Home


 • Wasiliana na Godius Rweyongeza Sasa

  Habari yafuatayo ni mawasiliano Unayoweza kutumia kumpata GODIUS RWEYONGEZA

  Simu: +255 (0) 684408755

  Whatsap: +255 (0) 755848391

  Email: songambele.smb@gmail.com

   

  Kupata vitabu vyake wasiliana Moja kwa Moja na +255 (0) 684408755 (more…)

 • Hakuna kitakachobadilika kama wewe hutabadilika

  Hakuna kitakachobadilika, kama wewe hujabadilika.

  Kitu chochote unachotaka kibadilike, Anza wewe kukifanyia kazi.

  Kama mahusiano Yako unataka yabadilike Anza kuyafanyia kazi

  Kama ni Hali Yako ya kipato , chukua hatua, Anza kulifanyia kazi Hilo. Na pengine unaweza kuanza na programu yetu ya mafunzo ya kuongeza kipato mara mbili; ambayo unaweza kuyapata hapa

  Ebu labda nikiuulize, ni ni kitu gani ambacho ungepend kuona kinabadilika kwenye maisha yako. je, ni kwa namna gani upo tayari kulipa gharama kwa wajili yakufanjikisha hicho kitu.

  Na kumbuka kwamba kulipa gharama iyo kunatofautisha kati ya watu ambao huwa wanafanikisha malengo yao na wale ambao huwa wanaishi tu kuwa na matamanio juuu ya melengo, huku wakiwa hawachukui hatu yoyote.

  Badala tu ya kuishia kutamani kwamba ungeweza kufanya mabadiliko. sababisha mabadiliko kwelikweli bila ya kurudi nyuma.

  Uwe na wakati mwema

 • Usiogope kukosea

  Vitu vingi ambavyo huwa tunafanya kwenye maisha huwa vinahusisha makosa. Ni vigumu kuanza kufanya kitu kwa ufanisi wa asilimia 100 hasa unapofanya mara ya kwanza.

  Mtoto anapoanza kutembea, haanzi kutembea huku akiwa anatembea kwa usahihi asilimia 100. Anaanza kwa kuanguka, ila ni kupitia huku kuanguka ndiyo baadaye anaweza kutembea vizuri bila wasiwawasi wowote. Baadaye tunakuja kumwona huyo mtoto akikimbia mbio za marathon n.k

  Unaikumbuka siku yako ya kwanza kazini?

  Mara nyingi siku ya kwanza ya kufanya kitu huwa siyo bora sana. Ila kadiri unavyokuwa unafanya ndivyo unakuwa unazidi kuwa bora zaidi.

  Huwezi kusema kwamba mimi nasubiri kuw amkamilifu ili nianze. Hakuna kitu ambacho huw akinaanz akikiw ana ukamilifu wa asilimia 100.

  Simu za kwanza hazikuwa kamilifu.

  Ndege za kwanza hazikuwa kamilifu.

  Ukamilifu kwenye hii dunia haupo. Ndiyo maana utagundua kwamba kompyuta huwa zinakuja katika matoleo. Kuna toleo la kwanza, kuna toleo la pili na kuendelea.

  Hii haimaanishi kwamba uanze kutoa kazi ambazo hazina ubora, badala yake kila kazi ambayo utaweka mkono wako, hakikisha kwamba ndiyo kazi bora kuliko zote kwa wakati huo. Kama badaye kutatokea kwamba kunahitajika marejekebisho, au kuna vitu unatakiwa kuboresha basi utaboresha.

  Lakini pia, unapotoa kazi yako, kuna watu wanatoa mapendekezo yao ya nana gani uweze kuboresha kazi yako. Ni vitu gani zaidi ambavyo unaweza kuongeza ili kuifanya kuwa bora zaidi. Haya maoni, haya siyo ya kupuuza. Yafanyie kazi. Boresha kazi na ifanye kuwa bora zaidi.

  Baada ya kusema hayo,naomba nikutakie kila la kheriii.

  SOMA ZAIDI: Usiogope Kuuliza

  Makala  hii imeandikwa name rafiki yako

  Godius Rweyongeza

  0755 848 391

  Morogoro-Tz

  Tuwasiliane kwa godiusrweyongeza1@gmail.com

 • NJIA ZA KUEPUKA KUGHAIRISHA MAMBO 2024

  Rafiki yangu mpendwa salaam, hongera sana kwa siku hii nyingine nzuri sana. Leo hii ni tarehe 1.2.2024. ni siku nyingine bora kabisa. Tayari mwezi mmoja umepita tangu tuuanze mwaka mpya wa 2024, kazi imebaki kwako sasa. Ni kwa namna gani mpaka sasa unaendelea kufanyia kazi malengo yako? Unajiona ukiwa unaelekea malengo yako au unakwama sehemu? Kumbuka, mwaka mpya siyo mwaka mpya tena, na usipoanya kitu, maana yake huu mwaka unaenda kuupoteza wote, bila ya kuwa umefanya kitu cha maana.

  Kwanza labda nikuulize, una malengo ambayo unayafanyia kazi? Ukweli ni kuwa kama hauna malengo, kuna kosa kubwa ambalo unafanya. Hakikisha kabisa unakaa chini na kuweka malengo yako sasa.

