Kama kila mtu angekuwa ni…


Hivi kaa chini ufikirie kama kila mtu angekuwa ni mzembe kama wewe.

Kama kila mtu angekuwa na visingizio kama wewe

Kama kila mtu angekuwa ni mwoga kama wewe

Kama kila mtu angekuwa ni mlalamikaji kama wewe.

Kama kila mtu angeona aibu kuitumia akili yake?

Kama kila mtu angesema ni acha nile maisha leo kesho itajijua yenyewe

Hivi unadhani nani angethubutu kufanya vitu vya tofauti. Ni nani angethubutu kutengeneza nguo unazovaa? Ni nani angethubutu kuanzisha biashara ambazo zinakusaidia wewe kuweza kufanya kazi zako.

Bila shaka asingekuwepo. Kila unapoona kitu kizuri basi ujue kwamba kuna watu waeamua kuachana na uoga, ulalamikaji, uzembe, kutupia watu lawama na wamekuwa tayari kubeba majukumu ya maisha yao.

Hivyo basi, kitu ambacho unapaswa kufanya kuanzia leo basi ni kuchukua hatua, kuacha kulalamika, uzembe, kutupia watu  lawama na uwe tayari kubeba majukumu yanayokuhusu.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X