Home


  • Wasiliana na Godius Rweyongeza Sasa

    Habari yafuatayo ni mawasiliano Unayoweza kutumia kumpata GODIUS RWEYONGEZA

    Simu: +255 (0) 684408755

    Whatsap: +255 (0) 755848391

    Email: songambele.smb@gmail.com

     

    Kupata vitabu vyake wasiliana Moja kwa Moja na +255 (0) 684408755 (more…)

  • Elimu Ambayo Haifundishwi Shuleni (part 1)

    Tangu ukiwa mtoto unaambiwa kwamba nenda Shuleni, usome Kwa bidii Ili Uje Upate ajira. Umependa Shuleni, umesoma Kwa bidii SI ndio?

    Hongera sana. Leo nipo hapa kukwambia mbali na hayo yote tuliyojifunza Shuleni, Bado Kuna mambo ya msingi sana kwenye maisha ambayo hukufundishwa, na mambo Haya ni ya msingi mno, kiasi kwamba haupaswi kuyapuuza. Yajue uyatumie Kwa manufaa yakuinue, au Yapuuze uendelee kubaki hivyohivyo na pengine kurudi chini zaidi

    Katika video ya leo nimeeleza juu elimu isiyofundishwa Shuleni, ikiwa ni sehemu ya kwanza kabisa.

    Ifuatilie vizuri. Usisahau KUWEKA maoni Yako Ili tuweze kuendelea mbele kuandaa sehemu ya pili ya video hii

     

    jIF

    Masomo mengine muhimu: Hii nidyo sababu kuu kwa nini unapaswa kuhudhuria semina ya kuongeza kipato chako mara mbili mwaka huu

  • Hivi Ndivyo Vitu Ambavyo Vinakukwamisha Wewe Na Nini Cha Kufanya

    UNAENDELEAJE RAFIKI YANGU WA UKWELI, Karibu Tena kwenye blogu yetu kwa ajili ya mafunzo mengine mazuri ambayo nimeandaa kwa ajili yako. Siku ya leo  nina ujumbe mfupi tu kwa ajili yako. na ujumbe huu siyo mwingine bali ninataka kukwambia kuwa;

    Asilimia kubwa ya vitu ambvyo vinakuzuia wewe kufanikiwa ni vitu ambavyo viko ndani ya uwezo wako. Ukiweza kuvuka hivi vikwazo ambavyo vipo ndani ya uwezo wako. Utaweza kufanya makubwa sana.

    Vikwazo hivi ambavyo vipo ndani ya uwezo wako ni pamoja na

    1. Ukiachana na uzembe na kuchapa kazi, utaweza kufanikisha makubwa
    2. Kutokuwa na ratiba. Hiki ni kitu kingine ambacho ndani ya uwezo wako. Ukianza kuipangilia ratiba yako, itakusaidia sana kufanya makubwa bila kusukumwa na mtu yeyote. Ratiba yako inapaswa kuwa imebana muda wote, kiasi kwamba upatikanaji wako uwe ni mgumu mara zote.
    3. Kutokufanya maamuzi. Muda mwingine kutokufanya maamuzi kunakukwamisha sana wewe kupiga hatua. Inawezekana ni kuchelewa kufanya maamuzi, au kutofanya maamuzi kabisa. Unachotakiwa kufahamu ni kuwa maamuzi ni sehemu ya maisha yako. hakuna namna ambavyo unaenda kuyaepuka. Kitu kikubwa ni kwamba unapaswa kuyafanya kwenye maisha yako ya kila siku. Usiogope kufanya maamuzi hata kama muda mwingine yanakuogopesha.
    4. Kutaka kufanya kila kitu mwenyewe. Hiki ni kitu kingine ambacho kinakwamisha watu wengi. Ukweli ni kuwa huwezi kufanya kila kitu mwenyewe. Ni lazima uwe tayari baadhi ya vitu vingine kuwapa wengine wafanye. Maisha ni kusaidiana, ukitaka kupambana na kila kitu, ukweli ni kuwa
    5. Kutokufanya kazi kwa viwango vikubwa. Hiki ni kitu kingine ambacho kipo ndani ya uwezo wako.

