UCHAMBUZI WA KITABU CHA WEALTH OF NATIONS-5 (Mwanzo Wa Hisa)


Utajiri wa mataifa
Ukurasa wa 50-53
Mwanzo wa Hisa
Kadri ninavyoendelea kusoma kitabu hiki hapa, ninaendelea kugundua jinsi ambavyo mataifa yaliweza kujitengenezea utajiri na kufika yalipo. Kuna vitu vingi sana vya kujifunza kwenye kitabu hiki hapa.
Moja ya maswali ambayo nilikuwa najiuliza hivi hisa zilianzaje?
Maana sasa hivi utasikia watu wanasema, nimenunua hisa za Vodacom. Au mwingine utasikia anakwambia hisa za CRDB zimepanda/zimeshuka bei? Sasa ilikuwaje kuwaje hadi watu wakaanza kuwa na mfumo huu wa hisa?
Mfumo huu wa hisa umekuwepo kwa kipindi kirefu sana. Yaani sio kwamba umeanza jana. Umeanza kitambo sana.
Kwanza kabisa tuelewe msingi mkuu wa hisa, ili tuweze kuendelea vizuri.
Msingi wa hisa umelala kwenye kukusanya nguvu kutoka kwa watu wawili na zaidi, ambapo watu hawa huchanga pesa kwa pamoja ili kuanzisha au kukuza biashara.
Sasa msingi huu wa kuunganisha nguvu haujaanza leo. Ulianza zamani sana. Kuna kipindi baadhi ya watu walikuwa wanamiliki ardhi kubwa sana. Na watu hawa walijulikana kama mabwana (landlords).
Sasa kwa mtu ambaye hakuwa na ardhi kama angetaka kulima, alikuwa anafanyaje?
Hapa alikuwa anapaswa kwenda kwa bwana (landlord) ili apewe ardhi ya kulima.
Ila kwa  kupewa kwake ardhi hiyo, wakati wa mavuno kuna kiasi alipaswa kukirudisha kwa bwana wake, aliyempa ardhi.
Sasa hapa ndipo tunaona kwa mara ya kwanza suala zima la hisa linazaliwa.  Naona umefunguka juu ya hili hapa na umefurahi kweli😀😀😀
Vizuri kabisa. Tuendelee kuwa pamoja.
Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X