Sehemu Wanapokosea Wajasiriamali


Watu wengi wamekuwa wakifahamu kuwa ujasiriamali ndiyo njia ya uhakika ya kutoboa na kufanya makubwa. Hata hivyo, wengi wamekuwa wanakosea kwa namna wanavyofanya ujasirimali na biashara zao kiasi kwamba, kutoboa kwao imekuwa ni ngumu sana.

Kinachowakwamisha watu wengi ni kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja. Unakuta mtu ameanzisha biashara, wakati huohuo ana kitu kingine anachofanya sehemu nyingine. wakati huoho anapoteza muda mwingi sana kwenye mitandao. Biashara yake ikiwa bado haijatengamaa anasikia kwamba kuna fursa ya kuwekeza pesa zake sehemu akapata mara mbili ndani ya muda mfupi, anakimblia kuwekeza huko.
Maabo yake yakiwa bado hayajakaa sawa anakimbilia kucheza vikoba ili siku moja aje apate mkopo.

Na hapa ndipo wanapokosea wajasirimali wengi. Yaani, wanafanya vitu vingi sana, kwa wakati mmoja. ukifanya vitu vingi kwa wakati mmoja rafiki yangu, ni wazi kuwa huwezi kuona matokeo unayotegemea. Maana utakuwa unatawanya nguvu zako badala ya kuziweka sehemu moja. Nguvu zako ukiziweka sehemu moja, utapata matokeo makubwa kuliko ukitawanya nguvu zako kwenye maeneo mengi.

Ni kama mwanga wa jua. Huu mwanga huwa una nguvu kubwa sana, ila huwa umetawanyika. ila ukikusanywa sehemu moja, huwa unawasha moto. sasa na wewe kama unataka kuwasha moto, kama unataka biashara yako iende kwenye ngazi za kimataifa, basi washa moto na weka nguvu zako sehemu moja. Sehemu ambapo utaweza kupata matokeo makubwa.

Nakuhakikishia kuwa hiki ni kitu ambacho watu wengi hawapo tayari kukifanya, ukiweza kukifanya, kitakupa matokeo makubwa sana.
Kila la kheri.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X