usipofanyia kazi ndoto zako kuna mtu atakuajiri ili ufanyie kazi ndoto zake


Rafiki yangu, watoto wadogo huwa wanaongoza kwa kuwa na ndoto kubwa sana. Ukiongea na mtoto yeyote yule mdogo atakwambia ndoto zake kubwa, tena kwa kujiamini.

Ongea na MTU mzima sasa. UNAWEZA kutamani kuzaba baadhi ya watu vibao. Watu walewale ambao walikuwa na ndoto kubwa utotoni, kwa sasa hawana tena hizo ndoto kubwa.

Ndoto ileile waliyokuwa nayo utotoni ukiwakumbushia wataanza kukupa sababu kibao kuonesha kwa Nini HAIWEZEKANI kufanyika.
Watakwambia uchumi mgumu.
Watakwambia vyuma vimekaza.
Watakulerea sababu nyingine kibao.

Rafiki yangu, wewe ni mmoja wa hao watu?

Ndoto Yako. Naam ndoto Yako Ni kitu muhimu ambacho haupaswi kupoteza. Na ukiona umepoteza ndoto zako, ujue tu lazima Kuna MTU anaenda kukuajiri ili ufanyie kazi ndoto zake.

Unajua kwa nini?

Kwa sababu dunia haipendi kukaa na utupu. Popote pale kunapokuwa na utupu dunia inatafuta sababu ya kuhakikisha pamejaa.

Kama sehemu Haina mazao Basi itakuwa na magugu.
Kama sehemu ubongo hauna mawazo chanya, basi utakuwa na mawazo hasi.

Kumbe na wewe usipofanyia kazi ndoto zako, lazima tu kutakuwa na mtu ambaye atakuajiri ili ufanyie kazi ndoto zake. Kama MTU hatakuajiri ufanyie kazi ndoto zake. Basi visingizio vitakumeza, kwenye kufanyia kazi ndoto zake.

Sasa rafiki yangu, kuanzia leo amua kitu kimoja tu. Kufanyia kazi ndoto kwa kufa na kupona. Pambania ndoto zako rafiki yangu hata kwa kuanzia chini Sasa hivi.

Kila la kheri

Sasa kitu kikubwa cha kufanya leo ni wewe kuhakikisha kwamba unaanza kufanyia kazi.


One response to “usipofanyia kazi ndoto zako kuna mtu atakuajiri ili ufanyie kazi ndoto zake”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X