Deprecated: Constant FILTER_SANITIZE_STRING is deprecated in /home/songambele/public_html/wp-content/plugins/blogger-to-wordpress-redirection old/b2w-redirection.php on line 91
Sababu mbili Kwa Nini kila anayetaka kuwekeza anapaswa kuwa na biashara pia - SONGA MBELE

Sababu mbili Kwa Nini kila anayetaka kuwekeza anapaswa kuwa na biashara pia


Rafiki yangu mpendwa salaam, sina shaka unaendelea vizuri. KWENYE makala ya Leo ningependa kuongea na Wewe juu ya sababu mbili kwa nini haswa unapaswa kuwa na biashara kabla ya kuwekeza.

Kuna watu AMBAO Huwa wanapenda kuwekeza ila huwa hawataki kujifunza Kuhusu biashara wala kujua chochote biashara. Ukweli ni kwamba uwekezaji na biashara ni vitu ambavyo vinaendana, hivyo ni muhimu sana kama mwekezaji ukawa na biashara na ukajua namna biashara zinavyoendeshwa.

Hii ni kutokana na ukweli kuwa unapowekeza unakuwa kwenye biashara. Ukiwekeza kwenye hisa, hatifungani au VIPANDE Bado unakuwa unawekeza kwenye biashara. Hivyo, wewe kuwa na biashara yako ni jambo la muhimu sana maana kwanza utakuwa unajua namna unavyoendesha biashara yako lakini pia utaweza kumfuatilia namna wanavyoedesha biashara unayowekeza.

Sababu ya pili Kwanini unapaswa kuwa na biashara yako kabla ya kuwekeza ni kwa sababu NJIA Bora ya kuwekeza ni kuruhusu biashara yako ikusaidie kuwekeza.

Kuna aina fulani za uwekezaji mkubwa zinaweza kuwa ngumu kwako kufanya hasa pale unapokuwa na kipato Cha kawaida. Ila ukiwa na biashara yako, ni uhakika kuwa biashara yako inaweza kukusaidia wewe kufanya uwekezaji ambao pengine usingeweza kuufanya binafsi.

Hii ni Kwa sababu ukiwa na biashara unaweza kuweka juhudi kwenye biashara na KUONGEZA mapato na hivyo kuweza kufanya uwekezaji wowote unaotaka. Ila Kwa upande mwingine ukitegemea mshahara pekee inakuwa vigumu mshahara wako kuongezeka na kukuwezesha kufanya uwekezaji mkubwa unaotaka.

Kumbe Kwa sababu hiyo unahitaji kuwa na biashara ili biashara ikusaidie kufanya uwekezaji wowote unaotaka hata kama ni mkubwa.

Ikumbukwe kuwa, kama umeshaanza kuwekeza na Hauna biashara usije ukaacha kuwekeza ili uanzishe biashara kwanza. Endelea kuwekeza huku ukianza kujenga biashara.

Biashara haipaswi kukuzuia wewe kufanya uwekezaji. Na uwekezaji haupaswi kuzuia wewe kuanzisha biashara. Kuwa na hivi vitu viwili Kwa pamoja.

Au kwa kuwasiliana nami Kwa Namba ya simu 0684408755.

Pata hiki kitabu kwa 20,000 hardcopy na 10,000 softcopy


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X