Habari za leo rafiki na ndugu msomaji wa
SONGA MBELE BLOG . Imani yangu unaendelea
vyema katika hatua ya kutafuta na kuelekea
mafanikio.Karibu sana katika makala yetu ya
leo.
Je, nawezaje kuondokana na umaskini wa kipesa? Je nawezaje kuingiza pesa kwenye mzunguko ikawa msaada mkubwa kwangu? Siku zote pesa haionekani kutosha. Kuongezeka kwa mshahara hakuonekani kuondoa matatizo ambayo mtu anayo. Kuna mtu aliwahi kusema “mahitaji yako huongezeka kuendana na mshahara wako.”
Sehemu ya kipato chako hutumika kununua chakula na hivyo kiasi hicho ni cha mkulima au muuzaji wa chakula gengeni. Nyingine hutumika kununua nguo na hivyo kiasi hicho ni cha mwenye duka, nyingine hutumika katika afya kumbe kiasi hicho ni cha daktari au mtalaamu wa afya. Kingine unakitumia katika uasafiri na hivyo kiasi hicho ni cha konda. Mambo mengine ambayo hutoa na kupeleka pesa yako kutoka mfukoni ni elimu na mawasiliano.
Je wewe ya kwako inaendaje?
Hii ndiyo sababu inayonipa ujasiri wa kusema jilipe mwenyewe kwanza sehemu ya kipato unachoingiza.
Katika hali kama hiyo tuliyoina hapo juu ina maana mtu utaishia kufanya kazi kubwa sana lakini kipato unachopata kinashibisha tumbo na kinachukuliwa na wengine.
Je nitawezaje kujilipa mwenyewe na ninapaswa kujilipa kiasi gani? soma zaidi makala hii ina maelezo ya swali hili. Siri Ya Babilon Kuwa Mji Tajiri Kuliko Yote Duniani
2. Ongeza uwajibikaji wako
Je akiba yako unaifanyia nini? Najua kuna baadhi ya watu ambao wakiwa na pesa mfukoni hawatulii mpaka pale watakapokuwa wameitumia yote imeisha. Na mwingine anapokuwa na pesa ananunua chochote kinachokuja mfukoni mwake. Bila kujali kimo kwenye bajeti au la. Je wewe ni mmoja wapo? Huu ni ugonjwa ambao kila mtu anapaswa kupambana kuutibu mpaka pale utakapopona
Usiongozwe na majirani au marafiki katika matumizi. Yaani usifanye kile unachoona wanafanya. Unanunua gari au friji au kabati au meza kwa sababu jirani, rafiki, dada, kaka, mjomba au mtu yeyote wa karibu kanunua?. Nunua kwa sababu kimo kwenye bajeti. Amua kuitumia vizuri kila sarafu na iangize ikufanyie nini? Najua wengi chenji ianyorudishwa baada ya kununua kitu huwa inaonekana haina maana sana. Hakikisha hauipotezi hii.
Soma zaidi hapa; Wafanyabiashara waliofanikiwa wanavyotunza muda
3. Chagua uwekezaji sahihi.
Baada ya kujilipa mwenyewe kiasi fulani baada ya muda fulani utagundua kwamba akaunti yako inaanza kutuna. Unachohitaji kujua ni kwamba pesa siku zote lazima iwe katika mzunguko na unahitaji pesa ikufanyie kazi. Siri ya mafanikio ni kuwa na pesa inakufanyia kazi.
4. Ifanye nyumba yako iwe sehemu ya kukuingizia kipato.
Nampenda sana Robert Kiyosaki mwandishi wa kutabu cha RICH DAD POOR DAD ambaye ameeleza vizuri sana ni lini nyumba yako inakuwa raslimali na kini nyumba yako inakuwa dhima.
Siwezi kusisitiza kwamba unapaswa kuwa na nyumba yako nzuri na ya kuishi ila anachokisema Kiyosaki ni kwamba unapokuwa na nyumba yako mwenyewe ya kuishi haikupi faida yoyote bali itakachokifanya ni kuondoa sehemu ya kipato chakk na na kukitumia kulipa kodi, umeme na mengine.
Kiyosaki anashauri ununue raslimali kabla ya kununua au kujenga dhima kama nyumba ya kuishi. Raslimali utakayonunua ndiyo itakayogharamia nyumba ambayo utaijenga au kununua.
Kwa wale ambao tayari wana nyumba unaweza kufanya moja kati ya haya au yote kwa wakati mmoja.
- Weka bustani mbele ya nyumba yako ambayo itakuingizia kipato cha kuendeshea nyumba lakini pia itakupa chakula.
- Toa sehemu ya nyumba au vyumba ambavyo huvitumii na uvipangishe vikusaidie kuingiza kipato.
- Unaweza pia kuamua kufanya uwekezaji kwenye nyumba yako mwenyewe mfano unaanzisha duka au kitu kingine ambacho unafikiri unaweza kuwekeza.
Soma zaidi hapa; Zifahamu Njia Za Kuifanya Pesa Ikufanyie Kazi