Habari za rafiki yangu na msomaji wa blogu yako ya songa mbele karibu sana katika makala leo ambapo tunaenda kujifunza kitu kipya kwenye maisha yetu.
Mara nyingi huwa tunajiuliza tuanzie wapi, tufanye nini?
Tunaangalia fursa hatuzioni.
Kwa leo ningependa kujibu swali hili la nitaanzia wapi na kutoa jibu na mbinu ambazo zitakusaidia kupata wazo la biashara au njia ambayo utaitumia kufikia mafanikio.
1. Tafuta kalamu na karatasi, tafuta sehemu ambayo imetulia ambapo hatutasumbuliwa.
2. Jiulize Je, nina hali gani sasa?
Andika chini kila wazo ambalo linakuja akili mwako sasa. Majibu yako yasiwe marefu na magumu.
Unaweza kusema sifurahii kazi yangu! Nahitaji kujitegemea.
3. Je, nina ujuzi gani? Je, raslimali gani ambazo ninazo na zipo kwenye mazingira yangu? Jibu maswali hayo vizuri.
4. Je, nautumiaje muda Wangu vizuri?
Andika vile ambavyo unavyotumia ndani ya siku husika ikiwemo muda wa kula, kulala, na mapumuziko n.k.
5.Je, ni huduma gani naweza kutoa kwa jamii yangu?
6. Je, msaada gani naweza kupata kutoka kwa wazazi Wangu au familia?
7. Andika hapa kitu ambacho utakifanya.
andika sentensi yako kwa mfumo huu
KUFIKIA…….. MIMI……..(jina)NAAMUA KUFANYA YAFUATAYO…………..KWA KUTUMIA RASLIMALI ZIFUTAZO………
Hiyo ndiyo sehemu muhimu sana ambavyo unaweza kuanzia kwa sasa.
Ni sehemu ambavyo inaweza kukutoa moja mpaka kileleni?
Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA