Ili ufanikiwe katika biashara unahitaji kutunza mda.Kama hutatunza mda sio tu kwamba utapoteza malengo lakini pia utapoteza wateja,hela,na pia unaweza kupoteza na biashara.
Hapa kuna mambo matatu ambayo unaweza kuchukua ili kutunza mda wako.
1.kuwa na mpango.
Unahitaji kujua kile ambacho unataka kufikia na mda ambao unataka kiwe kimekamilika. Kuwa na mpango kutasaidia sana wewe kufikia malengo yako. Kwa hiyo anza kuandika chini lengo lako na mbinu utakazozitumua kufikia hilo lengo. Jambo hili huonekana rahisi lakini watu wengi huwa hawafanyi hivi,hivyo husumbuka na kupoteza mda mwingi.Nakushauri usifanye kosa kuhusiana na hili suala.
2.Panga Mambo gani yakamikike katika kila hatua
Chukua kila hatua na uwekee hatua ndogondogo ambazo utapitia ili kufikia hatua kubwa.Hii itakusaidia kuifikia kila hatua vizuri na kwa usahihi wa hali ya juu. Lakini pia hukusaidia wewe kutosahau jambo ambalo wewe hukutaka urudi nyuma ili uweze kulisahihisha, kwa sababu kusahihisha kosa kutachukua mda lakini pia kunaweza kuchukua hela.
3.Kamilisha kila hatua
Mwisho unapokuwa unaangalia jinsi ya kutunza mda wako unapaswa kuhakikisha unakamilisha kila hatua na hatua zote ndogondogo. Weka mda flani kila siku kutafakari mpango wako na hatua zako
Angalia ni vitu gani ukifanya na vitu gani hukufanya. Usitake kuwa na haraka maana hakuna kitu kisichohitaji mda kufikia malengo na kukamilika.
Kumbuka kwamba hata ukifikia hatua mbili au tatu kwa siku, hatua hizi hukupelekea kwenye mafanikio.
Wafanyabiashara waliofanikiwa wanajua umuhimu wa kutunza mda na hufuata njia ambayo huwasaidia kufikia malengo yao kwa ubora wa hali ya juu. Lakini pia wanajua umuhimu wa kufanya kazi ili kuweza kufikia malengo yao vizuri.
Kwa kufuata hatua hizo utaweza kufikia malengo yako na kuondoa vikwazo vya mda.
Endelea kusoma makala za kuelimisha na kuhamasisha kila siku kutoka SONGA MBELE
Ni mimi ndugu yako Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391
Asante