Hii ndiyo Siri ya wewe kutengenezea utajiri mkubwa kwenye maisha.


Na siri hii ni kwamba kama unataka kuwa tajiri basi fanya kinyume na watu wengine wanavyofanya.

Mara nyingi watu wengi huwa wanafuata mkumbo kwenye maamuzi yao. Kwa hiyo, maamuzi yao yanakuwa siyo sahihi. Mtu anafanya kitu Kwa sababu na jirani yake anafanya.

Mtu anajiunga na VICOBA Kwa sababu jirani na rafiki zake wote wamejiunga na VICOBA.

Hata hivyo, matajiri siyo watu wa kufuata mkumbo. Wana msimamo kwenye maamuzi yao na mara nyingi maamuzi yao yanakuwa ni ya tofauti na watu wengine.

Mfano, utakuta watu wa kawaida wanasema kwamba uwekezaji ni hatari na hivyo hawawekezi. Matajiri wanajua kuwa uwekezaji ni hatari ila wanatafuta namna Bora ya kuwekeza huku wakiondoa au kupunguza hatari.

Watu wa kawaida wakiwekeza wanawekeza Kwa mkumbo, labda mfano hisa zinapokuwa zinapanda bei Kwa Kisha wanakuja kuuza Kwa hasara. Matajiri wanawekeza muda kujifunza na hivyo wanapochukua maamuzi ya Kununua hawanunui tu Kwa mihemko inayowaongoza watu wa kawaida Bali Kwa sababu wamefanya utafiti wao wa kina na wamejiridhisha kuwa uwekezaji fulani uko sawa.

Kwenye maisha yako hata kama huna mpango wa kuwa tajiri, jitahidi kuwekeza kama tajiri. Fanya kila kitu kama matajiri wanavyofanya. Utanishukuru sana Kwa hili rafiki yangu.

Kwa kusema hayo basi naomba nikusisitize Tena Kwa mara nyingine kuwa Siri ya wewe kumtengenezea utajiri mkubwa kwenye maisha yako ni kufanya KAZI na shughuli zako, kinyuma kabisa na watu wengine wanavyofanya.

Kila la kheri


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X