    Ukweli ni kuwa kazi yoyoote ile ambayo wewe unashika, unapaswa kuifanya kwa viwango vikubwa kiasi kwamba uwashangaze watu watu watakaoshika kazi hiiyo. Je, umekuwa unafanya hivi. Au watu wamekuwa wanashika kazi hiyo na kuona kwamba wewe unashangaza kwa kutofanya kazi kwa ubora. Kama ni hivyo, basi unapaswa kurekebisha ambacho umekuwa unafanya, ili uweze kufanya kazi zako kwa viwango vikubwa na viwango vya hali ya juu. Nakutakia siku njema.

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

    Unaweza kujifunza zaidi kwa kufuatilia makala za Godius Rweyongeza kwenye youtube channel yake ambayo unaweza kuipata kwa kubonyeza hapa

    mafunzo mengine zaidi huwa anayotoa kupitia email. unaweza kujaza taarifa zako hapa ili mmoja wa wale ambao wananufaika na mafunzo yake kwa email

    Kila la kheri

    Godius Rweyongeza

  • Mambo 15 ambayo Godius Rweyongeza anashauri Uanze Kuyafanyia kazi Mara Moja

    Habari ya Leo. Hongera sana Kwa siku hii nyingine njema sana

    1. Tuitumie Leo kufanya makubwa. Kila mmoja Kwa jukumu lake analopaswa kufanya, alifanye Kwa weredi mkubwa

    2. Mabadiliko Unayotaka kuyaona Anza kuyasababisha mwenyewe siku ya Leo Kwa kufanya jambo lolote hata kama ni Dogo.

    3. Ukitimiza wajibu wako na Kila mmoja akatimiza wajibu wake, hii dunia Itakuwa sehemu nzuri sana kuishia.

    4. Vitu vingi ambavyo vitakupa MAFANIKIO MAKUBWA vinahitaji uvifanye Kwa kurudia rudia mara Kwa mara. Uwekeze mara Kwa mara, ujifinze mara Kwa mara, uongeze kipato chako mara Kwa mara n.k

    5. Usiischoke safari ya KUELEKEA malengo na ndoto zako kubwa. Endelea kupambania Kila siku.

    6. Ukweli ni kuwa usipofanyia kazi NDOTO ZAKO hakuna mtu atazifanyia kazi Kwa niaba Yako

    7. Muda Mzuri Wa kupanda mti ulikuwa ni miaka 20 iliyopita, ila muda mwingine Mzuri zaidi ni Sasa

    8. Kama Kuna jambo linakukwamisha, jifunze Hilo jambo kupitia usomaji wa vitabu.

    9. Mara zote kuwa unasoma kitabu.

    10. Kama hauna ndoto kubwa sahau kuishia maisha yenye mafanikio makubwa

    11. Fikiri Kwa ukubwa

    12. Jihusishe na watu chanya

    13. Pangilia siku Yako Kila siku

    14. Anzisha biashara 2024.

    15. Shukuru Kwa mambo mazuri mengi uliyonayo. Familia, wazazi, watoto, mwenza, afya njema kuiona siku ya Leo ……

  • Kwa Nini tunahitaji HAMASA Kila siku

    Siku Moja ZigZiglar alikuwa anaongea mbele ya umati, ndipo kijana. Mmoja akasimama na kumuuliza swali gumu Kwa kusema, Kwa Nini hizi HAMASA Huwa hazidumu?

    ZigZiglar alimjibu Kwa kusema kwamba HAMASA ni kama kuoga. Hauogo TU mara Moja na kuacha, Bali unaoga Kila siku, kwako Kila siku, inakuwa ni sehemu ya kuoga.

    HAMASA ni kama kuoga tunaigitaji Kila siku, tunahitaji HAMASA Kwa sababu.

