Author: Godius Rweyongeza

  • Vitengo Vitatu Ambavyo Vipo Kwenye Kila Biashara.Hata Kwenye Biashara Yako Vipo Hata Kama Hujui. Virasimishe Sasa

    Siku za nyuma nilikuwa najiuliza maswali mengi ambayo hayakuwa na ukomo. Hivi huwa inakuwaje kunakuwa na vitengo kwenye biashara au taasisi. Ni nini ambacho huwa kinafanyika mpaka watu wanajua kitengo fulani na fulani vinapaswa kuwa sehemu tofauti? Biashara inapaswa kuwa imefikia ngazi gani ili kuweza kuwa na hivyo vitengo vyote? Siku ya leo ninaongelea vitengo…

  • Aina Tano (05) ya watu ambao kila mfanyabiashara anapaswa kujenga nao urafiki wa karibu

    Rafiki yangu wa ukweli salaam. Hongera sana kwa siku hii nyingine ya leo. Leo nataka kukwambia aina tano ya watu ambao kama mfanyabishara unapaswa kuanza kujenga nao urafiki mapema. Unapaswa kuanza kujenga urafiki wa namna hii mapema sana bila kujali biashara yako ni ndogo au kubwa. #1. ni wanasheria. Hawa ni watu muhimu sana kwenye…

  • Epuka Makosa Haya Matano (05) Kwenye Biashara Yako

    Rafiki yangu mfanyabiashara, Leo nataka nikuainishie MAKOSA matano ambayo wafanyabiashara Wengi hufanya. Tafadhali hakikisha kwamba unayaeouka Haya MAKOSA Kwa manufaa ya biashara Yako ya Sasa na baadaye Kosa la kwanza: kutioipa biashara Yako jina. Labda nianze Kwa kukuuliza jina biashara Yako ni lipi? Kama biashara Yako Haina jina unakosea sana. Mtoto akizaliwa anapewa jina Wewe…

  • Huu Ndiyo Muda Mzuri wa Kusema Kwamba Umefanya Mauzo Kwenye Biasshara yako

    Rafiki yangu wa ukweli, salaam. Hongera sana kwa siku hii njema ya leo. Kwenye biashara kuna kitu kimoja tu ambacho watu huwa wanakosea. Na kitu hiki huwa ni kuhesabu vifaranga kabla havijatotolewa. Yaani, kuhesabu kwamba wameuza wakati bado kabisa hawajauza. Unakuta mtu anahesabu kwamba ameuza pale anapoahidiwa na mteja kwamba atakuja. Au anahesabu kwamba ameuza…

  • Aina za mazoezi Unayopaswa kuwa unafanya

    Mazoezi ni sehemu muhimu ya maisha yetu. Kuna aina tatu ya mazoezi ambayo unapaswa kufanya kila siku, unajua ni aina zipi? Mazoezi ya mwili. Kama kukimbia, Kwa siku tenga walau musu saa Kwa ajili ya hili Mazoezi ya akili. Haya niazoezi unayafanyia Kwa kujifunza, KUSOMA VITABU na kupata mafunzo ya semina n.k Mazoezi ya kiroho.…

  • Jinsi Ya Kujilipa Mshahara Kutoka Kwenye Biashara Yako. Njia Mbili Zilizothibitishwa

    Changamoto kubwa ambayo imekuwa inawakumba wafanyabiashara wengi ni kuchanganya pesa zao na pesa za biashara. Makala ya leo, inaenda kuwa mwarobaini wa hili. Sikiliza uhusiano mkubwa uliopo kati yako wewe na biashara yako ni kwamba wewe ni mmiliki wa biashara, lakini fedha za biashara haupaswi kujimilikisha na kuzifanya kuwa za kwako. Fedha za biashara ni…

  • Kanuni Ya Miezi Sita Kwenye Biashara, Na Kwa Nini Kila MfanyaBiashara Anapaswa Kuifahamu

