Fanya kazi na kitu unachotaka kufanya kwa ubora


Katika kazi au kitu chochote kile utakachoamua kufanya. Weka moyo, akili na kila kitu kwenye hicho kitu. Yaano, zama kabisa kwenye kile kitu kiasi kwamba hakuna kitu ambacho kinapaswa kukutoa wewe kwenye reli ya kukamilisha hicho kitu.

Yaani, kwenye hili nataka upate mfano wa simba. Si unamjua Simba si mnyama mkubwa kuliko wote mbugani. Simba si mnyama mwenye akili sana kuliko wote. SIMBA si mnayama mwenye nguvu sana kuliko wote mbungani.

Lakini cha kushangaza ni kwamba simba ara zote anaitwa Mfalme wa nyika. Unajua kwa nini anaitwa mfalme wa Nyika.

Sababu ni moja tu

Ni kwa sababu huwa anathubutu, na huwa akiamua kufanyia kazi jambo lake huwa harudi nyuma. Hiki ni kitu ambacho kinamtofautisha na wanyama wengine.

Mpaka kuna usemi unaosema kwamba ni bora kuwa na kundi la kondoo ambalo linaongozwa na simba kuliko kuwa na kundi la simba linaoongozwa na kondoo.

Kwa nini? Kwa sababu simba akiamua, ameamua. Harudi, na wala harembi mwandiko. Sasa katika mazingira kama hayo, simba akiwa na kondoo ni wazi kuwa kondoo nao watafuata mkondo wake.

Lakini kondoo akiwa anaongoza kundi hilo, basi ni wazi kuwa akiongopa na akageuza mbio, basi ni wazi kuwa  hata wale simba watakimbia

Kwenye maisha yako rafiki yangu. Kuwa simba.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X