NGUVU YA NENO: MANENO HUUMBA NA KAULI 101 UNAZOPASWA KUZIEPUKA ILI KUFANIKIWA


UTANGULIZI

Maneno huumba. Ni usemi mfupi wa wahenga ila wenye maana kubwa sana. ni ukweli kuwa maneno yana uwezo wa kuumba kitu chochote. Ukitaka maneno yakuumbie kitu kizuri, basi unaongea maneno chanya. Ukitaka maneno yakuumbie kitu kibaya basi unaongea unaongea maneno hasi. Ni hivyo tu. Sasa kwenye kitabu hiki nimeona nikuletee kauli 101 ambazo unapaswa kuziondoa kwenye kamusi ya maongezi yako. La sivyo kauli hizi hapa zinaenda kukuangusha chini na kukufanya uendelee kupata matokeo mabaya. Kauli zenyewe ni;

1. Kumekucha na makucha yake

Hii ni kauli ambayo Watu wengi huwa wanaitumia katika kuonesha kuwa dunia siyo fair, dunia siyo nzuri na wala haifai. Ukisema kumekucha na makucha yake maana unategemea mabaya yatokee ndani ya hiyo siku, ndio maana unasema kumekucha na makucha yake.

Sasa badala ya wewe kuamka asubuhi na kusena kuwa kumekucha na makucha yake, amka asubuhi na anza kujisemea kuwa leo ni siku nzuri sana. Siku ya Leo ninaenda kufanya makubwa.
Kwa jinsi hiyo utaianza siku yako kwa namna chanya na hata kila utakachokutana nacho utakitafsiri katika namna chanya, tofauti na pale ambapo utaianza siku yako kwa mtazamo hasi, kila kitu kitakachotokea kwako, kitaonekana kibaya.

2. Sina fedha/sina hela

Hii ni kauli ambayo moja kwa moja inakufunga na kukufanya usione upenyo wa kutoka. Ukisema sina hela maana yake unakuwa unainyima akili uwezo wa kufikiri nje ya boksi na kuona fursa gani zaidi unazoweza kupata.

Badala ya kusema sina fedha, unaweza kujiuliza hivi hapa nawezaje kupata fedha? Au ni mbinu gani naweza kuitumia kupata fedha? Ukisema hivi unakuwa umeifungua dunia nyingine ya fursa na kuona vitu ambavyo watu hawaoni.

Kuna misemo ambayo imezoeleka kutolewa na watu siku hizi kiasi kwamba imekuwa ni sehemu ya pili ya maisha ya hawa watu. Unakuta mtu anasema “usawa huu wa Magufuri pesa imekuwa ngumu sana”. Utasikia mwingine anasema “vyuma vimekaza” wakati mwingine akitaka kukwambia kuwa hana pesa basi utasikia akisema, “sina hata mia mbovu”. Yaani kumaanisha kuwa hana kitu kabisa mfukoni mwake.

Ukifuatilia kwa umakini. Yaani kwa jicho la tai anayeuangalia mchezo kutokea juu angani na kutoa tathimini, unaona wazi kabisa kuwa suala la vyuma kukaza sio jambo la leo au jana.  Historia inaonesha kuwa katika kila nyakati kumekuwa na mambo kadha wa kadha ambayo yamekuwa yakitokea na kusababisha vyuma kukaza. Hata hivyo kitu kimoja kimebaki uhakika siku zote. Wale wanaotengeneza pesa siku zote huwa hawaoni kukaza kwa vyuma kama tatizo. Badala yake huwa wanaona fursa kwenye hilo.

Ngoja nikueleze kiundani suala hili ili uweze kunielewa. Kukaza kwa vyuma kama wanavyosema wengine maana yake ni kutokuwepo kwa pesa. Sasa tujiulize ni kitu gani kinakufanya wewe ukose pesa?  Unaweza kuwalalamikia watu wote duniani ila mwisho wa siku mtu anayesababisha kukaza kwa vyuma ni mmoja tu. Na mtu huyu ni wewe.  Hii unatokana na ukweli kwamba pesa inafuata mkondo kwa wale wanaoiita. Kama wewe hauiiti ije kwako haiwezi kuja, utapishana nayo njiani tu.