  Maandiko mengi ambayo niliandika ndani ya mwezi wa kwanza, yalikuwa yakielekeza namna ya kuweka malengo 2024, namna ya kuyafanyia kazi  hayo malengo na mpaka kuyafikia. Kama kwa bahati mbaya hukufuatila haya mafunzo, nashauri, utembelee blogu yangu ya SONGAMBELE (www.songambele.co.tz) ili uweze kujifunza zaidi kuhusu haya mambo yote ambayo nakwambia.

  Nakushauhri pia uweze kujipatia nakala ya kitabu cha NGUVU YA KUWEKA MALENGO. Kitabu hiki ni mwogozo wa kuweka malengo. Kama kwa bahati mbaya mpaka hivi tunavyoingia ndani ya mwezi wa pili, unaingia bila ya kuwa na malengo. Basi, jiwekee mkakati wa kuhakikisha kwamba unakuwa na malengo, mapema sana ndani ya huu mwezi. Malengo ndiyo ramani pekee ambayo itakuongoza, wewe kuelekea na kufikia kule ambapo unataka kufika. Ukweli ni kuwa huwezi kufanikisha mambo makubw kama hauna malengo.

  Sasa kwa kuwa tumeshaongelea sana kuhusu malengo, ndani ya huu mwezi wa pili tutakuwa tunaongelea zaidi kuhusu NAMNA GANI AMBAVYO UNAWEZA KUACHA TABIA YA KUGHAIRISHA MAMBO.

  Kwa hiyo, ninaenda kuchukulia kwamba tayari una malengo, kama hauna malengo. Pata huo mwongozo ambao nimekuelekeza uupate, ndani ya huu mwezi wa pili nataka uache tabia ya kughairisha malengo na miipango yako ambayo umeiweka kwa ajilil ya mwaka wako 2024. Unaachaje tabia hii tabia.

  Sasa tuambatane kila siku kwenye makala ambazo nitakushirikisha karibia kwa mwezi mzima bila ya kuacha.

  Kugharisha mambo ni kuacha kufanya jambo ambalo liko mbele yako kwa sasa kwa huku ukiwa unajiambia kwamba jambo hilohilo utalifanya kesho au siku nyingine. Na muda mwingine unaweza kuwa hujiambii kwamba hilo jambo utalifanya kesho au siku nyingine, lakini unaweza kuwa kwenye fikra zako unaamua kwamba unafanya jambo jingine ambalo kwa muda huo unaona kwamba linafaa wakati jambo hilohilo ambalo unafanya siyo la muhimu kwa wkaati huo.

  Mfano, jukumu lako kuu kwa wakati huo linaweza kuwa ni kutafuta na kuwafikia wateja kadhaa kwa wakati huo. Lakini ukajikuta kwamba unaacha kufanya hilo jukumu na badala yake unaenda  facebook au kwenye mtandao mwingine wa kijamii na kujikuta kwamba unapoteza muda wako wa thamani huko. Mwisho wa siku uttajikuta unajiambia kwamba hii ndiyo inaenda kuwa ni mara yangu ya mwisho kufanya hili, halafu kesho yake jambo kama hilo hilo linajirudia. Unajuikuta kwamba umerudi kwenye hali hiyohiyo.

  Sasa ili tuweze kuachana na tabia ya kughairisha mambo unapaswa kuanza na kuingalia thamani ya muda wkao.

  Muda wako ni wa thamani. Najua hili siyo mara yako ya kwanza kuliskikia. Siyo mara yako ya kwanza kusiikia kwamba muda ni mali. Siyo mara yako ya kwanza kusikia kwamba muda unapaswa kuwa unautumia vizuri. Sasa kwa kuwa unajua haya mambo, ninachotaka kukwambia ni kukueleza kwa undani zaidi ni kwa namna gani muda ni wa thamani..

  Hivi inakuwaje muda unasemwa kuwa na thamani kiasi hicho. Yaani, muda unakuwaje mali? Hili limeanzaje?

  Ngoja nikuelekeze vizuri ili uweze kunielewa.

  Mimi, wewe na mtu yeyote unayemfahamu leo hiii hapa duniani, na hata wale usiowafahamu, sote kwa siku moja tuna saa 24. Hakuna mtu yeyote Yule ambaye ana muda mwingi zaidi ya mwingine. Mpaka leo hii unaposoma hapa, hakuna kifaa chochote kile ambacho kimegunduliwa ambacho kinaweza muda wa mtu yeyote.

  Sekunde moja ambayo imepita sasa hivi, naam, hii sekunde, haitakaa irudi tena. Ikishapita ndiyo itakuwa imepita, ni juu yako sasa kuhakikisha kwamba kila sekunde inayokuja kwako unaitumia vyema kabisa.

  Moja ya kipengele muhimu sana linapokuja suala zima la muda ni kwmaba muda huwezi kuukopa, wala kuukopesha. Muda siyo kama fedha. Na ndiyo maana unaambiiwa kila siku kuwa unaweza kukopa fedha, lakini huwezi kukopa muda. Limekaaje hili, ngoja nikuoneshe hapa..

  Tuanze na dhana ya kukopa na kukopesha fedha. Leo hii ukiwa hauna fedha, unaweza kwenda benki yoyote ile na kuwaambia kuwa ungependa kukopa kiasi fulani cha fedha, halafu hiyo benki, watakuwa tayari kutoa fedha na kukupa. Lakini huwezi kwenda benki kukopa muda.

