Uchambuzi wa kitabu cha NO excuses


Kitabu: No Excuse
Mwandishi: Brain Tracy
Mchambuzi: Hillary Mrosso

Utangulizi

Mwandishi wa kitabu hiki anataka tuwe watu wa matokeo na sio watu wa kutoa sababu kwanini hakuna matokeo. Maneno kidogo kazi zaidi, matokeo zaidi. Karibu tujifunze mambo 100 niliyoyaona ndani ya kitabu hiki kizuri.

  1. Kuna sababu zaidi ya 1000 kwa nini umeshindwa kufanya jambo fulani, lakini hakuna sababu nzuri kati ya hizo za kwanini umeshindwa.
  2. Kanuni ya kwanza ya mafanikio ni kujitoa kwenye kundi la wanaolalamika na kutoa sababu nyingi za kushindwa kufikia malengo yako na kuingia kwenye kundi la watendaji.
  3. Usiwe tena na visingizio vya kwanini hujafanya hiki au kwanini hujaweza kufikia malengo yako. Ondoa sababu na visingizio, maneno kidogo matokeo zaidi.
  4. Usitumie ubongo wako wa thamani kuunda au kujaribu kujitetea kwanini hujachukua hatua kufikia malengo yako, au kukamilisha mambo muihimu kwenye maisha yako.
  5. Mwandishi anataka tujiulize, je kuna mtu yeyopte duniani mwenye sababu na visingizio kama mimi na amefanikiwa? Usikubali sababu zikwamishe kufikia malengo yako.
  6. Fanya kitu na maisha yako, fanya tu jambo fulani muhimu na maisha yako, acha kutoa visingizio na sababu, sababu hazitakuletea mafanikio, just do something.
  7. Jishangaze wewe mwenyewe kwa kuwa mtendaji na kuondoka kwenye kundi la watu wa visingizio na maneno mengi. Maneno mengi hayatakuletea mafanikio, matendo na kuchukua hatua ndio huleta mafanikio.
  8. Unatakiwa kuwa na nidhamu ili uweze kuchukua hatua kufikia ndoto zako, bila nidhamu utakuwa mtu wa maneno meeengi, utakuwa na visingizio vingi na sababu zisizoisha.
  9. Ndidhamu binafsi ni ile hali ya kufanya jambo fulani ulilotakiwa kufanya kwa wakati ulioupanga, bila kujali unajisikia kufanya au hujisikii.
  10. Nidhani binafsi ndio huwafanya watu wa kawaida wasio na vipaji wala kudhaniwa kuwa na uwezo mkubwa kufanya mambo makubwa kwa ufanisi mkubwa.
  11. Mwandishi Brain anasema jambo la muhimu kwenye maisha yetu ni kuwa na nidhamu binafsi, anashauri tujidhibiti, tujiweze, tujitawale.
  12. Mafanikio yatakuwa yako pale ambapo utaweza kuthibiti hisia zako, hamu au matamanio yako na mitazamo yako.
  13. Watu wenye mafanikio makubwa ni wale wanaofikiri kwa mapana na kwa miaka mingi ijayo yaani long-term thinkers.
  14. Watu waliofanikiwa kwenye maisha wanafanyia kazi sana eneo lao la nidhamu binafsi kila mara.
  15. Kuwa na nidhamu kali ya kufanya kile ambacho ni sahihi.
  16. Watu waliofanikiwa wana tabia ya kufanya yale ambayo watu wasiofanikiwa hawafanyi.
  17. Tabia mbaya ni rahisi kuzitengeneza lakini ni ngumu kuishi nazo, lakini tabia njema ni ngumu kuzitengeneza lakini ni rahisi kuishi nazo.
  18. Kila tabia inafundishika na inawezkeana kujifunza na kuwa na tabia hiyo. Hivyo amua kuingiza na kujifunza tabia unazozitaka kwenye maisha yako.
  19. Kila unapojitahidi kutengeneza nidhamu kwenye eneo fulani la maisha yako, unatengeneza na kuimarisha eneo lingine la maisha yako.
  20. Kila unapokazana kutengeneza nidhamu kubwa kwenye maisha yako, ndio unavyoongeza Kiwango cha kujipenda na kujikubali. Watu wanaojipenda wanatenga muda wa kutengeneza mambo muhimu kwenye maisha yao.
  21. Kuna amani, furaha, hali ya kujiamini na kujipenda pale unapoongeza nidhamu kwenye maisha yako. Usikubali maisha yako yaende tu bila muongozo maalumu, dhibiti na amua vitu unavyosimamia kwenye maisha yako.
