Je,Upo Tayari Kupoteza? Utapoteza Nini Sasa?


Katika maisha ya sasa hivi kuna vitu ambavyo ukiviongelea utaonekana umeweuka au umepoteza mwelekeo.

Miongoni mwa vitu ambavyo ukiviongelea utaonekana wa ajabu ni KUPOTEZA.
Ili uweze kutoka sehemu ulipo na kwenda hatua ya ziada lazima ukubali kupoteza.

Unashangaa! Huu ndio ukweli ambao lazima uukubali!

Ili uweze kuruka na kufika mbali lazima  kuchuchumaa kwanza.  Kama uko na Mimi mpaka hapo utakubaliana na mimi kwamba kuchuchumaa ili uruke ni KUPOTEZA.

Unahitaji kupoteza simu (yaani uiuze) ili upate mtaji.
Unahitaji kupoteza facebook ili upate mtandao mkubwa zaidi wa watu.
Unahitaji kupoteza….ili upate….

Soma Zaidi  Kama Ningekuwa Wewe Ningefanya Hivi

Je, wewe lengo lako ni kupata nini?
Je, upo tayari kupoteza?
Utavpoteza nini?

Miongoni mwa watu ambao mimi nawapenda sana, na ni mfano mzuri katika kupoteza ni MATHAYO.
Ukisoma kitabu cha Mathayo 9:9-13
Utagundua Mathayo alipoteza. Mathayo aliitwa na Yesu ili amfuate. Alipoteza. Hakuna mafanikio bila kupoteza.

Mathayo alipoteza ila alipata sana.
Alipoteza kazi nzuri lakini alipata majaliwa na kudra za mola.
Alipoteza pato zuri lakini alipata heshima
Alipoteza usalama wa kiuchumi lakini alipata maisha yenye usalama wa na matukio mazuri
Alipoteza vitabu vya ushuru akapata kuandika Kitabu cha injili ya mathayo.
Alipoteza vitu akawapata watu

Kamwe asingeweza kupata vitu hivi kama asingekuwa tayari kupoteza.

Kumbe na wewe kubali kupoteza ili upate zaidi.

hivi hapa ni vitu vitano ambavyo unahitaji kuvipoteza haraka sana ili upate zaidi.

1. Poteza Muda wa kuangalia TV
Je, kwa siku unatumia masaa magapi kuangalia TV? Kubali kupoteza.
Punguza muda wako wa kuangalia Tv sasa ili uweze kupatamuda zaidi wa kusoma vitabu. Muda zaidi wa kufanya shughuli za kukuza uchumi wako.
Poteza tv upate muda wa kukuza mahusiano yako.
Usiendelee kung’ang’ania vipindi vya TV ambavyo haviongezi thamani kwako. Ng’ang’ania mafanikio.
Poteza TV upate zaidi.

Kwa lugha nyingine suala hili la poteza upate tungeweza kulisema kwa lugha kama hii. MWAGA ILI UJAZWE, NA UJAZIWE ZAIDI.

Soma zaidi. Kosa Moja Unalopaswa Kuepuka

2. Poteza Mitandao.
Unatumia masaa mangapi kwenye mtandao kila siku? Je, unapoamka asubuhi kitu chako cha kufanya ni nini? Je, ni kuchukua simu na kuangalia kitu gami kinaendelea facebook?
Je, ni kusoma mtandao wa udaku?
Kitu unachokifanya mtandaoni kina faida gani kwako na na kwa watu wengine?
Poteza hayo yote ambayo unafurahia kwenye mtandao ili uwze kupata zaidi.
Poteza sasa ili ufurahie keaho yako bora.
Kama kuna kitu unakilalamikia siku hii ya leo bila kuchukua hatua. Hakuna mbinu ya tofauti ya kupata kile unacjokitaka kama kupoteza Sera za kulalamika.

Wewe Ni Zaidi Ya Ulivyo Sasa,
Wewe Ni Zaidi ya ulivyo sasa.
Kujiunga na kundi la wasp la HAZINA YETU BONYEZA HAPA
Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
www.songambeleblog.blogspot.com
Ili kupata kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI  tuwasiliane kupitia 0755848391

Bonyeza hapa ili uweze kupata makala maalumu kila wiki.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X