Leo hii nataka nikuoneshe namna utakavyoiita pesa ije kwako na iendelee kuwa ya kwako milele na milele. Siku nyingine kabla hujasema pesa ni ngumu hakikisha unarudi hapa kusoma andiko hili ili uone Kama umelitendea haki. Ila kama utasoma hapa na kuishia tu kusema kuwa huyu jamaa anaandika vizuri basi mimi nakuhakikishia utaendelea kusema kuwa pesa ni ngumu. Kama utasoma hapa na kufanyia kazi ulichojifunza hapa, basi tutakutana sehemu siku moja ukifurahi kwa sababu ya kile ukichojifunza hapa siku ya leo.

MOJA, KAMA PESA NI NGUMU MAANA YAKE HUJATOA HUDUMA KWA JAMII
Zig Ziglar amewahi kusema kuwa utapata kitu chochote unachotaka kama utawasaidia watu kiasi cha kutosha kupata kile wanachokitaka. Kitu ambacho unapaswa kuelewa hapa ni kuwa kuna watu wana pesa zako mkononi mwao. Ila hizo pesa hazitakuja kwako kirahisi. Labda uwakabe (na ukifanya hivyo jela itakuwa rafiki yako). Ila njia pekee ya kuzitoa hizo pesa kwa watu na kuzileta kwako ni kuhakikisha kuwa una bidhaa ambayo unaweza kuwauzia hao watu. Hiki kitu ndicho Zig Ziglar anakiita kuwasaidia watu kupata WANACHOTAKA.
Kuna watu wanahangaika kwa sababu huduma fulani hawaipati vizuri. Lakini wewe ukiweza kuwafikishia hiyo huduma kwa ustadi watakuwa tayari kukulipa na hiki ndicho Zig Ziglar anakiita kuwasaidia watu kupata WANACHOTAKA.

Kuna watu hawajui kwamba wewe ni mtaalamu na umesomea ujuzi fulani chuoni. Sasa huo ujuzi uliojifunza chuoni ukiweza kuutafsiri na kuuleta kwenye maisha ya kawaida hapa mtaani. Ukautumia ujuzi huo kuwasaidia watu kupata kitu fulani ambacho unaona kitaalamu hakifanyiki vizuri. Hapo utakuwa umewasaidia watu kupata kitu wanachokitaka.

Nikukumbushe kuwa pesa hazitakuja kwako kama wewe utakuwa tu umelala halafu unaishia kusema pesa ni ngumu au vyuma vimekaza. Pesa itakuja kwako pale ambapo utaamua kutatua matatizo ambayo jamii inakumbana nayo.
Muuza maji hapati pesa kwa kuuza maji bali kwa kutatua tatizo lako la kiu.

Mtu daladala hapati pesa kusafirisha abiria, bali kwa kutatua tatizo lako la kusafiri na kufika eneo husika mapema.
Mitandao ya simu haipati pesa kwa kuuza vocha bali kwa kuunganisha na watu walio mbali na wewe.
Wewe unatatua tatizo gani?

Shida yako wewe imelala kwenye  haya maeneo mawili.
Kwanza unaamini kuwa hakuna kitu kingine kipya unaweza kufanya kuondokana na hali hiyo uliyonayo.

Yaani, umejikatia tamaa mwenyewe. Na kama umekata tamaa mwenyewe hata akitokea mtu akakupa mamilioni ya pesa hayatakusaidia. Cha kufanya inuka tena na anza kupambana.

Tatizo lako la pili, unaona kuwa haya ninavyoongea hapa yanawafaa wengine na sio wewe. Huchukui hata hatua ya kuanza, unabaki kusema tu haya yanawafaa watu wenye hela zao bana. Hivi unadhami hao unaosema wana hela zao walizaliwa nazo? Kuna wengine walikuwa na maisha mabaya pengine zaidi ya wewe. Kuna wengine walikuwa na madeni makubwa kuliko hata wewe hapo. Ila walisimama wakabeba majukumu yao na sasa unawaonea gere. Usipochukua hatua UTAJIJU.

