KUWA IMARA


Tunaishi katika dunia ambayo haipendi vitu ambavyo siyo imara. Na hili jambo la KUWA imara halijaanza leo. Limekuwepo kwa siku nyingi sana.

Vitu ambavyo vimekuwa imara kwa miaka mingi ya nyuma, ndivyo ambavyo viliendelea kuishi, huku vile ambavyo siyo imara vikidhoofu na kufa.

Watu wanyonge, mimea minyonge, wanyama wanyonge havina nafasi kubwa ya kuishi Kama vile vitu ambavyo ni imara. Hivyo, na wewe unapaswa KUWA imara.

Najua hiki kitu kinaweza kuonekana cha ajabu sana hasa kwa upande wako ukizingatia kwamba umezoea kuambiwa KUWA wewe Ni MNYONGE. Na hivyo kuna watu wanakutetea wewe na unyonge wako.

Ninachotaka kukwambia ni kuwa, usikubali kuwa MNYONGE. Unyonge ni hali ya chini ambayo MTU yeyote hapaswi kuibeba.
Unapaswa KUBEBA ujasiri, uthubutu, na sifa nyingine za aina hii.

Unyonge haukai meza moja na ujasiri. Unyonge hauwezi kukaa meza moja na uthubutu. Unyonge hauwezi kukaa meza moja na utawala.
Ukiwa MNYONGE unanyongwa na haki yako hupewi. Huo ndio ukweli.

Kitabu: How to Win Friends and Influence People

Hivyo, nataka ujiondoe kwenye hali ya unyonge kuanzia Leo hii na uanze kuwa jasiri, uwe imara.

Kanuni ya Darwin
Darwin na wanasayansi wengine waliotangulia kabla yake kama akina Lamark na wengine ambao wamefuata baada Yao wamethibitisha kuwa viumbe ambavyo huwa ni vinyonge huwa vinapotea na kutoweka kwenye uso wa dunia, huku vile ambavyo ni imara viking’aa na kufanya makubwa zaidi.

Mfano wa kawaida ni kwenye wanyama. Ukiwa na mbuzi au kuku umewafuga. Halafu hao wanyama ukawawawekea chakula. Wanyama ambao ni imara watakuwa mstari wa mbele kula na hata watafukuza wale ambao siyo imara. Wale ambao siyo imara watafukuzwa na kukaa pembeni. Ni mpaka pale wanyama walio imara watakapokuwa wamemaliza kula ndio na wale wanyonge watakula. Kama chakula ni kidogo, Basi wanyama wanyonge wataishia kujiramba tu.

Hiki kitu hata sisi kwetu wanadamu ,hujawahi kuona kwenye sherehe kinaletwa chakula watu wanakigombania? Unajua ni watu wa aina gani ambao huwa wanaishia kula chakula cha aina hiyo? Ni wale ambao huwa wanakuwa imara. Wanyonge wanakaa pembeni.

Na hiki halitokei kwenye chakula tu, Bali hata kwenye tendo. Wanyama ambao siyo imara hawapati nafasi ya kufanya tendo na wanyama wengine. Kitu kinachofanya mbegu zao zisisambae Kutoka kizazi kimoja KWENDA kingine.

Katika ulimwengu wa leo unahitaji kuwa imara.

Achana na dhana ya kujiita MNYONGE kuanzia leo.
Kuna watu wamekuwa wanakuita MNYONGE . Na hata wewe mwenyewe umekuwa unajiita MNYONGE. Rafiki yangu sikiliza, kuanzia leo hii kataa kuitwa MNYONGE. Na wala wewe mwenyewe usijiite MNYONGE.

Anza kuishi kama MTU imara. Ongea Kama MTU ambaye yuko imara. Tembea kwa kujiamini kama MTU ambaye yuko imara. Kwa jinsi hiyo, utakuwa umetengeneza ulimwengu wako wa TOFAUTI na watu watakupenda.

Utakuwa kama Moto. Moto ni hatari sana. Ukiugusa tu, unaungua. Lakini watu duniani kote wanaupenda kinachofanya watu wapende Moto ni kwa sababu ya uimara wake. Moto hautetereki kwenye uimara wake. Ukiingia kwenye kumi na nane zake unaungua. Ukitumia vizuri unakusaidia kutengeneza vitu vingine ambavyo ni imara. Mfano, ukiutumia kuunguza tofali unazifanya imara zaidi.

Lakini ukiutumia vibaya unaunguza nyumba. Mbali na madhara yote ambayo Moto unaweza kufanya ila tunaupenda kwa sababu ya uimara wake. Tukiwa na baridi tunawasha Moto na kuusogelea karibu kwa sababu tunajua kwamba moto ni imara na hauyumbishwi na baridi. Hivyo tunausogelea ili tupate joto.

Tukihitaji nyama choma, tunaenda kutafuta moto kwa mara nyingine. Tunajua moto ni imara na utatusaidia kugeuza nyama ya kawaida kuwa choma.

Tukihitaji chakula, tunaufuata Tena Moto. Tunamenya ndizi zetu na kuziweka kwenye moto, noto unaturudishia ndizi zikiwa zimeiva.

Huo ndio uimara wa Moto.

Na wewe unahitaji kuwa imara pia


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X