Njia ya uhakika ya kupata bahati maishani mwako


Rafiki yangu unajiuliza ni kwa namna gani unaweza kupata bahati maishani mwako. Siku ya leo nina njia moja ya ukweli na ya uhakika ya kukufanya wewe uweze kupata bahati maishani mwako. Na njia hii ni wewe kufanya kazi kwa bidii.

Kuna mtu mmoja aliwahi kusema kwamba kadiri ninavyokuwa nafanya kazi kwa bidii ndivyo ambavyo ninakuwa na bahari, hiki kitu kimenifanya siku ya leo nikukumbuke na wewe.

Ninajua kwamba ukiweza kufanya kazi kwa bidii utaweza kuwa na bahati kwenye eneo lolote la maisha yako. Hivyo basi rafiki yangu, kama unataka kuwa na bahati maishani mwako, fanya kitu kimoja. Fanya kazi kwa bidii.

Jitume zaidi kwenye kazi zako. Maana kadiri utakavyofanya kazi kwa bidii ndivyo ambavyo utazidi kuwa mwenye bahati zaidi.

Najua utasikia mambo memngi kuto kwa watu mbalimbali. wapo watakaosema kwamba, unapaswa kufanya kazi smar (work smart)t badala ya kufanya kazi kwa bidii. Ila ninachotaka kukwambia rafiki yangu ni kitu kimoja tu. Inalipa sana kufanya kazi kwa bidii.

Ni kweli utahitaji kufanya kazi smart, ila bado kufanya kazi kwa bidii ni jambo ambalo haliepukiki kwa upande wako.

Jinsi  nyuki ambavyo huwa wanatengeneza bahati yao

Nyuki ni wachapakazi sana. Sote tutakubaliana kuwa asali ni tamu sana na tunaipenda kwelikweli. Ila mpaka unaona huo utamu ambao nyuki wanakuwa wameutengeneza unapaswa kujua kwamba hao nyuki wanakuwa wamefanya kazi kwa bidii sana nyuma ya pazia. Hawalali na kusubiri siku moja ambapo asali itajitengeneza yenyewe, badala yake, kila siku, bila ya kujali ni mvua au jua, wanakuwa wanafanya kazi kwa bidi kuhakikisha kwamba wanatengeneza bahati yao.

Jinsi Mchwa wanavyotengeneza bahati yao

Mchwa ni wadudu wengine ambao huwa wanajiwekea akiba kubwa sana ya chakula. Akiba hii huwa wanaiandaa wakati wa kiangazi na huja kuitumia baadaye kwenye masika. Huu uchapakazi wa mchwa unapaswa kuuiga pia maana utakufanya uweze kutengeneza bahati kwenye maisha yako na hatimaye kuweza kuwa mtu bora kuwahi kutokea kwenye maisha yako

Rafiki yangu, nakupa mifano yote hii ili uone kwanza ujifunze kwa asili, maana asili haidanganyi. Asili haifeki, asili haifanyi vitu kwa ajili ya kuja kupost facebook wala instagram, asili inafanya vitu kwa sababu vinapaswa kufanyika.

Pili nimekuandakia haya yote ili luweze kuona kwamba inawezekana kutengeneza aina yoyote ile ya maisha unayotaka. Na inawezekana kwelikweli.

Na mwisho nimekuandikia hapa ili na wewe uweze kuchukua hatua mathubuti kwenye maisha yako. Badala ya kubweteka na kukaa bila ya kufanya kitu au jambo lolote.

Kila la kheri.

Makala nyingine Zinazoenda na hii

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

,

One response to “Njia ya uhakika ya kupata bahati maishani mwako”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X