ZAMA ZIMEBADILIKA -1


Zama za sasa hivi zimebadilika kabisa. UKitaka kupata matokeo ya tofauti kwenye zama hizi basi Unapaswa kuwa tayari kufanya vitu vya tofauti na vile ulivyozoea. Kiufupi ni kwamba vitu ambavyo vimekufikisha wewe hapo ulipo, havitweza kukusogeza mbele zaidi ya hapo. Kwa hiyo unapaswa kujisukuma zaidi ya hapo, ili uweze kupata matokeo ya kitofauti kabisaa!

Moja ya kitu ambacho Unapaswa kukifahamu kwenye zama hizi ni kwamba hutaweza kufanya kila kazi wewe peke yako. Kuna kazi unapaswa kufanya wewe. Kuna kazi utapaswa kuwafundisha wengine. Kuna ujuzi unapaswa kuwa nao wewe na kuna ujuzi ambao unapaswa kuuelekeza kwa watu wengine wakusaidie ili sasa wewe upate muda wa kushughulika na kazi kubwa zaidi  zinazokusogeza kwenye mafanikio.

Kuna njia nne ambazo unapaswa kuzitumia katika kufundisha watu kitu kipya kwenye zama hizi.

1.  KUKIFANYA KITU MWENYEWE.
Kama una ujuzi kwenye zama hizi na unapenda kuutoa kwa mtu ili awe anaufanya kwa niaba yako, wewe ukiendelea na kazi nyingine. Basi anza kwa kuufanya huku ukimuita mtu huyo ambaye unataka kumfundisha akuangalie unavyofanya.

2. MRUHUSU MFANYE PAMOJA NA WEWE
Akishaona jinsi unavyofanya, hasi kifuatacho ni kufanya kile kitu kwa pamoja.
Ila wewe ndiye unakuwa mtendaji mkuu na yeye anakuwa msaidizi mkuu.

3. KIFANYE TENA KWA PAMOJA
Zamu hii mnaendelea kukifanya kwa pamoja ila sasa yeye ndiye anakuwa mtendaji mkuu na wewe unakuwa msaidizi tu. Pale ambapo utahitajika ushauri ndipo utautoa. Au pale utakapohitajika kufanya kitu ambacho kinaonekana hakieleweki basi hapo ndipo utakifanya.

4. ACHA AKIFANYE
Hapa sasa wewe unaishia kuangalia kinavyofanyika. Tayari umemfundisha mtu, kiasi  anaweza kuendelea na kazi/shughuli hiyo bila hata kuhitaji uwepo wako. Wewe zamu hii unafikiria mambo makubwa zaidi ya kukufanya usonge mbele.

Kwa hakika zama zimebadikika. Na ufundishaji nao umebadilika. Kuna hatua NNE ambazo unapaswa kuzitumia kufundisha / kufundishwa.

Na kama wewe ndiwe unafundishwa basi utapaswa pia kufuata hizi hatua nne bila kuruka hata moja
1. Utapaswa kumwangalia mtu akifanya
2. Utafanya naye (yeye hapa ndiye mtendaji mkuu)
3. Utafanya Naye (wewe hapa ndiye mtendaji mkuu)
4. Utafanya ( yeye ataishia tu kukuangalia).

#ZAMA_ZIMEBADILIKA_KABISA
#MaishaYamebadilika
#AjiraHatarini
#NaWeweBadilika

Kitabu cha rejea: ZAMA ZIMEBADILIKA cha Mwandishi, Godius Rweyongeza

Karibu sana

Imewandikwa na
Godius Rweyongeza
www.songambeleblog.blogspot.com
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X