TABIA ZA WATU WANAOLIPWA SANA


Rafiki yangu, kila sekta huwa ina watu wake ambao huwa wanafanya jambo fulani. Na ili uweze kuwa kwenye kundi fulani, lazima uwe na tabia ambazo zinaenda na ambao wako kwenye sekta husika. Kwa mfano ili luweze kuwa kwenye kundi la watu ambao wanalipwa sana, lazima uwe tabia za watu ambao wanalipwa sana, hivyo vhiyo kama unataka kuwa kwenye kundi la watu wanasiasa, lazima uwe na tabia za wanasiasa,  ukitaka kuwa kwenye kundi la mafisadi, sharti uwe na tabaia za mafisadi, hivyo hivyo ukitaka kuwa kwenye kundi la ombaomba, sharti uwe kwenye tabia za ombaomba.

Ili uwe mwanamuziki ambaye analipwa sana, sharti uwe na tabia za wanamuziki ambao wanalipwa sana.

Kwenye hiki kitabu,  unaenda kujifunza tabia za watu wanaolipwa sana. ukizifuata hizi tabia na kuziishi vizuri, ni wazi kuwa na wewe unaenda kulipwa kwa kiwango kikubwa kulikoambavyo umekuwa unalipwa sasa hivi. je, upo tayari kuhakikisha kwamba unaanza kulipwa zaidi ya ambavyo unalipwa sasa hivi? karibu sana uweze kujipatia nakala ya kitabu hiki cha kipekee sana.

TABIA YA KUWEKA MALENGO MAKUBWA NA KUYAFANYIA KAZI HATUA KWA HATUA

Nilichokuja kugundua kwenye maisha ni kwamba karibia kila mtu ana malengo makubwa.Hii haijalishi mtu huyo anafanyia kazi maengo hayo, au hafanyii kazi malengo hayo. Utakuta kwamba huyo mtu ana malengo makubwa na anayafanyia kazi hayo malengo yake. Sasa changamoto ya malengo haya makubwa inakuja kwenye kuyafanyia kazi. kuna wale ambao wanakuwa tayari kuyafanyia kazi  haya malengo makubwa, wakati wengine wakiwa hawako tayari kuyafanyia kazi malengo hayo makubwa, ila wakiwa wanasubiri itokee siku moja ambapo wataweza kuyafanyia kazi malengo yao makubwa bila ya shida yoyote

Rafiki yangu kama unataka kuyafanyia kazi malengo yako na kuyafanikisha bila ya shida yoyote ile, hakikisha kwamba hausubiri mpaka uwe umeweza kufikia ngazi fulani ya kiamaisha ili uweze kufanikisha malengo yako au kuyafikia malengo yako, badala unapaswa kua tayari kuanza kuyfanyia kazi malengo yako hatua kwa hatua mpaka kuweza kuyafanikisha.

PILI NI TABIA YA KUJIFUNZA BILA UKOMO

Hii ni tabia nyingine ya watu wanaofanya makubwa, hawa watu wanajisukuma kwa vyovyote vile kuhakikisha kwamba wanakuwa ni watu wa kujifunza bila kukoma. Yaani, kila siku wanahakikisha kwamba wanajifunza kitu fulani na wanakifanyia kazi. Hiki kitu kinapaswa kuwa hivyo kwa upande wako pia.

Rafiki yangu, kuanzia leo hii anza kujenga tabia ya kujifunza kila siku bila ya kuwa na ukomo. Yaani, kwako kujifunz linapaswa kuwa ni jambo endelevu ambalo unalifanya kila siku bila ya kuacha. Na hata leo hii unapaswa kuhakikisha kwamba umechukua kitabu  na umekisoma. Rafiki yangu, anza kufanyia kazi hili jambo kuanzia siku hii ya leo.

TABIA YA KWENDA HATUA YA ZIADA KWENYE CHOCHOTE KILE AMBACHO WANAFANYA

Watu wanaolipa sana huwa wanaenda hatua ya ziada kwenye kitu chochote kile ambacho wanafanya. Yaani, huwa hawafanyi kazi au jambo lao lolote lile kwa ukawaida, badala yake huwa wanahakikisha kwamba wanajituma kwenye kazi na kwenye kitu chochote kile ambacho wanafanya ili mwisho wa siku waweze kupata matokeo makubwa.

Kwenda hatua ya ziada kwenye kazi au chochte kile ambacho unafanya kunaweza kuonekana kama jambo la kawaida sana kwa kila mtu, ila kitu kikubwa sana ambacho ninataka nikuthibitishie wewe rafiki yangu kwamba kama, ukijenga utaratibu wa kwenda hatua ya ziada kaaribia kwenye kila kitu ambacho unafanya, mwisho wa siku utaweza kufanya makubwa sana. Naam, utaweza kufanya makubwa mno

TBIA YA KUPENDA KAZI

Watu wanalipwa sana ni watu ambao wanapenda sana kazi. Yaani, kwao hata iweje, maisha yao yamejengwa kwenye kazi. wanaweza kuanzia chini kabisa kwenye maisha, wakiwa hawana akiba, wala kiasi chochote au kitu chochote cha kuwafanya kuwa na maisha ya maana, ila kutokea hapo hicho kitu kikawafanya waendelee kujituma na kufanya kazi kwa juhudi mpaka mwisho wa siku wakaweza kufanya makubwa. Naam, wakaweza kufanya makubwa mno.

Na wewe kuanzia leo hii ningependa upende kazi. Kazi ndiye rafiki wa kweli ambaye unaweza kuambatana nayepopote pale utakapokuwa. Kazi ni rafiki ambaye hawezi kukuacha kamwe kwenye maisha yako. Rafiki yangu penda kazi.

Rafiki yangu, kuanzia leo hii, anza kujenga tabia za watu wamabo wanalipwa sana. Kwa kufanya hivi, utajikuta kwamba kipato chako kinaanza kuongezeka, penginE mara ya kwanza taratibu sana. ila kadiri ambavyo utaendelea kulifanyia kazi hili, ndivyo ambavyo mwisho wa siku utakuwa na uwezo wa kuingiza kipato kikubwa mno.

Kwa kuanzia rafiki yangu, nakushauri, uhakikishe umesoma kitabu changu cha JISNI YA KUONGEZA THAMANI YAKO.

Hiki kitabu kina mwongozo utakazokusaidia wewe kuanza kulipwa zaidi ya unavyolipwa sasa hivi.

Kupata kitabu hiki wasiliana nasi kwa 0684408755

Gharama ya kitabu ni 30,000/- ila kwa sasa utakipata kwa ofa ya 20,000. Piga 0684408755


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X