Jinsi Ya Kujenga Mafanikio Makubwa Hata Kama Hauna Kitu


Hapo zamani za kale, ili kujenga utajiri ulipaswa kuwa na ardhi kubwa, ng’ombe na vitu vingine vinavyoendana na hivyo. Ulipokuwa na vitu vya aina hiyo, hapo sasa ndipo watu walikuwa wanasema kwamba mtu fulani ni tajiri. Ila leo hii mambo yamebadilika.

Baadaye ilikuwa inaaminika kwamba ili kujenga utajiri unapaswa kuwa walau na konekisheni na ndugu au mtu ambaye ni tajiri au ambaye anafanya kazi kwenye taasisi kubwa. ila leo hii mambo hayo yote yamebadilika, huhitaji kuwa na konekisheni wala ndugu yako ambaye anafanya kazi serikalini, huhitaji kuwa fisadi, huhitaji kuwa mashamba mengi wala ng’ombe elfu. Unahitaji kutumia kile ulinacho. Na kwa sababu hiyo, siku ya leo ninaenda kuandika makala ya kina inayoeleza namna ambavyo unaweza kufanikiwa kwa viwango vikubwa hata kama hauna kitu.

Hatua ya kwanza ya kujenga mafanikio makubwa hata kama hauna kitu ni

1. KUJUA KITU UNACHOPENDA NA KUANZISHA BIASHARA KWENYE KILE UNACHOPENDA

Rafiki yangu, najua kuna vitu kadha wa kadha unapenda hivi kwako vinapaswa kuwa sehemu ya kuanzia. Haitoshi tu wewe kila siku kwenye kuangalia mechi kila siku, huku ukishangilia kwamba Mayele kafunga au hajafunga. Baala yake unapaswa kuangalia fursa iliyojicicha kwenye hicho kitu mbacho unapenda na namna ambavyo unaweza kuitumia hiyo fursa kufanya makubwa.

Ukishajua kitu ambacho unapenda, basi acha kufanya mambo mengine yoyote yale, badala yake wekeza nguvu na muda wako kwenye hicho kitu unapenda.

Jenga biashara kwenye hicho kitu. Jenga hata biashara ya kuanzia chini.

2. ANGALIA RASILIMALI ZILIZO KWENYE MAZINGIRA YAKO UNAZOWEZA KUANZA KUTUMIA SIKU YA LEO

Kuna rasilimali ambazo naamini unazo ambazo unaweza kuanza kutumia.unaweza ukawa unafikiria kufanya makubwa sana ambayo pengine hayajawahi kufanyika kwenye hii dunia, lakini unachopaswa kufahamu ni kwamba, hayo makubwa unaweza kuanza nayo kidogo kidogo na kwenda nayo hatua kwa hatua mpaka ukaweza kuyafanya kuwa makubwa zaidi.

Kuna rasilimali nyingi zimekuzunguka ambazo unahitaji kuhakikisha kwamba umezitumia. Nguvu zako, muda wako, mazingira  yaliyokuzunguka na mengine mengi. Tumia hizi rasilimali kuhakikisha kwamba unafanya makubwa. Naam, makubwa sana.

3. TOA THAMANI KUBWA TENA BURE

Najua u ataka kulipwa tena kwa viwango vya juu. IlA NJIA NZURI YA wewe kuweza kulipwa ni kuanza na kile ulichonacho, ukiweza kufanyia kazi vizuri kile ulichonacho, utaweza kufanya makubwa sana. tumia kile ulichonacho kwanza.

4. JIPE MUDA

Kila kitu hakitaweza kufanyika ndani ya siku moja. unahitaji kujipa muda ili kuweza kujenga mafanikio ambayo unataka. Mafanikio makubwa hayajengwi ndani ya siku moja au wiki moja. badala yake ni kwamba yanachukua muda.

5. JIJUE MWENYEWE

Jijue mwenyewe ni vitu gani unaweza zaidi kuliko vingine. badala ya kupambana kufanya kila kitu, wekeza nguvu na muda wako kwenye vitu vichache ambavyo unaweza kuliko kufanya kila kitu  bila mpangilio.

6. PAMBANA KWA BIDII

Rafiki yangu, malengo yako na ndoto zako unapaswa kuzipambania kwelikweli bila ya kurudi nyuma. Na hili hakikisha kwamba unalifanyia kazi bila ya kurudi nyuma. Kiufupi. Hakikisha kwamba kila unapoamka mpaka unapoenda kulala, unakuwa umepambana na kupambana zaidi. ukiona imepita siku bila ya kufanya kitu chochote kwenye ndoto yako. Basi ujue hiyo siku umeipoteza.

7. TUNZA MUDA WAKO VIZURI

Muda ndiyo rasilimali pekee ambayo inaweza unayo bure na ambayo ukiipoteza unakuwa umeipoteza. Kwa hiyo basi, mara zote pambana kuhakikisha kwamba unautumia muda wako kwa uzuri na kwa weredi mkubwa kuhakikisha kwamba muda wako unakuwa wenye manufaa.

Watu wanaofanikiwa sana na wale ambao hawafanikiwi sana wana muda uleule. Tofauti kati ya wale wanaofanikiwa sana na wale ambao wanakuwa na mafanikio ya kawaida ipo kwenye matumizi ya muda. Hivyo basi, ili uweze kufanya makubwa unapaswa kuhakikisha kwamba unautumia vizuri muda wako. Anza na dakika yako moja ya sasa, kisha pangilia saa lako moja la baadaye na kisha siku yako nzima. Muda wako ni rasilimali muhimu sana ambayo unapaswa kuitumia vizuri sana.

8. PENDA MCHAKATO

Mchakato ni muhimu zaidi kuliko lengo. Watu wengi huwa wanaweka malengo mwanzoni mwa mwaka, ila malengo ni kitu kimoja. Kufanyia kazi yale malenngo ndio jambo lenyewe haswa. Na hili ndilo ambalo ningependa ulifahamu siku ya leo

9.ACHA KUJALI SANA KILE AMBACHO WENGINE WANAFIKIRIA

Najua kuna mengi sana ambayo watu wengine wanafikiria. Acha kujali sana mambo ambayo watu wengine wanafikiria. Badala yake wekeza muda wako na nguvu zako kwenye kile unachofanya tu.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.


2 responses to “Jinsi Ya Kujenga Mafanikio Makubwa Hata Kama Hauna Kitu”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X