  Leo ikitokea kwamba una fedha nyingi, unaweza kuwakopa rafiki zako. Au unaweza kuwekeza hizo fedha sehemu yoyote ile ambayo unataka wewe. Lakini ukweli ni kuwa huwezi kukopesha muda wako kwa mtu. Akautumia muda wako halafu akaja kukurudishia muda wako baadaye.

  Ndiyo maana tunapoanza kuliangalia suala zima la kughairisha mambo tunapaswa kuanza kuliangalia suala la muda wako. Maana vitu vyote tunavyovifanya kuelekea malengo yetu, na vitu vyote ambavyo hatufanyi, yote hayo tunayafanya ndani ya muda tulionao.

  Sasa swali langu la kwanza kwako ni kuwa muda wako una thamani kiasi gani?

  Njia rahisi ya kutambua thamani ya muda wako nia kuangalia kipato ambacho unaingiza sasa hivi

  Kama kwa sasa hivi unaingiza kipato cha milioni  moja kwa mwezi. Maana yake thamani ya saa lako moja ni milioni moja kugawa kwa siku thelathini, kugawa kwa saa 24. Yaani, (1,000,000/30/24) tunapata kuwa thamani ya saa lako moja ni sawa na 1,388.88

  Huwa napenda kuipima thamani ya muda wako kwa kuangalia zaidi kile kipato ambacho ungependa kufikia ndani ya huu mwaka.

  Kama huu mwaka ungependa kipato chako kiwe ni milioni mbili. Maana yake ni kwamba milioni 2,000,000/30/24. Maana yake thamani ya ya muda wako ni 2,777.77

  Ila ngoja ni kwambie kitu, kama umepiga kwa kutumia hizi hesabu na bado thamani ya muda wako ni chini ya elfu tano, sikiliza, weka kiwango cha chini kabisa cha thamani ya saa lako moja kuwa elfu tano. Hiki ndicho kinapaswakuwa kiwango chako cha chni kabisa kwa mtu wa nguvu kama wewe ambaye unafuatilia mafunzo yangu kila mara, ni kiwango amabcho unapaswakuanza kukifnayia kazi.

  Hii ndiyo kusema kwamba haupaswi kufanya kitu chochote ambacho ni cha viwango cha chini ya elfu tano kwa saa yako moja.

  Kama kitu unachofanya ndani ya muda wako ni cha thamani ya chini. Yaani, thamani yake ni chini elfu tano kwa muda huo. Ujue kwamba unajiumiza.

  Kwa kulijua hili litakusaidia wewe kuweza kujali muda wako zaidi na kuwekeza muda wako kwenye maeneo ambayo yanazalisha matokeo makubwa zaidi kuliko eneo jingine.

  sasaa baada ya kujua thamani ya muda wako, maana yake hii itakuongezea hasira ya kujali zaidi muda wako kuliko mtu mwingine yeyote.

  Lakini pia hutakubali kufanya majukumu ambayo yapo chini ya viwango vyako

  Sasa mtu mmoja aliniuliza, kuwa kama thamani ya muda ni elfu tano kwa saa. Lakini kuna saa ambazo ninakuwa sipo kazini, ambao ni muda kaupumzika.

  Ngoja nikwambie kitu.

  Muda wako unapaswa kuwa na thamani bila ya kujali ndani ya huo muda unafanya kazi au hufanyi kazi.

  Muda wakowote unapaswa kuwa na thamani, ngoja nikuelekeze zaidi.

  Namna unavyotumia muda wako wa ziada, muda wako wa mapumziko, ndivyo ambavyo utaweza kutumia muda wako wa kazi. Kama muda wako wa mapumziko unalewa, kwa kisingizio kuwa ni muda wako wa mapumziko. Ni ukweli kuwa huwezi kuzalisha matokeo muda wa kazi ukifika na huwezi kuwa na ufanisi.

  Jambo  hili litapekelea wewe kuwa ufanisi kidogo na kuzalishaji kidogo muda wa kazi. Kumbe, kwa sababu hiyo, unapaswa kuheshimu muda ambao hufanyi kazi, kama ambavyo unaheshimu muda wako wa kufanya kazi. Unapaswa kuheshimu muda wako wa kulala kama amabvyo unaheshimu muda wako mwingine. Kwa sababu hivi vitu vyote vinaungana, namna unavyotumia muda wako mwingine wa mapumziko, ndivyo ambavyo utatumia muda wako wa kazi. Ukitumia muda wako wa ziada, muda wa kazi pia hutaweza kuzalisha matokeo mazuri na yanayoeleweka.

  Sasa kazi ambayounapaswa kufanya siku ya leo ni moja hasa tunapoanza kuliongelea zaidi suala zima la kughairisha mambo. Jua thamani ya muda wako. Kama bado hujui thamani ya muda wako, yaani ksa saa moja, weka kiwango cha chini kabisa kuwa elfu tano, unawez akuweka kiwango chochote kile cha juu, ila isiwe chini ya elfu tano.

  Je, wewe umeifahamu thamani yako ya muda?

  Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza

  Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza; kupitia mtandao wake wa songambele (www.songambele.co.tz)

  Kwenye mitandao ya kijamii. Godius Rweyongeza apatikana kama Godius Rweyongeza.

