Kupe Hawa Wanne (04) Wananyonya Muda Wako Kila Siku.


Je ni siku gani imekuwa ya matokeo makubwa sana kwako. Je, ni wiki gani imekuwa ya matokeo makubwa sana kwako? Ni mwezi gani umekuwa wa matokeo makubwa sana kwako?

Watu wengi hupoteza mda wao wakifanya mambo ambayo hayaongezi  thamani kwao.

Mambo baadhi ambayo hupoteza mda wako ni intaneti, kujaribu kubadili mambo nje ya uwezo wako, kuongea badala ya kufanya, kuogopa, kusubiri watu wengine wakufanyie, kufikiria mambo ya zamani.
Haya hapa ni baadhi, kati ya mambo machache yanayopoteza mda wako.


1. Mitandao ya kijamii: Watu wengi sasa  wana ulevi wa kimtandao,wanafuatilia mambo mengi sana mitandaoni ambayo hata hayasaidii. Mtu hataki kupitwa na kinachoendelea mitandaoni. Hata mtu akilala, akiamka tu kitu cha kwanza kushika ni simu ili aangalie kitu gani kinaendelea mitandaoni. Anataka ajue nani kapost nini?

Na watu wamesemaje? Anataka ajue picha aliyopost watu wameiongeleaje. Hata kama yuko kazini atataka ajue nini kinaendelea mitandaoni, hii  huweza kupelekea kutofanya kazi kwa ufanisi. Na kupoteza mda.

Ushauri: punguza mda wa kuwa mitandaoni, utumie walau kusoma vitabu kama huna jambo la kufanya. Soma makala za kuelimisha kwenye blogu kama SONGAMBELE BLOG. Iondoe mitandao ambayo haina umuhimu kwenye simu janja yako.

Sio lazima upate notification kutoka kwenye mitandao ambayo utabakiza kwenye simu yako, maana zitasababisha uvutike kuingia mitandaoni.

2. Kuchati: Utasikia mtu anasema “mimi nina uwezo wa kuchati meseji 1000 kwa siku na hazitoshi”
Mwingine anasema “mimi nina uwezo wa kuchati kwenye mitandao mitatu kwa wakati mmoja, nipo facebook, nipo wasapu, nipo instagram, na nina chati kwa meseji za kawaida, na ninawajibu watu wote meseji zao kwa wakati”.  Wote hao wawili wanaongea kama vile kuna mashindano ya kuchati basi mwishoni wataibuka videdea.

Hasha! Sio hivyo! Ni ajabu sana kumwona mtu anaweza kutuma meseji nyingi kiasi hicho lakini bado watu anaowatumia meseji hizo hawajui ni bidhaa gani wanaweza kupata kwake. Au hawajui anajishughulisha na nini?  Je wewe ni mmoja wao?

Je upo kwenye makundi kama nane ya wasapu ila hata hawajui upo duniani hapa unafanya nini?

Ushauri: Badilika sasa! Acha kufuata mkumbo. Sio eti kwa sababu ulimwona fulani anachati basi na wewe unaanza kufanya hivyo.

Utumie huo mda wa kutuma na kujibu meseji kufanya mambo ya muhimu. Fikria ni jinsi gani unataka kuwa badae? Fikria safari yako ya mafanikio inaanza lini?

Fikria nani utaongozana nae kuelekea kwenye  mafaniko? Je safari yako ya mafanikio itaanzia wapi?

Wape taarifa wale unaochati nao kwamba sasa kwako inapatika bidhaa fulani. Wape taarifa za mabadiliko ya huduma zako. Kwa kufanya hivi utakuwa umetendea haki mitandao unayotumia.

3. Kuisubiria kesho.
Acha kuisubiria kesho. Hutakuja kuipata tena leo. Haijalishi umefanya nini zamani. Haijalishi uko chini kimaendeleo au hujioni kuwa na thamani. Ukweli kwamba unaishi kunakufanya kuwa na thamani kubwa sana.

Ushauri: Anza leo kwa kuchukua hatua moja mbele. Kama hauna uhakika ufuate njia gani ni vizuri kuusikiliza moyo wako. Mda haurudi nyuma .  Mda unaopoteza leo hautakuja kuupata tena.

Kumbuka wakati wewe unahangaika kupoteza mda,wapo watu wanahangaika kuyatumia vizuri masaa 24 tuliyopewa sote bure kabisa.

4.Kupigania usahihi.
Kupigania usahihi, sio tu kwamba utachelewa kukamilisha jambo fulani bali pia kutapoteza mda wako ukifikiria jambo gani ni sahihi na jambo gani sio sahihi lakini pia utapoteza mda kabla ya kuanza jambo kwa kuogopa kukosea. Fikria juu ya sheria ya 80/20. ( Asilimia 80 ya matokeo yako inatokana na asilimia 20 ya uwekezaji wako.)

Ushauri: usiogope kufanya kosa, wala usiogope kuanzisha biashara, kwa kuogopa kushindwa. Kuwa tayari kukabiliana na changamoto. Maana katika safari ya Maisha hakuna mafanikio yanayotokea bila changamoto.

Watu waliofanikiwa sio kwamba hawajakutana na changamoto ila ni kwamba hawakuogopa changamoto.

Badilika sasa na chukua hatua za kubadili maisha yako ili uzidi kusonga mbele, maana hakuna mda mwingine wa kufanya hivyo.

Ni mimi ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391.
Asante

Endelea kusoma blogu hii kwa makala zaidi za kuelimisha.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X