Tabia Tano(05) Zitakazokufanya uwe na Maisha ya Furaha


Sote tunahitaji kuwa na maisha bora na  furaha kwenye maisha yetu. Lakini  huwa tunakutana na vikwazo na matukio ambayo hutufanya tusiwe na furaha.
Mambo hayo yanaweza kuwa kushughulika na watu wabaya, kufanya kazi maeneo tusiyoyataka na mipango kutokamilika. Hayo na mengine mengi huweza kutuondolea furaha, kuridhika na kuharibu mtazamo wa akili  zetu

Kuna uzoefu mbaya wa akili kuweza kutegemea matatizo na kutoridhika pamoja na kuondoa hali ya furaha.
Hii husababisha mtazamo hasi wa akili kiasi kwamba pale tunapokuwa na furaha mtu hutegemea kitu kibaya kutokea na hivyo kuondoa furaha yake.
Ili kuwa mtu mwenye mafanikio lazima kuondoa huu mtazamo hasi na wenye kuharibu.

Mara tunahusisha furaha na mambo ya nje kama vile kutafuta upendo na kwenye starehe.
Hivi vitu vinaweza kuleta furaha lakini usivitegemee. Haupaswi kusubiri matukio mazuri yatokee ili uwe na furaha. Unaweza kujihusisha na maksudi katika vitendo ambavyo huleta furaha.

Je, mabadiliko ya mazingira huweza kutengeneza furaha?
Ingawa furaha huonekana kutokea kwenye matendo ya nje ambapo kwa mda wewe huweza kusahau matatizo na magumu yako. Hii hutokea pale unapofanya kitu ambacho wewe unapenda kufanya unapotulia. Hii hutokea pale tunapopata habari njema au kitu kizuri kinapotokea na kuondoa akili yako katika mambo yanayo kusumbua.

Kiukweli furaha hutokea ndani yako na haitegemei watu au matukio. Hii inaanisha kwamba tunaweza kupaya furaha hata kama tunapitia kwenye hali mbaya. Ukiamini tofauti kutaweka akili yako,  furaha na unavyojisikia katika mikono ya watu wengine.

Furaha ni hisia ya ndani, hisia ya kuridhika kukamilika na kutulia. Unapokuwa na furaha hujisikii kuwa na dhiki, hauhofii chochote na haufikrii kitu chochote kibaya.

Nina uhakika umewahi kuwa na furaha katika maisha yako tena mara nyingi. Haijalishi umepitia katika hali gani hata katika hali mbaya lakini bado kuna nyakati za furaha. Unapokuwa na furaha unasahau matatizo yako kwa mda na unafurahia amani ya ndani. Ningependa kukupa baadhi ya tabia ambazo zinzaweza kukupa furaha katika maisha yako.

1.Tafuta furaha katika kitu kidogo kilichokuzunguka.
Usisubirie kitu cha kipekee kutokea, ili uwe na furaha. Mambo ya kipekee hayatokei kila siku lakini kuna mambo madogo ambayo unaweza kufurahia na yapo kwa wingi sana. Hapa kuna baadhi ya mifano.

  • Kusoma kitabu kizuri.
  • Kupata kifungua kinywa kizuri kabla hujaenda kazini.
  • Kutumia mda wako na ndugu zako na uwapendao.
Unaweza kutafuta vitendo vingine ambavyo huleta furaha amani na utulivu na kusahau yote yanayokusumbua.
2. Tafuta muda wa kutulia na kuona mambo ya asili.
Nenda katika hifadhi, fukwe za bahari, mito na maziwa. Ukiwa karibu na mazingira haya utajisikia una amani na utivu ambavyo ni viungo muhimu vya furaha.
3.Furahia maisha na marafiki zako.
Unapokuwa na marafiki, furahia kila dakika ukiwa nao. Furahia amani, upendo na furaha. Washirikishe wenzako hali ya furaha na wasikilize. 
Kama kuna matatizo unataka kuwaambia au kama kuna jambo baya unataka kuwashirikisha basi chagua mda wa kufanya hivyo.
4. Epukana na wivu.
Badala ya kuwa na wivu kwa mafanikio ya watu wengine, hamasishwa na mafanikio yao vutiwa nayo, jitume kujua jonsi walivyofanikiwa na fuata njia zao.
Kuona wivu ni sawa na kuiambia akili yako na ulimwengu kwamba wewe si mshindi bali ni mshindwa. Kushiriki furaha na mafanikio ya watu wengine hukufanya wewe kuvutika ilikupata mafanikio mafanikio na kukuweka katika njia ya mafaniko zaidi.
5. Kuwa mkarimu na wafikrie watu wengine.
Ukiwapokea watu kwa furaha na wewe watakupokea kwa furaha na hiyo itasababisha amani ya ndani na furaha.
Ni mimi rafiki na ndugu yako 
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
Unawwza kuupenda ukutasa wangu wa facebook kupitia   fb.me/songambele


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X