    Hapa kuna sababu kumi kwa nini tunahitaji kuwa na motisha kila siku:

    1. Kuendeleza Utendaji: Motisha inatusukuma kufanya kazi kwa bidii na ufanisi zaidi katika shughuli zetu za kila siku.

    Soma Zaidi: Vitu Vitatu (03) Vitakavyoongeza Ufanisi Kazini Kwako

    2. Kuwajibika: Motisha inatusaidia kuwa na uwajibikaji kwa malengo yetu na kufanya maamuzi sahihi katika kufikia mafanikio.

    Soma zaidi: Kitabu: How to Win Friends and Influence People

    3. Kukabili Changamoto: Motisha inatupa nguvu ya kukabiliana na changamoto mbalimbali tunazokutana nazo katika maisha.

    Soma zaidi: NYUMA YA USHINDI

    4. Kuweka Lengo: Motisha inatusaidia kuweka malengo na kufanya jitihada za kufikia malengo hayo kila siku. Kumbuka Kila siku ni siku inayohitaji motisha na HAMASA, bila hili kwenye malengo Yako hutoboi.

    Soma zaidi:NGUVU YA KUWEKA MALENGO

    5. Kuendelea Kujifunza: Motisha inatuchochea kutafuta maarifa zaidi na kuendelea kujifunza ili kukuza ujuzi wetu. Kumbuka maarifa ni Muhimu hasa kama tunataka kupata MAFANIKIO MAKUBWA. Bila kuendelea kujifunza utajikuta kwamba umepitwa na vitu vingi.

    Soma zaidi: Mambo 5 ya kujifunza kutoka Kwa Wajasiriamali Wenye Mafanikio

    6. Kuboresha Uhusiano: Motisha inaweza kuboresha uhusiano wetu na wengine kwa kutupatia nguvu ya kufanya mazungumzo na kushirikiana.

    7.  Kudumisha Mtazamo Chanya: Motisha inatusaidia kuwa na mtazamo chanya kuelekea maisha na kuvumilia changamoto zinazojitokeza.

    8. Kupunguza Stress: Motisha inaweza kupunguza viwango vya stress na wasiwasi kwa kutupa lengo na kusudi la kufanya kazi.

    9. Kuimarisha Afya: Motisha inaweza kuhamasisha mazoezi na mtindo bora wa maisha, hivyo kuchangia katika afya njema.

    10. Kufikia Mafanikio: Hatimaye, motisha inatuwezesha kufikia mafanikio na furaha katika maisha yetu kwa kutimiza malengo na ndoto zetu.

    SOMA ZAIDI: Audiobook Ya Kitabu Cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA Sasa Ipo Tayari

    Kiufupi ni kwamba tunahitaji motisha Kila siku Kwa sababu motisha inaambukizwa. Ni kama joto. Ukiwa na HAMASA na motisha Kila siku, unaweza kuwaambukiza na wengine ambao wamekuzunguka kuwa na HAMASA pia.

    Hivyo, kuwa na HAMASA rafiki yangu.

    Kila la kheri.

    Imeandaliwa na

    Godius Rweyongeza

    Unaweza kujifunza zaidi Kutoka Kwa GODIUS RWEYONGEZA

    Kupiti YouTube channel yake hapa

  • Njia Tano Za kuwa na Ukuaji Kwenye Maisha, Biashara na Kila kitu unachofanya

    Rafiki yangu, hongera sana kwa siku hii ya kipekee. Leo ni siku nyingine bora kwa ajili yako. Hakikisha kwamba unaitumia vyama siku ya leo. Na moja ya kitu muhimu sana ambacho unapaswa kukifanyia kazi kuanzia leo ni kukua.

    Ukuaji ni moja ya kitu muhimu sana hasa unapokuwa unataka kufanya makubwa. Unaanzia hapo hapo ulipo, unafanya yale unayoweza kufanya sasa hivi., lakini habari njema ni kwamba haupaswi kuendelea kubaki hapohapo. Unapaswa kuendelea kukua mar azote.

