Mabilioni yayeyuka upatu mpya


Hiki kichwa wala hata siyo mimi niliyekitunga, kilikuwa ni kichwa kwenye gazeti la mwananchi juzi. Ni moja ya habari ambayo imetikisa kwenye vyombo vya habari, na kwenye mitandao ya kijamii. Swali ambalo unaweza kuwa unajiuliza ni kuwa inawezekanaje watu wanalizwa kila mara kwa kutapeliwa na bado wanazidi kutapeliwa?

Utapeli hautaisha hapa duniani.

Moja kati ya matapeli wakubwa sana ambao waliwahi kuishi hapa duniani, ni bwana mmoja ambaye anajulikana kwa jina la Ponzi. Huyu jamaa alifanya utapeli wake miaka ya 1920

Huu ulikuwa ni mradi ambao ulikusanya pesa nyingi za watu na baadaye jamaa akawa ameyeyuka na pesa za watu.

Mpaka leo hii michezo ya upatu mingi imekuwa inajulikana kwa jina la PONZI SCHEME. Ikichukua jina la tapeli mkubwa sana kuwahi kutokea hapa duniani. Kabla ya huyu jamaa utapeli ulikuwa ukifanyika na hata baada ya utapeli huo mkubwa alioufanya, bado utapeli umekuwa unafanyika. Kwani mwaka 2008,  tapeli mwingine mkubwa  kwa jina la Bernoff alikuwa ametapeli watu zaidi ya dola bilioni 64.

Huu nao ulikuwa ni utapeli mkubwa sana.

Naweza kuonekana naongelea utapeli unaoendelea kwenye nchi za watu wengine, halafu ikaonekana kama vile hapa kwetu hakuna uutapeli unaonendelea.  Hapa kwetu pia utapeli umekuwa unaendelea kwa wingi sana.

Nadhani, mara ka mara umekuwa unasikia watu wanavyotapeliwa.

Juzijuzi tu hapa kulikuwa na watu wanaitwa Kaylinda, hawa waliyeyuka na pesa nyingi za watu pia. Sasa juzi tena gazeti la mwananchi lililipoti taarifa ya mabilioni ya watu kulizwa kwa mabilioni yao kupelekwa.

Unachopaswa kufahamu mpaka hapa ni kwamba utapeli upo na utaendelea kuwepo kwa miaka yote ambayo binadamu atakuwa hapa duniani.

Hii hapa ni sababu kwa nini utapeli utaendelea kuwepo hapa duniani.

Kwanza unajua kwa nini watu huwa wanatapeliwa?

Watu huwa wanatapeliwa kwa sababu wanapenda kupata faida kubwa ndani ya muda mfupi, au huwa wanataka kupata fedha nyingi ndani ya muda mfupi na bila ya kufanya kazi. Hiki ndicho chanzo cha watu kutapeliwa. Na ndio maana watu wataendelea kutapeliwa.

Watu wataendelea kutapeliwa kwa sababu wanapenda hivyo vitu viwili nilivyoanisha hapo juu. Faida kubwa kutokana na uwekezaji wao, tena ndani ya muda mfupi pamoja na pesa nyingi tena bila ya kutoa jasho.

Sasa kwa kuwa matapeli wanayajua hayo mambo mawili, wakija kukutapeli wanaanzia hapo.

Wanakuahidi kukupa fedha nyingi ndani ya muda  mfupi, tena bila ya kufanya kazi au kutoa jasho.

Kwa kuwa watu wanataka kuwekeza na kupata mrejesho mkubwa, hapo ndipo wanaanza kuchutapeliwa.

Viashiria kwamba hapa uwekezaji fulani ni upatu

1. Unaambiwa kwamba ufanye uwekezaji na hakuna hatari yoyote ile kwenye uwekezaji huo.

Kila uwekezaji una hatari zake, ukiona mtu anaanza kukwambia uwekezaji fulani hauna hatari yoyote, basi ujue kwamba hicho ni kiashiria cha kuwepo cha mchezo wa upatu.