    Kuna kanuni ya miezi sita kwenye biashara ambayo wafanyabiashara wengi hawaifahamu. Ni kanuni muhimu ambayo kama mfanyabiashara unapaswa kuifahamu. Kutoifahamu kanuni hii kutakuponza sana Kanuni hii inasema kwamba, ukianza kufanya biashara, ndani ya miezi sita ya kuanza biashara kuna watu wengine wataanzisha biashara kama hiyo. HII kanuni inafahamika kama kanuni ya copy cat. ikimaanisha kwamba…

  • Viashiria kumi na sita (16) Kuwa Umebeba Ajira Za Watu

    Rafiki yangu mpendwa salaam, ujue mara kwa mara nimekuwa nakwambia kwamba inawezekana wewe umezaliwa kuajiri na siyo kuajiriwa. Siku ya leo ninaenda kukuonesha viashiria ishirini ambavyo vinaonesha kuwa wewe umebeba ajira za watu. Baada ya kuwa umesoma hapa sasa, kazi itabaki kwako kuhakikisha umefanyia kazi haya utakayokuwa umejifunza au la 1. Kiashiria cha kwanza kwamba…

  • UTABIRI: Kitu Kimoja Ambacho Ni Uhakika Hakitatokea Maishani Mwako

    Rafiki yangu wa ukweli, bila shaka unaendelea vyema kabisa na shughuli zako za kila siku. Siku ya leo nimekuandalia makala ya kushangaza kidogo. Na makala hii ni utabiri. Mimi syo mtu ninayeamini sana kwenye tabiri, unabii na vitu vinavyoendana na hili. Ila leo nimevutwa kukupa utabiri huu, na ninatoa utabiri huu nikiwa na uhakika kuwa…

  • Iga Ufe

    Kuna baadhi ya vitu huhitaji kuiga kwa watu wengine.  Badala yake unapaswa kuvifanya kulingana na wewe mwenyewe. Siyo kila kitu wanachofanya wengine kinaweza kukufaa na wewe pia. VIngine vinaweza kuwa sahihi kwao, lakini siyo sahihi kwako. Ni muhimu kwako kufahamu kipi ni sahihi kwako, na kuwekeza nguvu yako kubwa hapo. Kuna watu wanakopa na mshahara…

  • KIPAJI NI DHAHABU: Ila hapa kuna vitu vitano ambavyo kila mwenye kipaji anapaswa kufahamu

    Juzi kuna mtu alinifuata kikashani kwangu whatsap na kuniuliza, mbona kijana yule mwenye kipaji ameshindwa kusaidiwa?  Nilimwuliza kijana yupi? baadaye kidogo alinitumia picha za yule kijana pamoja na kazi alizofanya.  Nilitakafari hili kidogo, ila nikaja kugundua kwamba watu wenye vipaji kuna vitu vitabo muhimu ambavyo hawafahamu. Ningependa na wewe ufahamu hivi vitu, kuanzia leo hii,…

  • Kipaji chako umekiweka wapi? Umeajiriwa, umejiajiri au huna ajira?

    Dhahabu ni madini yenye thamani sana hapa duniani. Siku ya leo tarehe 29/3/2024 wakati naandika hapa, imabidi niangalie mtandaoni ili kuona bei halisi ya dhahabu sasa hivi kwenye soko la dunia. Ninachoona hapa ni kwmaba bei ya dhahabu kwenye soko la dunia siku ya leo ni kati ya dola 70,000 na dola 75,000 kwa kilo…

  • Acha Uvivu, Fanya Jambo Hili Kila Siku Bila Ya Kuacha

    Kufikiri ni jambo ambalo tunapaswa kulifanya kila siku. Wengi hudhani wanafikiri lakini kumbe siyo. Kufikiri ni kazi ambayo hatupaswi kuikwepa. Inapaswa kuwa sehemu aya maisha yetu ya kila siku. Hakuna mtu ambaye anawez akufanya hiki kitu kwa ajili yako. Kuna vitu unaweza kuwapa watu na wakafanya hivyho vitu ila huwezi kuifanya wewe. Jipe kazi ya…

  • Nguvu Ya Mtazamo (Ninalipwa laki mbili ndiyo maana mimi ni maskini vs Ninalipwa laki mbili ndiyo maana mimi ni tajiri)