  22. Nidhamu itakufanya uishi maisha bora, maisha ya uhuru na salama, nidhamu itakuepusha na mambo mengi magumu, nitamu itakuvusha kwenye milima na mabonde ya maisha.
  23. Mwanafalsafa mahiri wa siku nyingi Plato aliwahi kusema, ushindi wa kweli ni ushindi unaopata dhidi yako mwenyewe. Maana yake pata ushindi kwenye mambo yaliyoko kwenye maisha yako ambayo yanakupa changamoto. Pata ushindi dhidi ya tabia mbaya zilizopo kwenye maisha yako.
  24. Inapofikia suala la kufanyia kazi ndoto zako, mawandishi anasema kuwa tayari kufanya kazi kwa muda mwingi zaidi kuliko mtu mwingine. Jitoe zaidi ya wengine kufanya kazi bora kwa muda wa kutosha.
  25. Utayari wa kuendelea kufanya kazi zako kwa muda mrefu zaidi unaupata pale unapokuwa na nidhamu kwenye maisha yako.
  26. Usipokuwa na nidhamu kwenye maisha yako, maana yake umewaachia wengine kazi ya kukusimamia, kukutawala, kukuongoza nk. Nidhamu itakufanya uwe kiongozi, maneja na bosi wa maisha yako.
  27. Kuna kanuni ya mafanikio inasema, kama utafanya kile ambacho waliofanikiwa wanafanya mara kwa mara bila kuachaa, hakuna kitakachokuzuia kufikia mafanikio unayaoyatafuta.
  28. Kila kilichopo kwenye maisha yako ya sasa ni matokeonya mambo uliyoyafanya siku za nyuma. Maana yake kila unachokivuna ni matokeoa ya kila ulichopanda siku za nyuma kwenye maisha yako.
  29. Mafanikio ni kujua kile unachokitaka kwenye maisha yako, kujua gharama ambazo utaingia kufikia mafanikio hayo, na kunuia au kudhamiria kulipa gharama hizo ili kufikia mafanikio yako.
  30. Upo tayari kiasi gani kulipa gharama za kufikia mafanikio unayoyataka? Fikiria tena kwa upya kama upo tayari ili uchukue hatua mara moja.
  31. Lipa gharama zote, na sio ulipe nusu nusu, lipa gharama zote kufikia mafanikio yako, hakuna njia ya mkato kwenye mafanikio ya kweli.
  32. Gharama za mafanikio zinalipwaga zote na zinalipwa kwanza kabla ya kuyapata mafanikio, maana yake inahitaji zaidi dhamira ya kweli kwenye safari ya mafanikio, hutaweza kufikia mafanikio unayotaka kama utakosa uvumilivu kwenye mchakato.
  33. Mwandishi anasema kuwa mbobezi kwenye eneo lako, maana yake kuwa mtaalamu uliyebobea kwenye jambo unalolifanya kama ni taaluma, kazi, Sanaa, biashara, au ujuzi ulio nao.
  34. Kuwa na mipango ya muda mrefe ya kuboresha ujuzi ulio nao, noa ujuzi ulio nao kila mara ili uwe mbobezi na uweze kuleta mafanikioa makubwa yatakayoacha alama.
  35. Faya yale yaliyo magumu lanini ni ya muhimu zaidi, kuliko kufanya vitu vyepesi visivyo na umuhimu, Brain Tracy anasema tumia nidhamu kali kwenye kufanyia kazi jambo hili maana sio rahisi.
  36. Ili uwe mtu ambaye hujawahi kuwa kabla fanya vitu ambavyo hujawahi kuvifanya kabla, maana yake kama unataka kuwa mtu wa tofauti fanya vitu tofauti, kama unataka kubakia yule yule miaka yote fanya yale yale uliyofanya maiaka yote.
  37. Zawadi kuu ya maisha ya mafanikio sio fedha utakazozipata, bali ni aina ya mtu bora utakayekuwa baada ya kufikia mafanikio.
  38. Wajibika kwa viwango vya juu sana kwenye maisha yako, ingia kwenye majukumu makubwa ya kuboresha maisha yako kuliko matarajia ya watu kwako.
  39. Shika hatamu ya maisha yako, usimpe mtu mwingine Jukumu hili, wajibika asilimia 100, hakikisha unakuwa na udhibiti wote wa maisha yako.
