Unapaswa kuwa na vyanzo vingi vya kipato, la sivyo utakuwa na vyanzo vingi vya mahangaiko


Rafiki yangu mpendwa Salaam

Sina shaka unaendela vizuri kabisa

Siku ya leo nataka kukwambia kwamba unapaswa kuwa na vyanzo vingi vya kipato la sivyo utakuwa na vyanzo vingi vya mahangaiko. Hata hivyo, kabla hujaishia hapa na kwenda kukimbizana kuanzisha vyanzo vingi vya kipato. Ningependa tu uwe na subira, nasema uwe na subira kwanza ili usome makala hii mpaka mwisho ndiyo uende kufanyia kazi kile utakachojifunza.

Kuwa na maarifa nusu ni hatari sana. Hivyo kusoma makala nusunusu ni hatari na kunaweza kusiwe na manufaa kwako kama kuisoma makala yote kamil.

Namaanisha nini ninaposema vyanzo vingi vya kipato

Vyanzo/chanzo kwa umoja ni chimbuko la kitu fulani. Vyanzo vya kipato ni chimbuko la fedha ambazo unakuwa unapata. Hivyo ninaposema kwamba uwe na vyanzo vingi vya kipato, maana yake uwe na machimbuko mengi yanayokuingizia kipato kwenye akaunti yako ya benki.

Chanzo maarufu ambacho kimezoeleka kwa watu wengi, ni chanzo cha mshahara. Hata hivyo, kwenye ulimwengu wa leo, kuwa na vyanzo vingi siyo tena ombi. Ni lazima

Na ukweli ni kwamba siyo vigumu kiviiile kutengeneza vyanzo vingi vya kipato kwenye ulimwengu wa leo. Lakini pia siyo rahisi kama unavyoweza kufikiria.

Changamoto iliyopo unapokuwa na chanzo kimoja cha kipato

Unapokuwa na chanzo kimoja cha kipato ni kwamba chanzo hicho kinaweza kukwama kipindi fulani na hivyo kukufanya usiweze kuingiza pesa kama ambavyo unakuwa unataka. Au pale chanzo hicho kinapochelewa kuingiza kipato na kama ulivyokuwa unategemea basi moja kwa moja unakuwa unaenda kugonga mwamba.

Jinsi ya kuondokana na changamoto ya chanzo kimoja cha kipato

KWENYE biashara na kwenye maisha, hakuna namba mbaya kama sifuri na moja. kitu chochote kile unachozidisha na mojakinabaki kuwa vilevile. Wakati ukizidisha kitu chochote na sifuri kinabaki kuwa sifuri.

Hivyo rafiki yangu, ninachotaka kukwambia hapa ni kwamba unapaswa kuepuka kitu hiki kwenye maisha yako rafiki yangu. Epuka kuwa na chanzo kimoja cha kipato kadiri uwezavyo. Usiwe mtu ambaye unasema kwamba hauna kitu cha kufanya (Yaani 0) na wala usiwe mtu ambaye unategemea chanzo kimoja cha kipato. Badala yake kuwa na vyanzo vingi vya kipato. Yaani, walau kuwa na vyanzo vinne au vitano na zaidi vya kipato.

Usipokuwa na vyanzo zaidi ya kimoja cha kipato, ni suala la muda tu utaanza kuwa na vyanzo vingi vya mahangaiko. Unajua kwa nini? kwa sababu utaanza kujiingiza kwenye kukopa,  utaanza kujiingiza kwenye vikoba, utaanza kufanya vitu vingi ambavyo siyo sawa na mwisho wa siku utakuta kwamba umeanza kuwa na vyanzo vingi vya mahangaiko.

Suluhisho la hili rafiki yangu ni kuhakikisha kwamba unakuwa na vyanzo vingi vya kipato. Vyanzo vingi vya kipato vitakusaidia wewe kujiondoa kwenye majanga kama hayo ya mikopo lakini pia kukupa kipato pale unapokuwa unakihitaji.

Kuhakikisha kwamba unapata mwongozo wa kukutosha kwenye kutengeneza vyanzo vingi vya kipato. Nimeandaa ebook. Ebook yenyewe hii hapa

Kwenye ebook hii unaenda kujifunza yafuatayo.


2 responses to “Unapaswa kuwa na vyanzo vingi vya kipato, la sivyo utakuwa na vyanzo vingi vya mahangaiko”

  1. Nashukuru sana kuwa miongoni mwa wanadamu siku ya mwanzo mwa mwezi wa tano kupata madini haya adhimu,hakika nitajibidisha kufanya kazi,kuongeza maarifa yatakayoniongezea juzi nyingi za namna ya kutatua matatizo ya watu wengi zaidi.maana kupitia kutatua matatizo ndio chanzo Cha ukwasi.

  2. Ni kweli kabisa lazima uwe na vyanzo vingi vya kupata kipato basi mm niwe wa kwanza kupata hicho e-book na bei yake ni shilingi ngap

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X