2. wanatoa mrejesho mkubwa kwa watu wawekezaji wa kwanza ili kuwavutia watu kuwekeza zaidi. unachoopaswa kujua wewe kama mwekezaji ni kwamba hakuna uwekezaji ambao huwa unatoa mrejesho mkubwa tu mara zote. kuna wakati mrejesho unaweza kuwa ni mkubwa na muda mwingine ukapungua. Ila ukiona unaambiwa ukiwekeza utapata mrejesho mkubwa tu, au ukiona watu wanapewa mrejesho mkubwa tu kila mara. Basi hapo ujue kuwa kiashiria cha utapeli.

3. shughuli zinazoleta kipato hazijulikani. Yaani, wewe unaambiwa weka laki moja leo na kesho tutakupa laki mbili, lakini ukiwauliza ni shughuli gani ambazo zinawapa hicho kipato kwa haraka hivyo, wanakuwa hawako tayari kuziweka wazi. Ila wewe unaambiwa, wewe wekeza tu uone….

Ukiona hivyo, ukiwekeza tu ujue utaona kwelikweli…

Sasa ufanyeje ili kuepukana na kutapeliwa?

Rafiki yangu, hivi nilikwambia kwamba watu wamekuwa wanatapeliwa na wataendelea kutapeliwa kwa siku zote ambazo binadamu anaendelea kuishi. Ndio, sijakosea kwenye hili, na kuthibitisha hili wewe mwenyewe unaweza kujaribu kuorodhesha utapeli ambao umewahi kusikia au kuona kwa macho yako tangu umekuwa na akili timamu. Tuachane na tangu umekuwa na akili timamu, tuchukue tu hata miaka mitano iliyopita. ni mara ngapi umesikia watu wametapeliwa. Ni mara nyingi sana. na hao ni wale ambao walitangazwa kwenye vyombo vya habari, kuna wale amba habari zao hazisikiki kwenye vyombo vya habari, na hao ni wengi pia.

Ssa ufanyeje ili kuepukana na kutapeliwa?

Yafuatayo ni mabo ya kuzingatia.

Kwanza usikurupuke kuwekeza. Kisa unaona watu wengi wanakimbia kuwekeza na wewe unakimbia tu kuwekeza.

Pili, wekeza kwenye uwekezaji unaoeleweka. Kama kitu hukielewi, usiweke hela yako hata kama wanakuahidi kukupa hela mara elfu moja ya ile uliyoweka. Warren Buffet ni mmoja wa matajiri wakubwa sana hapa duniani, na anafanya uwekezaji. Lakini kitu kikubwa sana kuhusu gwiji wa uwekezaji ni kwamba huwa hawekezi kwenye vitu ambavyo havielewi. Yeye huwa anawekeza tu kule anapokuelewa.Hiki kitu kimefanya watu wengi wamseme sana, ila yeye kwa upande wake ameendelea kusimamia msimamo wake huo bila kuteteleka. Mfano, moja ya  msimamo wake ni msimamo wake wa kutowekeza kwenye makampuni ya mitandao ya intaneti. Ni aina ya biashara ambayo alikuwa haielewi, na hivyo hajawekeza huko. Ndio kuna watu wamewekeza na wanapata faida nzuri, ila yeye haelewi, hivyo, hata haweki nguvu kwenye hayo makampuni.

WEWE pia kwa upande wako unapaswa kuwa hivyo, usiwekeze kwenye kitu ambacho hukijui.

Tatu, Wekeza kwenye uwekezaji uliorasimishwa na serikali kama uwekezaji kwenye HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE unmerasimishwa na unaendeshwa chini ya soko la HISA LA DAR ES SALAAM. Kuelewa zaidi kuhusu hisa, hatifungani na vipande basi soma kitabu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. Hiki ni kitabu ambacho kimewasaidia watu wengi, na wewe kitakusaidia pia. Kipate hiki kitabu kwa manufaa yako.

Pata hiki kitabu kwa 20,000 hardcopy na 10,000 softcopy

Sambamba na hicho kitabu, kuna kitabu kingine muhimu sana ambacho unapaswa kuchukua. na kitabu hiki siyo kingine bali ni hiki hapa

Kipate kitabu hiki kwa manufaa yako

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.


One response to “Mabilioni yayeyuka upatu mpya”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X