    Jichukulie wewe kama kampuni. Kama ungekuwa kampuni, ni ukuaji watu wangekuwa wanahamasika kuwekeza kwenye kampuni hii (ambayo ni wewe) au wasingekuwa na hamu kabisa? Ni kitu gani kingewafanya wawe na hamu ya kuwekeza kwenye hii kampuni au kukosa hamu kabisa?

    Na swali tamu sana kuhusu hili ni kwamba je,. Wewe mwenyewe kama ungekuwa unawekeza kwenye kampuni ambayo ni wewe, ungewekeza kwenye wewe?

    Kama unaona kwamba kuna mapungufu, basi hayo mapungufu unapaswa kuyafanyia kazi kwa kuboresha zaidi. Ili uwe bora.

    Usikubali kuendelea kuwa pale kila siku.

    Kuhakikisha kwamba hauendelei kuwa hivyo hivyo kila siku, nimekuandalia vitu vitano muhimu sana ambavyo unapaswa kuzingatia ili kuwa na ukuaji kwenye hicho unacahofanya.

    Kitu cha kwanza ni kwa wewe kuhakikisha kwamba unakuwa mtu wa kujifunza kila siku. Mara zote jifunze, bila ya kuchoka. Kujifunza ni chanzo cha wewe kuendelea kuwa na maarifa mapya kila siku. Kama unataka kuwa na matokeo ya tofauti, endelea kujifunza kila siku, jifunze kupitia usomaji wa vitabu.

    SOMA ZAIDI: Ujumbe Muhimu Kwa Wasomaji Wote Wa Vitabu

    Kitu cha pili ni kwamba unapaswa kuboresha kile unachofanya. Mara zote boresha, maboresho haya yanaweza kutokana na namna unavyoona kwamba hiki kitu cha sasa kinafanyika, na sasa kinapaswa kuboreshwa zaidi. Lakini pia maboresho haya yanaweza kutokana na mrejesho ambao unaupokea kutoka kwa wateja. Kadiri unavyopokea mrejesho kutoka kwa wateja, boresha ili kupata mrejesho ambao ni bora zaidi ambao utakufanya ukue zaidi na zaidi.

    SOMA ZAIDI: AINA TATU ZA UJUZI UNAOHITAJI ILI KUONGEZA THAMANI YAKO NA KULA MEMA YA NCHI

    Tatu ni kufanyia kazi kile unachojifunza. Yaa, nakumbuka kwenye nambari moja nilikwmabia kwamba unapaswa kujijengea utaratibu wa kujifunza kwa kuasoma vitabu, lakini kitu kingine muhimu sana ni kwamba unapaswa kufanyia kazi kile ambacho unajifunza kwa vitendo. Mara zote fanyia kazi kile unachojifunza. Ukichukua kitabu na kukisoma, kamwe, usibaki tu kuwaambia watu kuwa ulisoma hiki kitabu. Badala yake, soma hicho kitabu kwa lengo kwamba utapata kitu ambacho utafanyia kazi kwenye maisha yako au biashara yako. kitu hiki utakachopata kama utakifanyia kazi, ni wazi kuwa utakuwa una uwezo wa kukua na kutoka hapo ulipo na kwenda hatua ya ziada.

    SOMA ZAIDI: Kitu kimoja unachopaswa kufanyia Kazi kwa uhakika 2024

    Nne, penda na kuwa mtu wa kutumia teknollojia. Ukweli ni kuwa teknolojia mpya zinazidi kugunduliwa kil asiku. Na kadiri hizi teknolojia zinavyozidi kugunduliwa ndiyo kunakuwa na mabadiliko makubwa ambayo yanayokea. Ikumbatie teknolojia, teknolojia, na itumie teknolojia na hasa kwenye biasara yako.