 • Vitu vitano ambavyo hakuna mtu yeyote anaweza kufanya Kwa niaba Yako

  Vitu vitano ambavyo hakuna mtu yeyote anaweza kufanya Kwa niaba Yako

  1. Hakuna mtu anaweza kukuamini wewe kama unavyojiamini. Wewe ndiye mtu Unayopaswa kujiamini Kwa asilimia zote hata kama wengine hawakuamini. Jiamini. Mwenyewe kwanza

  Ukiendelea kujiamini Kwa muda mrefu, hata kama wengine walikuwa hawakuamini, watakuamini TU. Jiamini.

  1. Hakuna mtu anayeweza KUFANYIA KAZI MALENGO Yako Kwa niaba yako. MALENGO Yako, yafanyie kazi wewe mwenyewe Kwa maana hakuna mtu wa kukusaidia kwenye Hilo.
  2. Kuanzisha biashara.
   Kama umekuwa unajiambia kuwa utaanzisha biashara na hujafanya hivyo, fanya hivyo. Hakuna mtu atafanya hili Kwa niaba Yako.
  3. Hakuna mtu atapenda watoto wako, mwenza wako, familia Yako Kwa niaba Yako. Ni jukumu lako
  4. Kufanya mazoezi. Hakuna mtu atafanya mazoezi Kwa niaba Yako.
   Hili jambo sharti ulifanye mwenyewe.

  Rafiki yangu, hayo ndiyo mambo matano ambayo hakuna mtu hata mmoja atayaganya Kwa niaba Yako. Unapaswa kuyafanya mwenyewe.

  Godius Rweyongeza
  +255755848391

 • Vitabu ambavyo kama mwanachuo unapaswa kujisomea.

  Hongera sana kwa kupenda kukisoma. Hii tabia nzuri ya kujisomea unapoianza ukiwa mwaka wa kwanza chuoni, itakupeleka mbali. Mpaka kuja kumaliza chuo, utakuwa mtu wa tofauti.
  Mtu wa tofauti kwenye tabia
  Mtu wa tofauti kwenye hatua unazochukua
  Mtu wa tofauti kwenye mtazamo na fikra.

  Hivyo, nikushihi sana usiache kujisomea vitabu hivi kipindi chote uwapo chuoni. Tenga muda wa kujisomea hata kama ni kidogo.
  Kisha soma.

  Vifuatavyo ni vitabu ambavyo kama mwanachuo unapaswa kuanza kujisomea.

  1. JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO.
  Hiki kitabu kitakupa mwongozo wa kuwa ndoto kubwa. Kitakufanya uanze kufikiri nje ya boksi. Wakati wenzako wanafikiri wamalize chuo, wapate kazi, wanakaoe na kuolewa. Wewe utakuwa na UNAFIKIRI zaidi ya hapo.

  Utakuwa ndoto kubwa ambazo zimekujaa na utakuwa tayari kuzifanyia kazi bila ya kurudi nyuma. Gharama ya kitabu hiki ni 25,000/- TU. Nakala ngumu. Lipia kwa TIGO PESA: 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA ili ukipate.

  2. NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA

  Hiki kitabu kitakuonesha kuwa ukiwa na ndoto kubwa unapaswa pia kuzifanyia kazi hata kama ni kidogo kidogo. Zifanyie kazi ndoto zako hatua kwa hatua. Anza hata kama ni kidogo. Kitu kidogo unachofanya Leo hii, kitakupeleka mbali kesho. Ukikifanya kwa uhakika na kwa msimamo.

  Kitabu hiki kimekuwa tiba kwa wengi, Nina uhakika kitakufaa na Wewe pia. Tena sana kwa maana ndiyo kwanza unaanza na tayari utakuwa na mwongozo sahihi wa kwenda nao ambao ni hiki kitabu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA.

  Kipate Sasa hivi. ni 25,000/- TU. Wasiliana na 0684408755

  3. MAAJABU YA KUWEKA AKIBA pamoja na MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA HATIFUNGANI NA VIPANDE

  Hivi ni vitabu viwili ambavyo vitakupa msingi wa elimu ya fedha na hasa kwenye maeneo mawili muhimu sana. KUWEKA AKIBA na KUWEKEZA KWENYE HISA HATIFUNGANI NA VIPANDE.

  Kama mwanachuo, Anza kujijengea utaratibu wa KUWEKA AKIBA. Anza kuwekeza kwenye HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. Kiasi hichohicho kidogo unachopata, tafuta namna ya KUWEKA AKIBA pia. Sikiliza ukilifanyia kazi hili, utanishukuru MAISHA Yako yote.

  Kuna watu utasoma nao mwaka wa kwanza Hadi mnamaliza wakiwa hawajui chochote kuhusu HISA, wataanza kazi wakiwa hawajui chochote kuhusu HISA HATIFUNGANI NA VIPANDE. Wachache watakuja kujua baadaye sana. Na wengine wanaoweza wasijue hiki kitu MAISHA Yao yote. Wewe kujua hivi VITU mara hii, ni hatua kubwa.

  Unachotakiwa kufanya Sasa ni kuhakikisha umepata nakala za hivi vitabu Sasa hivi. Kila nakala ni Kila nakala ni 25,000

  Pamoja na hivi pata hivyo vingine ambavyo nimetaja hapo juu.