2. KAMA PESA NI NGUMU MAANA YAKE UNAWAHUDUMIA WATU KIDOGO

Kiasi cha pesa unachoingiza kinaweza kuniambia ni idadi gani ya watu unaowahudumia. Kama unaingiza pesa kidogo maana yake UNAWAHUDUMIA WATU KIDOGO. Kama kuna kiasi kikubwa unaingiza maana yake unawahudumia watu wengi. Hii wala hata sio hesabu ngumu kama unavyofikiria.

Ebu tuseme wewe na Paulo mnauza maji. Paulo anawauzia watu 1000 na wewe unawauzia watu 100 kila siku na kipimo mnachotumia kuuza ni kile kile, bei pia sawa, unadhani nani atapata pesa zaidi?

Ukiona pesa ni ngumu unapaswa kujua kuwa unawahudumia watu kidogo. Kama umeajiriwa ujue unafanya biashara na mteja mmoja tu ambaye ni bosi wako. Sasa usitegemee ulipwe kwa viwango sawa na mtu ambaye anatoa huduma kwa wateja mia, elfu au laki moja.

3. KAMA PESA NI NGUMU UJUE KUWA HUJAJUA MISINGI NA MIIKO YA PESA.

Ni kawaida kuwa mwanasheria akienda chuoni lazima atafundishwa misingi ya sheria na miiko kwenye sheria. Daktari pia anafundishwa misingi na miiko.

Mwajiriwa kazini ataambiwa mambo anayopaswa kufanya kazini na yale anayopaswa kuepuka. Pesa pia ina misingi yake na miiko yake. Ukiona ni ngumu kwako basi ujue hii misingi hujaijua.
Hujajua kuwa unapaswa kuweka akiba kwa kila kiasi unachopata.
Hujajua pia kuwa unapaswa kupunguza matumizi yako na kubaki na mtumizi ya lazima tu.
Hujajua kuwa unapaswa kuanza kuwekeza ili pesa yako ikuzalie pesa zaidi.
Hujajua kuwa haupaswi kutumia zaidi ya kipato chako.
Hujajua pia kuwa haupaswi kukopa pesa ili utumie ili uje ulipe.
Hujajua pia kuwa mtu akikuahidi pesa, haupaswi kuiweka kwenye hesabu zako mpaka utakapokuwa umeipokea mikononi mwako.

Hiyo ndio misingi ya pesa miiko ya pesa.

HITIMISHO.
Naamini baada ya kuwa umesoma hapa, hutakuja kukosa mia mbovu kuanzia leo. Maana tayari unajua jinsi pesa inavyopatikana mpaka inavyotumika. Nikutakie kila la kheri.


3. Ni Bora kuzaliwa mbwa ulaya

Kuna wanaosema ni bora kuzaliwa mbwa ulaya kuliko kuzaliwa mtu Tanzania/Afrika.

Hiki Ni kiwango cha juu kabisa cha kutojikubali. Usipojikubali wewe unadhani nani atakuja kukubali wewe. Unapaswa kujikubali wewe kwa namna ulivyo.

Nakumbuka miaka kadhaa ya nyuma  kuna mtu wa karibu alinifuata na kuniambia kuwa alikuwa hapendi ufupi aliokuwa nao. Bora angekuwa mrefu kidogo. Niliwahi kuona pia mdada mmoja ambaye alikuwa hapendi mwonekano wa masikio yake. Kitu hiki Ni kibaya Sana. Na kinakufanya ushindwe kufanyia kazi mambo unayoweza kwenye maisha yako.

Upo hapo ulipo kwa sababu maalumu,na kusudi maalumu. Ndio maana umezaliwa sehemu ulipozaliwa, ukaenda kusoma shule uliyosoma, ukakutana na watu ambao umekutana nao. Yote hiyo ni maandalizi ya siku ambapo utapaswa kutumia nguvu na uwezo wako.

Konekisheni unazokutana nazo leo hii ni maalumu kwa ajili ya kuja kukufikisha sehemu fulani, watu unaokutana nao  watakuja kukusaidia ukianza kutumia fursa zilizokuzunguka.


One response to “NGUVU YA NENO: MANENO HUUMBA NA KAULI 101 UNAZOPASWA KUZIEPUKA ILI KUFANIKIWA”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X