    JIFUNZE ZAIDI: Jinsi Ya Kudandia Teknolojia Mpya

    Kitu cha tano na cha mwisho ambacho kitakufanya uwe na ukuaji kwenye maisha, kwenye biashara na kwenye maisha yako kiujumla ni kujifanyia tathmini. Tathmni ni moja ya kitu muhimu sana , ili kuona ni wapi umetokea, ni wapi umefikia na wapi unaelekea. Kwenye kila kitu ambacho unafanya, jifanyie tathmini. Tathmini ni muhimu kwa ukuaji wako. Hivyo mara zote jifanyie tathmini.

    Kama una mtoto utakuwa unajua wazi kuwa kila mwezi mtoto wako lazima apelekwe hospitali kwa ajili ya kliniki. Lengo la hii kiniki ni kujifanyia tathmini. Na lengo la tathmini hii ni kukusaidia kuboresha kile unachofanya, ili uweze kupata matokeo makubwa zaidi.

    SOMA ZAIDI: Kafanyaje huyu?

    kwa leo naishia hapo.

    Mimi naitwa Godius Rweyongeza

    Kwa mawasiliano zaidi: 0655848392

    Karibu sana

  • Huu Ndiyo Uwekezaji Bora Ambao Unapaswa Kuupa KIPAUMBELE sasa

    Hata kutunza familia ni uwekezaji. Ila uwekezaji baba ambao unapaswa kufanya mara zote ni

    1. KUWEKEZA KWENYE biashara. Huu ni uwekezaji Muhimu ambao Kila mmoja anapaswa kuufahamu. Sote tunamfahamu Warren kama mwekezaji Bora kuwahi kutokea, ila ukweli ni kuwa Warren Buffett siyo TU mwekezaji kwenye solo la HISA,Bali amewekeza kwenye biashara yake.


    Hivyo, WEKEZA kwenye biashara

    Anzisha biashara, endesha biashara Yako, KUZA BIASHARA Yako.

    Ukiwa na biashara unaweza kufanya karibia chochote unachotaka.

    Unaweza KUWEKEZA KWENYE biashara nyingine zaidi. Unaweza KUWEKEZA KWENYE soko la HISA n.k

    Hivyo, Anza KUWEKEZA KWENYE biashara kama ulikuwa hujaanza. Huku ukiendelea na mpango wako wa KUWEKEZA KWENYE soko la HISA na hasa Kwa kuanzia KUWEKEZA KWENYE VIPANDE

    Kama ungependa ushauri zaidi kuhusu uwekezaji.  Tafadhali wasiliana nami Kwa 0655848392

    Karibu sana

  • Huu ndio uwekezaji Bora kuliko wote

    Rafiki yangu, Kuna uwekezaji Bora kabisa kuliko uwekezaji wowote. Unajua uwekezaji huu ni upi?

    Ni KUWEKEZA KWENYE maarifa. Huu ndiyo uwekezaji Bora kabisa.

    WEKEZA kwenye maarifa mara zote

    WEKEZA kwenye maarifa.

    WEKEZA kwenye KUSOMA VITABU

    Hu ndiyo uwekezaji Bora kwako Kufanya.

  • Nimeandaa kozi fupi kwa ajili yako

    Rafiki yangu…………….

    Moja ya kitu ambacho ninapokea karibia kila siku, ni ombi la watu wakiniomba vitabu mbalimbali vya kiingereza. Wapo wanaoomba niwatafutie hivi vitabu kwa njia ya mtandao, halafu niwatumie.

    Sasa kitu kimoja ninachojua ni kwamba, nikipakue kitabu nikakutumia, ninakuwa sawa na mtu ambaye nimekupa samaki. Unajua ninaposema kwamba ninakuwa kama mtu ambaye nimekupa samaki ninamaanisha nini?

    Ili unielewe vizuri tuanze na usemi wa kihenga unaosema kwamba;

    Give a man a fish, and you feed him for a day; show him how to catch fish, and you feed him for a lifetime.

     

    Ikiwa inamaanisha kuwa;

    Mpe mtu samaki, nawe utamlisha kwa siku moja; mwonyeshe jinsi ya kuvua samaki, nawe unamlisha maisha yake yote.’