  40. Itakuhitaji utumie nguvu ya zaida kubadili maisha yako kuwa bora, itakugharim sana nguvu na nia ya kweli ya mabadiliko.
  41. Itakuchukua nguvu ya ziada ili kufanya kitu sahihi kila mara na kwenye hali zote.
  42. Tengeneza uaminifu na kuaminiwa kwenye maisha yako, na ukishatengeneza ulinde uaminifu wako kwa gharama zote.
  43. Maisha yanakuja kwetu kama mitihani na majaribio ili kutupima kama tupo tayari au tuna maanisha kwenye safari yetu ya mafanikio, kila hatua itakutaka kufanya maamuzi sahihi na kufanya kitu sahihi.
  44. Kila maamuzi utakayofanya yaaonysha thamani yako na hadhi yako. Hivyo chukulia kwa uzito maisha yako.
  45. Kila kitakachokuwa kinachukua muda na guvu zako kwa muda mrefu ndio kitatokea kwenye maisha yako. Hakuna kinachotokea kwa bahati mbaya kwenye maisha yako.
  46. Kumbuka changamoto hazitufanya kuwa watu fulani, bali zinatuonyesha sisi ni watu wa aina gani, hivyo zitumie changamoto kwa faida ya kuboresha zaidi.
  47. Mwanadamu mwenye hadhi ya chini sana hapa duniani ni yule ambaye hana maadili, hana tabia njema na hana misingi bora anayosimamia, yupo yupo tu, hana lengo lenye maana analotaka kukamilisha.
  48. Linda maadili na thamani yako isichafuliwe na mienendo ya maisha yako, linda jina lako lisichafuliwe na kashfa au sifa mbaya, linda sana hadhi yako isihusishwe na mambo mabaya.
  49. Jinsi unavyojipenda mwenyewe zaidi ndio jinsi utawapenda na wengine zaidi, na kwa kufanya hivyo upendo mwingi unarudi kwako.
  50. Fikiria tungekuwa na dunia gani kama kila mtu angekuwa anafanya na kufikiri kama wewe? Fikiria dunia ingekuwaje kama wote tungekuwa kama wewe.
  51. Dhamiria kuwa mtu bora kabisa kuwahi kuishi hapa duniani, kwa kufanya kazi bora, kuishi kwa nidhamu na kuacha kulalamika.
  52. Tathimini maisha yako, na ukiona hayakuridhishi yabadilishe ili yakuridhishe na yakufurahishe, kumbuka hakuna anayekuja kukusaidia kubadili au kukupa maisha mazuri, ni wewe mwenyewe unatakiwa kufanya maamuzi magumu ya kuyafanya maisha yako yawe bora.
  53. Usiishi kwa mkumbo, jifanyie upembuzi yakinifu kila mara, jikague kila mara, na jisemee moyoni mwako, kweli haya ndio maisha ninayoyataka? Haya ndio maisha niliyochagua kuishi? Kicha chukua hatua mara moja kuyafanya maisha yako kuwa mazuri.
  54. Jiwekee utaratibu wa kujisomea vitabu bora kabisa ili uweze kuwa na mawazo, fikra bora za kukusaidia kufanya maamuzi mazuri kwenye maisha yako, jizoeshe kuwa msomaji wa vitabu.
  55. Mwandishi anasema kila mtu anayetaka kufikia kilele cha mafanikio kwenye jambo lolote, anatakiwa kwanza kuwa na mtaji wa tabia bora za kumsaidia kufikia lengo hilo kubwa, pia amesema awe tayari kuvunja tabia zinazokinzana na mafanikio unayoyataka.
  56. Hakuna atakayefanya kwa ajili yako, kumbuka jambo hili kila siku, ni wewe unatakiwa kubeba Jukumu la kuishi maisha yako kwa asilimia 100.
  57. Jitolee maisha yako kama sadaka ili ujifunze bila kukoma, jitoe bila kujibakiza ili upate maarifa na ujuzi unaoutaka kwenye maisha yako. Jifunze bila huruma, fanya jambo hili la kujifunza kuwa ni jambo la maisha yako yote, kamwe usiache.
  58. Jifunze ujuzi mgumu ambao unahitajika sana kwenye jamii, tumia muda wako na nguvu zako kujifunza ujuzi mgumu wenye thamani kubwa ambao ukiujua sio tu utakuletea mafanikio bali utakufanya kuwa mtu bora kabisa.
  59. Mwandishi anasema itakugharimu nguvu kubwa sana ili uache kutoa visingizio, kutoa visingizio ni rahisi sana, mwandishi anasema kata kabisa kutoa visingizio na sababu, toa matokeo.