  *Hitimisho*
  Kama utafanya tabia ya kusoma vitabu kweli kuwa sehemu ya MAISHA Yako ya Kila siku, itakufanya kuwa mbele ya wenzako hapo chuoni.

  Nikutakie Kila la kheri.

  Vitabu vyote nilivyotaja hapo juu, unaweza kuvipata kwa kuwasiliana na 0684408755

  Karibu sana.

  Godius Rweyongeza
  0755848391
  Morogoro-Tz

 • maeneo matano Unayopaswa kuyawekea NGUVU mwaka 2024 kwenye kusoma na kujifunza na vitabu Unayopaswa kusoma.

  Isifike hatua ukaona kwamba umeshajua kila kitu. Siku ambayo utaona umeshajua kila kitu ndiyo siku ambayo utaanza kupoteza. Mara zote kuwa unajifunza.

  Kujifunza kuwe sehemu ya maisha Yako. Kama ambavyo Huwa hakuna wakati unaposema sasa nimeshakula inatosha sitakula Tena. Hivyo hivyo, kujifunza. Isifike hatua ambapo utaona kwamba imetosha.

  Kila mara kuwa na kitabu unasoma. Jiunge na kozi na programu mbalimbali na jifunze bila kuacha.

  Halafu Yale unayojifunza; yafanyie kazi mara zote bila kuacha.

  Sijui unanielewa hapo?

  Sasa yafuatayo ni maeneo matano Unayopaswa kuyawekea NGUVU mwaka 2024 kwenye kusoma na kujifunza na vitabu Unayopaswa kusoma.

  1. Jifunze zaidi kuhusu PESA. Wengi wanajua kuhusu matumizi ya PESA, lakini hawajui kuhusu kutunza PESA na kuifanya PESA iwafanyie kazi. Mwaka huu jifunze zaidi kuhusu namna ya kuitumikisha PESA. Na itumikishe haswa PESA kuanzia mwaka hata kama ni Kwa kiwango kidogo.

  Vitabu Muhimu vya kusoma kwenye hili ni kitabu Cha
  👉MAAJABU YA KUWEKA AKIBA 
  👉MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA HATIFUNGANI NA VIPANDE
  👉JINSI YA KUTENGENEZA MSHAHARA NJE YA MSHAHARA

  Anza na hivyo vitabu. Visome vizuri, mwenyewe utafurahi Kwa uamuzi huo utakaokupa umechukua.

  1. Jifunze zaidi kuhusu biashara.
   Ili uweze KUTENGENEZA kipato zaidi unahitaji kujifunza zaidi pia kuhusu biashara. Biashara ni njia ha KUTENGENEZA kipato zaidi ambacho hakina ukomo. Jifunze biashara na fanyia kazi Yale unayojifunza bila ya kurudi nyuma.

  Vitabu vya biashara ambavyo unapaswa kusoma 2024 ni pamoja na
  👉MAMBO 55 YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZIAHA BIASHARA
  👉NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA.

  Hivi vyote unaweza kuvipata Kwa kuwasiliana na 0684408755 Sasa.

  1. Jifunze kuhusu mtandao na JINSI ya kukutumia kwenye masoko na KUTENGENEZA fedha zaidi.
   Tofauti na zamani ambapo masoko yalikuwa yanafanyika Kwa njia za redio, runinga na magazeti. Leo hii unaweza kuwafikia wengi Kwa simu Yako TU. Unalionaje Hilo. Unachotakiwa kufanya ni kuwa na maarifa sahihi. Na maarifa haya sahihi utayapata kwenye vitabu hivi.
   👉zama zimebadilika: maisha yamebadilika, ajira hatarini na wewe badilika.
   👉JINSI ya KUTENGENEZA fedha Kwa Kile unachojua.
  2. Jifunze kuhusu KUWEKA MALENGO na kuyafanyia kazi.
   Hili ni eneo unalopaswa kulifahamu hasa Kwa mwezi huu wa Januari.

  Vitabu vya kusoma kwenye hili eneo
  👉JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO.
  👉NGUVU YA KUWEKA MALENGO.

  KUPATA vitabu hivyo, wasiliana na 0684408755

  1. Jifunze kuhusu kuongeza kipato chako. Hili litakusaidia mwaka huu kipato chako kisibaki palepale. Kuongeza kipato chako ni Muhimu sana. Maana kipato chako hakipaswi kubaki palepale.

  Vitabu Muhimu vya KUSOMA.
  👉VYANZO VINGI VYA KIPATO: Usipokuwa na VYANZO VINGI VYA KIPATO, utakuwa na VYANZO VINGI VYA mahangaiko.
  👉programu ya ONGEZA KIPATO CHAKO MARA MBILI.

  Hayo ndiyo maeneo Muhimu Unayopaswa kuyawekea NGUVU kwenye kujifunza mwaka 2024.

  Nikutakie Kila la kheri.

  Godius Rweyongeza
  0755848391
  Morogoro-Tz

 • Nawezaje kupata vitabu Vya Godius Rweyongeza?

   

   

  Rafiki yangu mpendwa salaam. Godius Rweyongeza yupo Morogoro nchini Tanzania. Ofisi zake zipo maeneo ya sabasaba. Hata hivyo hilo halikuzuii wewe kupata vitabu vyake popote pale utakapokuwa nchini Tanzania.

