Malengo Yako Ya Mwaka 2024 Usimwachie Mungu


Ni mwaka wa tatu sasa tarehe kama ya leo naandika makala  inayosisitiza kuhusu malengo na kwa nini haupaswi kumwachia malengo yako mungu. Mwaka juzi niliandika makala hii hapa. 

Makala hiyo hapo juu ina swali zuri sana ambalo nimekuwa napenda kuendelea kuwauliza watu kila mara.

Na hata juzi nilituma ujumbe kwa watu wa nguvu kupitia whatsap. Ujumbe huu ulikuwa na swali lililokuwa linauliza, umejiandaaje kwa ajili ya mwaka 2024? Lengo lako la mwaka 2024 ni lipi au unamwachia Mungu?

Cha kushangaza ni kwamba asilimia kubwa ya watu walisema kwamba wanamwachia Mungu. Kwa sababu ni mweza yote,

Ni alpha na omega.

anajua kesho yako

anachopanga yeye mwanadamu hawezi kupangua

na mengine mengi.

Ukweli ni kuwa malengo yako haupaswi kumwachia Mungu, japo ana sifa hizo ambazo watu wamekuwa wanatoa, ila ukweli ni kuwa Mungu mwenyewe anakuangalia wewe unavyofanya.

Mungu hawezi kukubariki ukiwa umebweteka, huna malengo, huna mwelekeo wowote, upo tu hapo. kitendo cha wewe kukaa chini na kuweka malengo ni sawa na sala ya kumwambia Mungu kwamba sasa naomba baraka zako uzielekeze hapa.

Kitamfanya aachilie baraka zake kuelekea kwenye lengo lako, kuliko pale unapokuwa hauna lengo wala ndoto yoyote ile unayoifanyia kazi.

Umekuwa unaishi kwa miaka mingi bila ya kuwa lengo lolote. mwaka huu fuata mwongozo huu hapa kuweka malengo. Hata kama hujawahi kuweka malengo, ebu ufanye mwaka huu kuwa mwaka wako wa kwanza wa kuishi kwa kufuata malengo.

Kamwe usije kusema kwamba nimechelewa kuweka malengo. Muda bado, ndiyo kwanza kumekucha ndani ya 2024! Na kama unajua biashara mara zote ni asubuhi. Huu ndiyo muda wenyewe wa wwe kuutumia muda wako vizuri sasa.

Ukiwa na malengo, utakuwa na kusudi, utakuwa unajuwa wapi unaelekea na nini ufanye ili uweze kufika huko.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X