    Rafiki yangu, mtazamo ni moja ya kitu muhimu sana hasa linapokuja suala la mafanikio. Mtu afikirivyo ndivyo anavyokuwa. Hivyo, kama unataka kufanikiwa, unapaswa kubadili mtazamo wako kutoka kuwa mtazamo hasi na kuw amtazamo chanya. Unapaswa kubadili mtazamo wako na kuanza kuona uchanya kwenye kile unachofanya. Hali na matukio mbalimbali yanayotokea kwenye maisha yako, badala ya…

  • Pesa Zako Zimejificha Kwenye Hiki Kitu

    Miaka kadhaa iliyopita, mtandaoni kulikuwa na picha ya mtoto mdogo iliyokuwa inasambaa kama moto wa kifuu. picha hii ilikuwa ikimwonesha mtoto mdogo tu, ambaye aliajiriwa na kampuni kubwa ya Google. Sasa swali kubwa ambalo unaweza kuwa unajiuliza, ilikuwaje huyu mtoto mdogo akaajiriwa na kampuni kubwa kama GOOGLE. Jibu ni moja tu, huyu mtoto alikuwa anajua…

  • Unajua Nini Kuhusu Bitcoin?

    Habari za Bitcoin sijui. Ila Habari za HISA, HATIFUNGANI NA vipande, nazijua. Niulize chochote kuhusu HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE nitakujibu. Na Tena ukitaka kuwa deep, basi hiki kitabu Cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE kitakuhusu.Na halafu utakipata Kwa bei nzuri TU. Hardcopy ni 25,000/-Softcopy ni 10,000/- Tumia namba ya simu 0684408755 Karibu…

  • Mshangao! Jinsi Muda Ulivyo wa Dhahabu Kwa Mfanyabiahsara na Mtu yeyote makini

    Leo nakuruhusu ufanye kitu kimoja tu, uzunguke popote pale hapa duniani, halafu  uje kuniambia ni wapi umekuta wanaweza kuongeza kiwango cha muda ndani ya siku. Ni wapi ambapo mtu anaweza kuwa na saa moja, lakini akaomba kuuongezewa saa jingine zaidi na akaongezewa? Ni wapi ambapo mtu anaweza kukopesha muda wake wa leo ili aje alipwe…

  • Mbinu Tano (05) Za Kudai Hela Uliyomkopesha Mzazi Wako

    1. SHERIA ya kwanza wazazi wape Hela ya kula2. SHERIA ya pili, usikopeshe Hela kama biashara Yako siyo kukopesha3. SHERIA ya tatu, wasaidie wazazi kuhakikisha wanakuwa na VYANZO vitakavyowaingizia KIPATO Ili wasikutegemee.4. SHERIA ya nne, ukimkopeshe mtu yeyote, mkopeshe Ile Hela ambayo wewe mwenyewe huihitaji.5. SHERIA ya Tano, kamwe watu wasijue lini Huwa unaingiza Fedha.…

  • Huu Ndiyo Ustaraabu Wa Hali Ya Juu Ambao Unapaswa Kuwa Nao

    Rafiki yangu wa ukweli, salaam. Hongera sana kwa kazi, siku ya leo, nataka kuongea na wewe kuhusu ustaraabu. Mara nyingi watu huwa wanapenda kuonesha ustaraabu kwenye maeneo tofautitofauti. Ila leo hii ninataka nikwambie kuhusu ustaraabu wa hali ya juu ambao unapaswa kuwa nao. Na aina hii ya ustaraabu ambayo unapaswa kuwa nayo ni kufanya kile…

  • Njia Tatu Za Uhakika Zitakazokusaidia Wewe Kuweka Akiba Bila Ya Kutoa (Namba 3 Ndiyo Yenyewe Haswa!)

    Wahenga wanasema kwamba ukiona vyaelea, basi ujue vimeundwa, hivyohivyo ndivyo ilivyokuwa kwa mji wa Babilon (Babeli) ambao kwa nyakati zake ulikuwa mji tajiri na wenye watu wenye utajiri. Simulizi zake na busara za nyakati hizo zimebaki vitabuni kwa ajli yetu sisi vijana wa miaka yetu kuzitumia kwa manufaa. Lakini moja ya kitu kimoja na kitu…

X