    Sasa mimi sitaki nikulishe kwa siku moja kwa kukupa samaki

    Nataka ujue kuvua..

    Siyo tu ujue kuvua, bali ujue kuvua na uwe na bwawa lako mwenyewe ambapo utaweza kuvua bila bughudha.

    Ndiyo maana, nimeamua kukuandalia kozi fupi tu, inayokuonesha namna ya kupakua vitabu mtandaoni.

    1. Ina njia ya uhakika
    2. Imetumiwa na watu zaidi elfu moja kwa mafanikio. Ukiitumia wewe pia utafanikiwa.
    3. Ni rahisi kufanyia kazi.
    4. Ni njia ambayo utaitegemea kwa miaka yako mingi inayokuja. Nimekuwa naitumia kwa zaidi ya miaka sita sasa. Itumie kwa manufaa yako pia.

    Kupata njia hii na mengine zaidi. Utapayapata kupitia kozi hii fupi ambayo nimeandaa

    BONYEZA HAPA KUPATA KOZI

  • Kitu kimoja ambacho kimenishangaza

    Juzi nilijaribu kutuma hiki kitabu cha MAAJABU YA KUSOMA VITABU kwenye makundi ya whatsap. Cha kushangaza ni kwamba kuna watu hawajawahi kupata hiki kitabu. Walikisoma na wengi waliweza kupata mrejesho ambao ni chanya, namna ambavyo kimebadili maisha yao.

    Wengine walishakisoma, ila kitendo cha kurudia kukisoma juzi, kiliwapa hamasa kubwa kwa mara nyingine na kuwafanya wajisikie wapya.

    Nimeona kwamba inawezekana hata hapa, inawezekana kuna watu hawajahi kupata hich kitabu au wengine wameshakisona na wangependa kukipata kwa mara nyingine. Ndiyo maana nimeona kwamba nikutumie na wewe….

    KWA HIYO, kama wewe umeweza kusoma hiki kitabu, inawezekana ukakisoma tena, kitakufaa sana.

    Kama hujawahi kukisoma, sasa ni muda mzuri wa wewe kukisoma.

    BONYEZA HAPA KUKIPAKUA

    Ukiataka kupata vitabu zaidi: wasiliana na 0684408755

    Mimi ni Godius Rweyongeza

    Karibu sana.

    NB: Unaweza pia KUPATA VITABU VYANGU ONLINE HAPA

    au HAPA

    JIFUNZE ZAIDI KWENYE BLOGU KWA KUBONYEZA HAPA

    JIFUNZE ZAIDI KWENYE YOUTUBE CHANNEL KWA KUBONYEZA HAPA

  • Jinsi ya kupakua vitabu unavyopenda kwa njia ya mtandao.

    Karibia kila siku huwa napokea ujumbe wa mtu ambaye ananiambia kwamba angependa kupata kitabu fulani na hasa vitabu vya kiingereza.

    Inawezekana na wewe kuna kitabu ambacho umekuwa unatamani kupata kwa siku sasa, ila hujui namna ya kukipata. Karibu kwenye kozi hii fupi.

    Ambapo unaenda kujifunza namna ya kupakua kitabu chochote (online). Hii ni kwa vitabu vya kiingereza tu.
    Kwenye kozi nitakuonesha hatua kwa hatua namna ya kufanya hivyo.
    Nitakuonesha machimbo mbalimbali muhimu vilipo vitabu ambayo unaweza kuyatumia mwenyewe kutafuta na kupata vitabu unavyotaka kwa uhakika wa asilimia (95-99.999) bila kukosa!

    Kama upo tayari.

    Utalipia 10,000/- tu. Kisha nitakuunga kwenye hii kozi. Na utapata mafunzo haya.

    Hutatoa tena gharama yoyote kununua softcopy ya kiingereza.

    Kama upo tayari, lipia 10,000/-
    Namba ya malipo ni 0684 408 755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Lipia sasa ili upate hii kozi.

    AU

    BONYEZA HAPA KUPATA KOZI

X