   

  Ili kupokea kitabu chako popote pale utakapokuwa nchini Tanzania na Afrika Mashariki,

  1. Kwanza unatakiwa kuchagua kitabu ambacho ungependa kupokea. Vitabu vya Godius Rweyongeza vipo katika mfumo wa nakala ngumu (hardcopy), nakala laini (softcopy) na nakala za sauti (audiobook). Kama unataka nakala za mtandaon (softcopy/ebooks) basi utalipia na kupokea ebooks zako hapohapo bilaya kuchelewa. Aidha kama unataka vitabu vya sauti; audiobooks utalipia na kutumiwa audiobooks zako mara moja. Kutokana na urefu wa audiobooks huwa zinatumwa kwa telegram tu. Vitabu vyote vya sauti (audiobooks) na vya mtandaoni (softcopy) vinapatikana kwa elfu kumi. Orodha ya vitabu itaambatanishwa hapo chini.
  2. Godius Rweyongeza pia ana vitabu vya hardcopy. Hivi unaweza kuvipata popote pale utakapokuwa nchini Tanzania. Unachotakiwa ni kuchagua kitabu cha Hardcopy unachotaka. Orodha Kamili ya vitabu vya nakala ngumu, hardcopy inaambatanishwa hapo chini.
  3. Ukishachagua kitabu chako, utafanya malipo, namba ya malipo ni airtel money 068440875 kama upo nje ya nchi ya Tanzania tumia namba hii YA M-PESA kufanya malipo: +255745848395. Hakikisha umeanza na code +255 kama inavyooneshwa hapo kama upon je ya nchi. Kwenye namba zote jina ni GODIUS RWEYONGEZA  Baada ya kufanya malipo, tuma uthibitisho kuwa umefanya muamala kwa namba ya simu 068440855 (whatsap/sms).
  4. Kwa vitabu vya mtandaoni (softcopy/audiobook) utavipokea ndani ya dakika tano baada ya kuwa umefanya malipo. Kwa vitabu vya nakala ngumu, vitatumwa na utapewa maelekezo ya kuvipokea. Lakini kama una mapendekezo ya gari gani tutumie wakati wa kukutumia vitabu vyako, utatutumia, nasi tutafuata hayo maelekezo yako. Ndani ya saa 48 unakuwa umepokea kitabu chako kulingana na eneo ulipo. Wakati kama upo karibu na Morogoro au Dar Es Salaam, basi huwa ni ndani ya saa 2. Kwa Dar Es Salaam na Morogoro tunafanya Delivery ila hapa unaongeza kiasi kidogo kwenye gharama ya kawaida ya kununua kitabu kwa ajili ya delivery.

  Rafiki yangu, hivyo ndivyo unaweza kupokea vitabu vya Godius Rweyongeza popote pale utakapokuwa nchini Tanzania, Afrika na Dunia nzima.

   

  Hapa chini nimeambatanisha orodha vya vitabu vyake vyote.

  Kwenye hii orodha.

  Vitabu 11 vya kwanza vinapatikana kwenye mfumo wa nakala ngumu.

  Vitabu sita vya kwanza vinapatikana kwenye mfumo wa sauti pia.

  Vitabu vingine ni nakala laini.

  Hata hivyo kuna vitabu vingine ambavyo vinapatikana kwenye mfumo wa nakala laini na nakala ngumu; na vingine vinapatikana kwenye mifumo yote; yaani, nakala ngumu, nakala laini na nakala yamtandaoni. Chagua mfumo wowote ule ambao ungependa kupata kwa sasa. Kisha lipia kitabu unachotaka.

   

  Kumbuka; nakala ya laini (softcopy/ebook) ni 10,000/- kwa kila nakala

  Nakala ngumu (hardcoy) ni 25,000/ kila nakala

  Na nakala za sauti ni 10,000/- kwa kila nakala.

  Ifutayo ni rodha kamili ya vitabu vya GODIUS RWEYONGEZA

  1. JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO

  Hardcopy (25,000). (hardcocopy)

  Audiobook=10,000/-

  Flash audiobooks zote + mafunzo ya ziada (150,000/-)

   

  1. Maisha Ni FURSA: Zitumie ZIKUBEBE

  (hardcocopy 25,000/-)

  Audiobook=10,000/-

  Flash audiobooks zote + semina+kozi+ mafunzo ya ziada (150,000/-)

   

  1. NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA

  (hardcocopy 25,000)

  Audiobook=10,000

  Flash audiobooks zote + semina+kozi+ mafunzo ya ziada (150,000/-)

   

  1. MAAJABU ya kuweka akiba

  Hardcopy 20,000

  (($oftcopy 10,000))

  Audiobook 10,000/-

  Flash audiobooks zote + semina+kozi+ mafunzo ya ziada (150,000/-)

   

  1. KIPAJI NI DHAHABU: Jinsi Ya Kugundua kipaji chako, kukinoa na kukiendeleza
   Hardcopy 25,000
   ($oftcopy 10,000)
   Audiobook 10,000
   Flash audiobooks zote + semina+kozi+ mafunzo ya ziada (150,000/-)

   

   

  1. JINSI YA KUONGEZA THAMANI YAKO ($oftcopy 10,000)

  Hardcocopy 25,000/-

  AUDIOBOOK (10,000/-)

