Mambo matatu Ambayo Kampuni Yako Inapaswa Kuwa Nayo


Habari za leo rafiki na ndugu msomaji wa SONGA MBELE BLOG . Imani yangu unaendelea vyema katika hatua ya kutafuta na kuelekea mafanikio.Karibu sana katika makala yetu ya leo ambapo tunaenda kujifunza kitu kipya ambacho kitabadili mwelekeo wa maisha yetu



Kampuni yeyote ili iweze kukua na kufikia hatua sana inahitaji walau kuwa na vitengo hivi vitatu ambayo ni ya muhimu sana. Vitengo hivi ni uzalishaji, utafiti na masoko.

Bila uzalishaji basi hapo  kampuni haiwezi kuwa na kitu cha kuuza, bila bila masoko kampuni haiwezi kuendelea na uzalishaji. Na bila utafiti basi kampuni itapoteza matumaini ya kusonga mbele na kuendana na hali ya mabadiliko yanaoendelea katika dunia hii.

 Hivi vitengo tunaweza kuviita kuwa ni  kichwa mikono na miguu ya kampuni. Tunaweza kusema kichwa kinasimama badala ya utafiti na mikono inasimama badala ya uzalishaji na miguu inasimama badala ya mauzo. ukiondoa kiungo chochote kati ya hivi basi umepoteza mwelekeo wa kampuni, kama ambavyo ukikata viungo hivi kwa binadamu na humpa maumivu na uchungu. hivyo hivyo ukiondoa kimojawapo kati ya hivyo basi utaifanya kampuni iwe na maumivu na uchungu.

Soma zaidi hapa; Huu ni utumwa ambao kila mmoja anapaswa kuuepuka

 Je, kuna ulazima wa kufanya utafiti kampuni ? Kiukweli uatafiti katika kampuni unafanyika kwa malengo mawili ambayo ni maendeleo  ya sasa ya kampuni na maendeleo ya baadae. yaani utafiti unafanyika ili kufanya ukuzaji wa uzalishaji wa bidhaa za sasa na ma uzalishai wa bidhaa za baadae. Wakati utafiti wa sasa unaendelea uzalishajii wa sasa hausimami bali unaendela kwa kasi ya hali ya juu sana.

kiufupi kampuni inakuwa na mambo  mawili ya kuweka maanani hali ya  sasa na hali ya baadae. Hali ya sasa itaonesha ni kwa jinsi gani kampuni inaendelea , katika uzalishaji, uuzaji na hali ya kipesa ya kampuni.  kitu cha msingi cha kujiuliza katika hali ya sasa ya kampuni ni kujiuliza, Je mimi ningekuwa mwekezaji ningewekeza katika kampuni hii? Hapo utaweza kupata mwanga mkubwa sana na kuona kama ungeweza kuwekeza au la!  Na kama ungeweza kuwekeza kwa nini au kama  usingeweza kuwekeza kwa nini? Hili swali ni la muhimu sana rafiki na unahitaji kulisoma na kulielwa zaidi na zaidi, ma jiulize swali kila siku asubuhi unapoamka na na jioni kabla ya kulala.

Kama kampuni yako haifanyi vizuri usihofu sana rafiki maana sasa ndio muda wa wewe kulifanya kampuni lako liwe bora sana na lenye manufaa na likuletee mabadiliko unayotaka ili baadae uweze kuyafurahia.

Kwa nini makampuni yanapenda kuendelea kukua hata kama yanafanya vizuri kwa sasa? 
Sheria inayofanya kazi kwa viumbe wengine ndiyo inayofanya kazi kwa makampuni mengine pia na ni sheria hiyo hiyo inafanya kazi kwa binadamu. Sheria inasema kwamba “a body tends to remain  in its own state of motion unless an external force is applied”

Kitu chcochote huendelea kukaa  katika hali yake ya kawaida  mpaka pale kani ya nje inapokuwa imetumika.

kampuni inayokua itapenda kuendelea kuwa katika hali yake ya ukuaji mpaka pale kani ya ziada kutoka nje itakapojitokeza na kampuni inayokufa itaendelea kukaa katika hali yake ya ziada mpaka pale kani ya nje itakapojitokeza
vivyo hivyo  hata wewe mtu binafsi. Siku zote utapendelea kuona unaendelea na kupiga hatua moja mbele au kusonga mbele, hakuna anayefurahia kukaa bila kusonga mbele, kampuni ambayo haikui ni sawa na kampuni ambayo imejiwekea kitanzi na inataka kujiangamiza. Meneja wa kampuni lazima alifahamu hili na alipe uzito mkubwa sana ili kampuni izidi kusonga mbele.

Endelea kusoma makala za kuelimisha na kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii

Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
0755848391
godiusrweyongeza1@gmail.com
Asaante


BIDEISM BLOG


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X