‘ADAM SMITH’ anasemaje juu ya swali langu na mengine zaidi yaliyo kwenye kitabu chake 

1. Mataifa matajiri yametengeneza utajiri wake kutokana na mgawanyo wa kazi. Ambapo sio mtu mmoja anayefanya kazi kubwa peke yake, hapa watu wengi wanashirikiana kufanya kazi ndogo ndogo ila kwa kuziunganisha zinatengeneza kazi kubwa zaidi ambayo hata mtu mmoja hawezi kufanya kwa siku au wiki.

2. Mataifa yaliyoendelea huyazidi mataifa jirani, katika kilimo na viwanda. Lakini huwazidi sana majirani kwa viwanda

3. Kadri nchi inavyoendelea kwenye viwanda ndivyo na kilimo chake kinaendelea na kuwa bora zaidi lakini wakati huo huo kufanya nchi hiyo iwe na uwezo wa kuzalisha chakula kwa bei nafuu sana kulinganisha na nchi masikini.

4. kutokana na kuboreshwa kwa mashine ya utendakazi kwenye nchi tajiri, mtu mmoja anaweza kufanya uzalishaji mkubwa sana kwenye eneo kubwa, kitu kinachozidi kupunguza bei ya bidhaa za kilimo zinazozalishwa na nchi tajiri.

5. Kadri mtu anavyokuwa anajishughulisha na kazi moja ndivyo anakuwa mtaalamu kwenye hiyo kazi, kiasi kwamba anaweza kufanya kazi kubwa sana kwa siku moja ukilinganisha na mtu anayetanga tanga kila siku akifanya kazi hii na ile.

6. Lakini pia, mtu anapokuwa na kazi moja maalum anapunguza muda wa mizunguko ya kutoka eneo moja kwenda jingine na hivyo kuongeza uzalishaji mara dufu

Soma Zaidi: IFAHAMU NGUVU YA KUTOA NA JINSI UNAVYOWEZA KUITUMIA KWA MANUFAA YAKO

Uchambuzi huu utaendelea kukujia kwa awamu kwa siku kadhaa zijazo.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X