Nijibu SMS 1000 Au Nisome Kurasa 1000? Ipi Bora? Nifanye Ipi?


Habari za siku ya leo rafiki yangu.

Binafsi naipenda sana mitandao ya kijamii. Inaniunganisha na watu ambao kama isingekuwapo basi ingekuwa vigumu kwangu kuonana nao.

Mitandao ya kijamii inanifanya najifunza na kusoma zaidi;

Inanifanya nijenge heshima yangu na mambo mengine mengi kutaja ila machache.

Soma zaidi; Vitabu Vitatu Vya Kusoma Kabla Mwaka Huu Haujaisha

Ujio wa mitandao hii umewafanya watu wengine wafaidike huku wengine wakiharibiwa na mitandao hii.

Kumekuwa na kasumba hii ya kuchati na kupost mitandaoni na kuchangia mada kwa mara kadri zinavyowekwa mitandaoni. Hali hii imewafanya watu wengi kupoteza muda.

Si hilo tu, hata umakini wa kazi unazidi kupungua. Unakuta unaongea na mtu yeye anachati.

Au umeenda ofisini, kule unakuta skretari yuko bize na kuchati au bosi mwenyewe yuko bize anachati. Tabia hii inazidi kukua na inazidi kuambukizwa kwa wototo na wajukuu wetu.

Soma zaidi; Hii Ndiyo Siri Ya Ilyonyuma ya neno Kuwa Updated

Ambacho huwa kinanishangaza sana na ndicho ningependa kukazia leo. Ni pale unapomwambia mtu kusoma kitabu akasema hana muda. Laikini hapo hapo unasikia akisema “jana nilikuwa na SMS 1000. Nimezitumia zote tena ndani ya SAA 1″. Tena mtu huyo anzidi kujidai kwamba “mimi SMS 1000 kwangu ni kidogo sana. Yaani hizo nazitumia tu kwa watu wachache na siridhiki”

Hapo ndipo huwa nashangaa unatoka wapi muda wa kuchati na kukosa muda wa kusoma kitabu?

Kama unapenda sana kuchati na bado unasingizia huna muda wa kusoma kitabu unadanganya.

Warren Buffet aliwahi kunukuliwa akimwambia kijana mmoja kwamba kama anataka kuwa kama yeye basi asome karatasi za A4 500 kila siku.

Na ili uweze kusoma karatasi hizi basi unapaswa kuondokana na falasafa ya sina muda.

Lakini ebu kwanza tujiulize?
Je ni lazima kutuma sms 1000 na zaidi kila siku?

Je, kati ya hizi sms 1000 ngapi ni za kibiashara?

Je, wale unaowatumia sms wanakujua wewe kama nani?

Kama unahisi kutuma sms 1000 na zaidi kila siku ni kitu damu damu na wewe basi nakushauri uishie hapa. Ili yule mwenye mapenzi ya kujifunza tuweze kwenda sawa.

Si lazima kutuma sms hizi zote. Na ukiwafuatilia watu wengi utagundua asilimia kubwa ya sms wanzotuma si za kujenga. Wala si za kukutoa SIFURI kwenda KILELENI.

Jumbe hizi mara nyingi si za kujenga.

Swali;
Nijibu SMS 1000 Au Nisome Kurasa 1000? Ipi Bora? Nifanye Ipi?

 Kumbe badala ya kujidai kwamba wewe ni bingwa wa kuchati na kutuma jumbe za papo kwa papo. Jidai kwamba wewe ni msomaji maarufu wa kurasa za vitabu. Jidai kwamba unaweza kusoma kitabu kizima na kukimaliza kila siku.

Soma Zaidi; Kitu Hiki Kitakunyima Ajira Kama Bado Unatembea Na Cheti

Jidai kwamba unaweza kusoma Kurasa 1000 kila siku.

Badala ya kujihangaisha na vocha iliyoisha huku ukiwaza utapata wapi Vocha nyingine ili ujibu sms, jihangaishe na kwamba kitabu kimeisha, sasa utasoma kitabu gani kingine!

Angalizo. Kama wewe huwa unajidai kwamba unatuma zaidi ya sms 1000 na zaidi kwa siku badilika.
Ukikutana na mimi jitahidi kujizuia wala usithubutu kuniambia hivyo. Sitakuvumilia. Lazima tu, ndio lazima tu sitakuvumilia.
Soma vitabu zaidi
Peruzi kwenye Kurasa za vitabu
Soma kuhusu pesa
Soma juu ya kile unachofanya.
Soma vitabu zaidi ya unavyochati.

Soma! Soma! Soma.

Chukua hatua sasa
Wewe Ni Zaidi Ya Ulivyo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X