  60. Tabia hazitakiwi kuwa kikwazo kufikia mafanikio yako, tabia zinatakiwa kuwa ni nyenzo muhimu za kufikia mafanikio, zifanye tabia zako zikusaidia na sio zikuharibie.
  61. Dawa ya kuua malalamiko, visingizio na sababu ni kukubali majukumu, sema nakubaliana na majukumu yote ya maisha yangu.
  62. Kuwa na muda wa kutosha wa kufanyia kazi mambo yako ya maana nay ale muhimu, hii itakufanya ukose muda wa kaunza kutengeneza hisia hasi na kufuatilia maisha ya watu wengine.
  63. Katika maisha tunafanya kazi kukamilisha malengo yetu au tunafanya kazi kukamilisha malengo ya mtu mwingine. Kuwa na malengo yako binafsi unayoyafanyia kazi kila siku.
  64. Kila siku chukua kalamu na karatasi uandike malengo yako makubwa ya maisha yako, hii itakufanya ukae kwenye msitari na ukumbuke una majukumu muhimu kwenye maisha yako.
  65. Mwandishi anasema hakuna malengo yasiyofikiwa, bali kuna muda wa kukamilisha malengo usiofikiwa, maana yake malengo yako yanatakiwa kufanyika ndani ya muda maalumu, usiweke malengo yasiyo na muda, weka muda wa kufikia malengo yako.
  66. Kughairisha mambo kunaiba sana muda wako na maisha yako. Usighairishe mambo muhimu kwenye maisha yako, kama jambo ni muhimu kwenye maisha yako usiliache bila kufanya.
  67. Washindi ni wale wanaochukua hatua hata kama hawana uhakika na mafanikio watakayopata.
  68. Kuchukua hatua na kuanza utekelezaji maana yake kuna vitu unatatua, kuna hatua unapiga, hii ni bora kuliko kuacha kuchukua hatua.
  69. Brian Tracy anashauri tuandike kila njia ambayo tunafikiri ni suluhisho kufikia malengo yetu, kuwa na utaratibu wa kuandika mawazo yako unayodhani ni njia za kukusaidia kufikia malengo yako.
  70. Pangilia majukumu yako kwa vipaumbele, la muhimu zaidi ndio lianze kisha lifuate ambalo ni muhimu nk. Weka vipaumbele kwenye majukumu yako, hii itakusaidia kukamilisha mambo muhimu itakuondolea matumizi mabaya ya muda.
  71. Ukishaweka vipaumbele vyako usianze kusubiria hali iwe nzuri ndio uanze utekelezaji, anza utekelezaji mara moja, usipoteze muda, wala usitengeneze visingizio au sababu.
  72. Kila siku uwe na kitu unakifanya kinachokusukuma kuyafikia malengo yako, hata kama ni jambo dogo kiasi gani usidharau, endelea mbele.
  73. Kumbuka siku zote za maisha yako kuwa, uwezo wako wa kujifunza hauna kikomo, uwezo wako wa kujua mambo mapya hauna kikomo; hivyo usijiwekee ukomo kwenye fahamu zako.
  74. Kwasababu kuna wengi waliofanikiwa na kuwa matajiri ni ushahidi mkubwa kuwa hata wengine wanaweza kufikia mafanikio na utajiri mkubwa.
  75. Mwandishi anasema amua kuwa bingwa na mbobezi kwenye kile unachokifanya, kuwa na msaada na mchango tegemezi, watu wakutafute kwasababu unajua na unaweza kuwasaidia.
  76. Soma angalau dakika 60 kila siku kwenye kila kitu unachokifanya, boresha ujuzi wako kila siku kwa kusoma mawazo mapya.
  77. Sikiliza mafunzo yanayoelimisha kuhusu kile unachokifanya au ule utalaamu wako; kamwe usihitimu elimu yako.
  78. Hudhuria semina, kozi au mafunzo mbali mbali kwenye kuboresha ujuzi wako. Usiache kujifuza na kukua kila siku.
  79. Kama haukui maana yake unakufa, hakikisha unaongeza vitu vipya vya kukufanya kuwa bora, kukua na kuwa mtu bora na wa kipekee kwenye kazi yako, biashara, Sanaa, nk
  80. Mwandishi Brain anasema TV yako inaweza kukufanya kuwa tajiri endapo utaizima, maana yake usitumie muda mwingi kuangalia vipindi vya TV au kufuatilia mitandao ya kijamii, itakupotezea muda wako wa thamani kubwa.
