Leo siku ya kitabu duniani…..


Frederick Douglass alizaliwa akiwa mtumwa kwenye mashamba ya huko Maryland nchini Marekani. Akiwa na umri wa mwaka 1 alitenganishwa na mama yake, ambapo hiki kinasemekana kilikuwa ni kitu cha kawaida sana kufanyika miongoni mwa watumwa.

Hivyo, Frederick Douglass alikuja kukutana mama yake mara nne zaidi kwenye maisha yake kabla mama yake hajaaga Dunia.

Akiwa kama mtumwa na miaka 8 aliepelekwa Kwa mmiliki wake mpya. Akiwa huko mke wa yule mmiliki wake akawa ameanza kumfundisha kusoma na kuandika. Hata hivyo, kabla masomo ya kusoma na kuandika hayajachanganya, yalisitishwa baada ya mmiliki wake kugundua kuwa mke wake alikuwa anamfundisha Frederick Douglass kusoma na kuandika.

Yule bwana alisema kwamba kisheria watumwa hawaruhusiwi kufundishwa Wala kuandika. Na isitoshe mtumwa akifundishwa kusoma atakuwa hashikiki. Kitu hiki kiliachavalama kubwa kwenye kichwa Cha Frederick Douglass. Kuanzia hapo akaanza kutafuta kila namna ya kujifunza kusoma maaana alishaona NJIA pekee ya yeye kutoboa kimaisha ilikuwa ni kujua kusoma na kuandika.

Ilimchukua Frederick Douglass miaka saba mpaka kujua kusoma na kuandika. Akawa ameanza kusoma vitabu, hasa vile vilivyokuwa vinahamasiha kukomesha utumwa

Baadaye kwenye maisha yake Frederick Douglass alikuja kuwa mtu mkubwa sana. Mshauri mzuri Kwa Marais wawili wa Marekani. Abraham Lincoln na rais Andrew Johnson

Ebu pata picha mtu ambaye alikuwa mtumwa, hakusoma shule Wala chuo chochote alivyoweza kufikia HATUA ya kufanya makubwa kiasi hicho.

Nimeamua nianze na stori hii ya Frederick Douglass Leo hasa ukilinganiaha kuwa Leo ni siku ya kitabu duniani.

Tunaishi kwenye zama zenye vitu vingi sana, ila kitu ambacho Bado hakijapoteza nguvu yake ni kusoma na kujifunza.

Kusoma siyo tu kwamba kilikuwa muhimu enzi za akina Frederick Douglass, Bali mpaka Leo hii.
Kwenye kitabu Cha Future shock, mwandishi Alvin Toffler

Anasema mjinga wa Karne ya 21 siyo yule ambaye hajui kusoma na kuandika. Bali mjinga wa Karne ya 21 ni yule anayejua kusoma na kuandika ila hasomi wala kuandika….

Sasa basi Leo ikiwa ni siku ya kitabu duniani. Nipende kukusisitza sana juu ya umuhimu wa kusoma vitabu, kama ambavyo nimewahi kuandika na kusisitiza juu ya umuhimu huu kwenye kitabu changu Cha MAAJABU YA KUSOMA VITABU

Hiki ni kitabu hiki Huwa nakitoa Bure kama zawadi Kwa watu wangu wa nguvu kama wewe. Kama hujawahi kusoma kitabu hiki, Sasa huu ndiyo muda wako wa kukisoma.
Kipate hapa.
Au unaweza Kusikiliza kilichosomwa Kwa sauti hapa.πŸ‘‡πŸΏπŸ‘‡πŸΏ

Aidha Kwa upande mwingine siku ya Kimataifa ya kusoma vitabu au International Book Day inaadhimishwa kila mwaka tarehe 23 Aprili. Lengo la sikukuu hii ni kusherehekea vitabu na kusisitiza umuhimu wa usomaji, kukuza utamaduni wa kusoma na kuboresha uelewa wa kijamii kwa ujumla.

Siku hii ilitangazwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kwa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) mnamo mwaka 1995, na tarehe ya maadhimisho 23 Aprili ikichaguliwa kuwa heshima ya waandishi wawili maarufu William Shakespeare na Miguel de Cervantes, ambao walifariki siku hiyo hiyo mwaka 1616.

Siku ya Kimataifa ya Vitabu inaadhimishwa kwa njia mbalimbali duniani kote, ikiwa ni pamoja na matamasha ya vitabu, hafla za kusoma, mihadhara, na shughuli za kupata vitabu vya bure au vitabu kupunguzwa bei. Siku hii pia hutumika kutoa hamasa kwa watu wote, hususan vijana, kuanza kusoma vitabu na kuendeleza utamaduni wa kusoma kama sehemu muhimu ya maisha yao ya kila siku.

Rafiki yangu nataka uitumie vizuri siku ya Leo.
Na Kwa kuwa ni siku ya kusoma vitabu duniani. Leo utapata ebooks zangu zote kwa sh 7,000/- tu badala ya 10,000/-

Audiobooks utazipata Kwa 5,000/- badala ya 10,000/-

Changamka Sasa upate ofa hii. Hii ni ofa ya Leo. Na ni ofa ya Leo tu. Mwisho ni saa nne usiku.

Cha kufanya, fanya malipo ya kitabu chochote unachopenda kwa Namba ya simu 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA. Kisha niambie ni kitabu kipi umelipia nikutumie.

Enjoy siku ya kitabu duniani

Cheers!

Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X