  Flash audiobooks zote + semina+kozi+ mafunzo ya ziada (150,000/-)


  1. VYANZO VINGI VYA KIPATO (10,000) Softcopy

  Hardcopy (20,000/-)

   

  1. NGUVU YA KUCHUKUA HATUA YA KWANZA
   Hardcopy 25,000/-
   Softcocpy=10,000/-

  2. MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE Hardcopy 25,000  ($oftcopy 10,000)
  3. Kutoka sifuri MPAKA KILELENI (20,000) (hardcocopy)
  4. JINSI ya kuwa mwandishi MBOBEVU
   Hardcopy 20,000/-
   ($oftcopy 10,000)
  5. TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA: tatizo Ni rasilimaliwatu tunaowapoteza (volume 1)

  Hardcopy 25,000/-

   ($oftcopy 10,000)

   

  1. AKILI YA DIAMOND (hardcocopy 10,000/-)
   Softcopy 10,000
  2. Mambo 55 ya Kuzingatia kabla ya KUANZISHA BISHARA (Softcopy 10,000)
  3. JINSI YA kuibua ubunifu ulio ndani yako ($oftcopy 10,000)
  4. ZAMA ZIMEBADILIKA: MAISHA YAMEBADILIKA, AJIRA HATARINI na WEWE BADILIKA
  5. NGUVU YA KUWEKA MALENGO (10,000) softcopy
  6. NGUVU YA WAZO (5,000/-) softcopy
  7. MWONGOZO WA WAPAMBANAJI(softcocpy 10,000/-)
  8. NYUMA YA USHINDI: Kuna Kushindwa, Kushindwa, Kushindwa
   Softcocpy 10,000/-
  9. JINSI YA KUTENGENEZA MSHAHARA NJE YA MSHAHARA $oftcopy 10,000/-
  10. FURSA AMBAZO VIJANA WA SIKU HIZI WANACHEZEA NA JINSI YA KUZITUMIA $oftcopy (10,000/-)
  11. UJUZI AMBAO KILA MFANYABIASHARA ANAPASWA KUWA NAO $oftcopy (10,000/-) 
  12. MAAJABU ya kusoma vitabu (free ebook & Audiobook)

  Flash audiobooks zote + semina+kozi+ mafunzo ya ziada (150,000/-)

  Ebook hii ya maajabu ya kusoma vitabu unaweza kuipta bure kabisa hapa.

  Audiobook yake pia unaweza kuipata bure hapa

  Ila kama ungependa kupata flash, yenye audiobooks zote nane. Pamoja na mafunzo ya semina mbalimbali ambazo nimekuwa natoa, kozi mbalimbali ambazo huwa natoa pamoja na  mafunzo mengine ya ziada, basi utalipia laki moja tu. Namba ya malipo ni 0684408755. Ukishafanya malipo, nitumie ujumbe kwenye namba hiyohiyo whatsap ili ni kutumie flash au vitabu vyako.

  Mimi nakupenda sana. Kama una swali lolote tafadhali naomba uniulize, nami nitakujibu. Asante.

  Godius Rweyongeza

  0755848391

  Morogoro-TZ

 • ACTIVE MODE ACTIVATED

   

  Mara kwa mara kuna watu huwa unakuta wameandika kwenye sehemu mbalimbali mtandaoni au nje ya mtandaoni wakiwa maneno kama “dancing mode activated” au running mode activated n.k

   

  Sasa tunapouanza mwaka mpya 2024, kuna maeneo muhimu sana ambayo wewe unapaswa kuya”activate” na kuhakikisha yako “activated” kwa mwaka mzima unaokuja.

  1. UWEKEZAJI (INVESTING MODE ACTIVATED). Huu mwaka huu, usirembe mwandiko linapokuja suala zima la uwekezaji. Zembea sehemu nyingine lakini usizembee kwenye uwekezaji. Ufanye uwekezaji kuwa kipaumbele kwako ndani ya huu mwaka. Yaani, kila unapopokea fedha, kipaumbele chako cha kwanza kiwe ni kufanya uwekezaji. Na hata baada ya kuwa umeweza kufanya uwekezaji, kiasi kingine ambacho kitabaki, ondoa matumizi yoyote yale ambayo siyo ya lazima ili fedha nyingi uweze kuielekeza kwenye uwekezaji.

   SOMA ZAIDI: Uwekezaji Kwenye Hisa vs Uwekezaji Kwenye Maeneo Mengine

  2. KUONGEZA KIPATO. Ili uweze kuweka akiba, unapaswa kuhakikisha kwamba una kipato cha uhakika. Wengi huwa wanafikiri kwamba tunapozungumzia kipato cha uhakika basi tunakuwa tunzungumzia ajira hasa ya serikalini.

   Japo wengi wanaiona ni ajira ya uhakika, ila mimi sioni uhakika wowote ndani yake. Ajira ni ajira tu. Kumbe unapasaw kuwa unafikiria nje ya ajira mar azote. Na unafikiria nje ya ajira kwa kuhakikisha kwamba, unaanza kutengeneza vyanzo vingine vya kipato ambavyo vinakuingizia kipato nje ya ajira yako. Kwenye maisha yako usikubali kipato chako cha mwaka jana kuendelea kubaki vilevile ya mwaka unaofuata. Kila mwaka tafuta namna ya kuhakikisha kwamba kipato chako unakiongeza walau mara mbili zaidi ya kilivyokuwa mwaka mmoja ambao umetangulia. Na kama kuna mbinu ambayo unaona unaitumia na inaleta matokeo, basi hiyo mbibu kamwe usiache kuitumia. Itumie zaidi na zaidi ili uweze kuleta matokeo makubwa zaidi.