  81. Lisaa la kwanza kwenye siku yako ni rada yako ya kukupa uelekeo wa siku yako, hivyo tumia vizuri lisaa la mwanzo wa siku yako.
  82. Ujasiri sio kukosekana kwa hofu, bali ni kuidhibiti hofu, kuitalwala hofu. Katika safari ya mafanikio tunahitaji sana ujasiri ili kuzuia hofu zisiturudishe nyuma.
  83. Ili utengeneza ubora ambao huna, unatakiwa kufanya kila kitu kwenye maisha yako kwa ubora unaotamani hadi ufikie ubora huo.
  84. Hakuna anayeweza kukufanya ukajihisi au kujisikia mnyonge na duni bila ya wewe kuruhusu kujisikia hivyo, usiamue udhaifu ndio utawale maisha yako.
  85. Kwenye maisha unahitaji ujasiri kila mahali, ujasiri wa kuchukua hatua, ujasiri wa kukataa kutoa sababu, ujasiri wa kuwa mvumilivu na kuendelea kuvumilia.
  86. Kuwa na ujasiri wa kuikabili hali inayokutia hofu, zikabili nyakati na hali unazoziogopa.
  87. Chukua hatamu ya kuzikabili na kuzithibiti dhoruba za moyo wako, maisha yametawaliwa na nyakati ngumu nyingi. Hivyo chukua uongozi wote wa maisha yako ili uzikabili bila uoga.
  88. Mark Twain aliwahi kusema, aliogopa vitu vingi sana kwenye maisha yako, na kati ya vingi alivyoogopa hakuna vilivyotokea kweli.
  89. Tegemea mabaya yanaweza kutokea kwenye maisha yako, usiogope na tengeneza ujasiri wa kukubali kila matokeo utakayoyapata.
  90. Anza mara moja kufanyia kazi mabaya au changamoto zilizotokea kwenye maisha yako, tafuta suluhisho la changamoto hizo.
  91. Kuwa kinganganizi kwenye safari yako, usiyumbishwa na kukosa muelekeo, kuwa buzi na majukumu yako, maana ndio yana maana sana kwako.
  92. Uvumilivu utakujengea misuli ya kusubiria na kukaa kwenye mchakato kwa muda mrefu, tengeneza na kubali kukaa kwenye mchakato wa mafanikio.
  93. Tengeneza nidhamu kubwa ya kukaa kwenye mchakato, hii itakufanya ujione mwenye heshima na kuongeza ujasiri na kujikubali.
  94. Kabla ya kuanza kufanya jambo kubwa na la muhimu kwenye maisha yako unaweza kujiambia kauli hii “sitakata tamaa, mimi sizuilike”.
  95. Hatakama utanguka chini na kuvuja damu mara nyingi, inuka tena uendelee na mapambano, hadi ufikie malengo yako.
  96. Jione wewe ni mtu mwenye nguvu, na una nguvu ya kustahimili magumu na changamoto zitakazokuja kwenye maisha yako, jikubali kuwa unaweza kuvuka kila changamoto itakayotokea kwenye maisha yako.
  97. Kamwe, kamwe usitumie nguvu na muda wako wa thamani kubwa kufanya mambo yasiyo muhimu, fanya mambo muhimu na ya maana sana kwenye maisha yako na kwenye jamii yako.
  98. Wewe ni kiongozi wa maisha yako, na kiongozi mzuri lazima awe na nidhamu kubwa na kali kwenye maisha yake, kupanga, kujiandaa, na kuwa na malengo yanayofikiwa.
  99. Usisema kitu chochote kuhusu mtu fulani ambacho haupo tayari kukisema mbele yake, maana yake usimsema mtu mwinge vibaya.
  100. Dhamiria kufanya vizuri kwenye siku za maisha yako zilizobakia. Nguvu zako na siku zako zilizobakia hapa duniani zitumie kuboresha maisha yako yaliyosalia. Hata kama umebakiza siku chache za kuishi hapa duniani. Kuwa mtu bora.

Asante kwa kusoma uchambuzi wa kitabu hiki, hiki ni kitabu kizuri sana, nashauri kila mtu akisome, ni kitabu kifupi na chepesi sana kukisoma. Usiache kumshirikisha mtu mwingine uchambuzi wa kitabu hiki. MANENO KIDOGO, KAZI ZAIDI, MATOKEO ZAIDI.

@Hillary Mrosso_30th April, 2023


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X