   SOMA ZAIDI: Unawezaje Kujiajiri kwa Mtaji Kidogo?

  3. Vitendo (action mode activated). Mambo yote unayojifunza hapa, hayatafnaya kazi kama wewe hutakuwa tayari kuyafanyia kazi. Ni mpaka ufanye kazi ndiyo utaweza kupata matokeo. Hivyo, mwaka huu fanyia kazi kila unachojifunza bila ya kurudi nyuma.

   SOMA ZAIDI: Nguvu Ya Vitu Vidogo Kuelekea Mafanikio Makubwa katika Vitendo;

  4. Biashara (business mode activated). Ili kuongeza kipato chako mara mbili unahitaji kuhakikisha kwamba unakuwa na biashara. Biahara ndiyo njia pekee ya uhakika ambayo inafahamika ya kuongeza kipato chako mara mbili zaidi kadiri muda unavyokwenda, ni tofauti na njia nyingine zozozte zile. Uongezwaji wa kipato kwenye ajira, una ukomo. Na mshahara kwenye ajira hauwezi kuongezeka mara mbili kila mwaka kwenye ajira. Lakini kwenye biashara, kama kweli utajifunza biashara kwa kina na kufanyia kazi yale unayotakiwa kufanyia kazi. Kama kweli utaongeza juhudi zaidi kwenye mauzo ya biashara yako, ni ukweli kuwa unaenda kufanya makubwa kwenye biashara yako bila ya kurudi nyuma. Hivyo basi, mwaka huu wa 2024, kama bado hauna biashara, anzisha biashara. Kama una biashara tayari, basi ongeza juhudi zaidi na zaidi li uweze kuwafikia watu wengine zaidi.

   SOMA ZAIDI: Vitu Vitano Vitakavyokuzuia wewe kufanikisha malengo yako

  5. Watu (people mode activated). Watu ni muhimu sana, ili ufanikiwe, unahitaji watu. Aidha ni watu wa kukusaidia wewe ili uweze kufanikisha ndoto na malengo yako. Wanaweza pia kuwa ni watu wa kukusimamia (makocha na mamenta). Aidha wanaweza kuwa ni timu yako unayofanya nayo kazi. Sasa wewe unahitaji ujuzi sahihi wa kukaa na watu na kuweza kufanya nao kazi. Unahitaji ujuzi wa kuhamasisha watu ili waweze kuchukua hatua kwenye majukumu yao ambayo wanatakiwa kufanyia kazi. Jifunze sana kuhusu watu nan a mna ya kushughulika nao. Huu ujuzi utakusaidia sana ndani ya huu mwaka 2024. Kummbuka, pesa zako wanazo watu. Kama umeajiriwa maana yake unamtegemea bosi wako ili aweze kukulipa mshahara (mtu). Na unahitaji kujua namna sahihi ya kuendana naye. Kama umeajiarji maana yake unategemea wateja wanunue kwenye biashara yako (watu). Na unapaswa kujua namna sahihi ya kushughulika nao. Kama umeajiri maana yake unafanya kazi na watu tayari. Unapaswa kujua namna sahihi ya kushughulika na watu wako. Kwa vyovyote vile rafiki yangu, hakikisha kwamba unakuwa na ujuzi sahihi wa kushulika na watu huu ujuzi utakusaidia parefu san akwenye maisha yako.

  Hizi ndizo aina za ujuzi ambazo unapaswa kuanza kuzifanyia kazi mara moja kwa manufaa yako wewe mwenyewe

 • Kitu kimoja unachopaswa kufanyia Kazi kwa uhakika 2024

  Kitu kimoja unachopaswa kufanyia Kazi kwa uhakika 2024

  Rafiki yangu, kuna kitu kimoja ambacho unapaswa kukifanyia kazi kwa uhakika mwaka 2024. Kitu hiki siyo kingine bali ni kutenda kile unachosema.

  Usishauri watu kitu ambacho Wewe mwenyewe hutakifanyia kazi.
  Usiwaambie watu wafanyevkitu ambacho Wewe hujawahi kufanya Wala mpango wa kufanya. Na Wala hutakaa ukifanye.

  Sema kidogo 2024, ila tenda sana
  Ukiwaambia watu juu ya habari ya kufanya mazoezi. Kuwa kipaumbele Wewe mwenyewe kwa kufanya mazoezi.

  Ukiwaambia watu weka AKIBA. Kuwa kipaumbele mwenyewe kwa KUWEKA AKIBA.

  Kumbuka, simaanishi kwamba mwaka huu ujioneshe. Kuna tofauti kubwa kati ya mtu anayejionesha na anayefanya kweli.

  Mfano, ninaposema fanya mazoezi. Simaanishi Sasa ujioneshe kuwa unafanya mazoezi. Ukiona mwaka huu unaanza kufanya kitu ili watu wakuone, ACHA.

  Fanya kwa msukumo kutoka moyoni na siyo kwa ajili ya kujionesha.

X