KITABU KIPYA: JINSI YA KUONGEZA THAMANI YAKO


Rafiki yangu mpendwa

Salaam,

Moja ya kitu muhimu sana unachopaswa kukifanyia kazi kwenye maisha yako ni thamani yako. Ila kwanza labda tujiulize thamani ni nini? Ili tujue maana halisi ya thamani nimelazimika kuangalia kwenye kamusi ya Kiswahili sanifu, ambayo inasema Kuwa thamani ni gharama au ubora wa kitu kutokana na hali na kuhitajika kwake na jamii.

Sawa hiyo ni maana ya thamani, na je, ipi itakuwa maana ya thamani binafsi. Thamani yako tunaweza kuiona kwa kuangalia vitu viwili muda na kiasi cha pesa unacholipwa ndani ya huo muda. Kwa mfano, kuna mtu kwa siku anaingiza kipato cha milioni kumi. Wakati kuna ambaye anaingiza kipato cha laki moja. Na wakati huohuo kuna ambaye hata elfu kumi hapati.

Kumbe hawa watu watatu thamani yao binafsi haiwezi kuwa moja. Pengine unajiuliza, imekuwaje mimi nimeamua thamani ya mtu ipimwe kwa kiwango cha fedha anachoingiza. Ukweli ni kuwa siyo mimi niliyegundua hili. Hiki ni kitu ambacho watu wengi wamekuwa wanakitumia kutoa thamani kwa watu, na hata kwenye familia nyingi mtu mwenye pesa anathaminiwa sana kuliko ambaye hana fedha.

Vikiitishwa vikao vya familia, kama kuna kuna watu wawili, mmoja mlevi mlevi na mwingine ni mtu ambaye anafanya biashara na ana kipato kizuri. Ikitokea mlevi akachangia kitu, watu watasema huo ni ulevi hata kama kaongea pointi ya maana, ila mwenye hela hata akiongea pumba, anaonekana ameongea pointi na hata kupigiwa makofi. Chezea hela wewe! Mtu mwenye hela yake anaitwa bosi mkubwa hata kama ni mdogo. Hahaha.

Sasa kwa kwa vile tunaishi kwenye dunia ambayo inathamanisha watu hivyo, hatuna budi kujua hili ili tuongeze thamani zetu au wewe unasemaje? Wewe pia unapaswa kujua thamani yako kwa sasa hivi, lakini pia unapaswa kufanya juhudi ili kufanya thamani yako iongezeke zaidi.

Mbinu unazoenda kujifunza kwenye kitabu hiki zitakusaidia kuongeza thamani yako mara mbili mpaka mara kumi zaidi. Yaani, utaweza kulipwa mara mbili mpaka mara kumi zaidi ya unavyolipwa sasa hivi. Kumbe basi naomba nieleweke kwenye suala moja tu, ninaposema kwamba unaenda kujifunza mbinu za kukusaidia wewe kuongeza thamani yako. Simaanishi kwamba, utaongeza thamani kwa kuwa mrembo zaidi. Wala simaanishi kwamba utaongeza thamani kwa kupata followers zaidi mtandaoni, na wala simaanishi kwamba unaongeza thamani yako kwa kuwa mrefu, mfupi, mtu wa miraba minne, mweusi, mweupe au maji ya kunde!

Bali namaanisha kuongeza thamani kwa kulipwa zaidi. Ukitumia mbinu zilizoainishwa kwenye hiki kitabu, utakuwa na uwezo wa kulipwa mara mbili mpaka mara kumi zaidi. Hivi kwa mfano unaanzaje kuacha kutumia mbinu hizi ili uweze kulipwa zaidi ya unavyolipwa sasa hivi.

Kabla hatujazama zaidi kwenye kitabu, ngoja kwanza tuone namna unavyoweza kujua thamani ya muda wako kwa sasa

Jinsi Ya Kujua Thamani Ya Muda Wako

Mimi na wewe tuna bahati ya kuwa na rasilimali nyingi ambazo tunaweza kutumia kwenye maisha yetu ya kila siku.

Rasilimali hizo ni kama

  • Ardhi
  • Madini
  • Maji
  • Fedha
  • Muda ……

Kati ya hizo rasilimali zote, muda ndio rasilimali ambayo ukiipoteza huwezi kuipata. Hivyo, unahitaji kuweza kuitumia vizuri rasilimali hii ya kipekee.

Na leo nataka nikwambie namna ambavyo unaweza kujua thamani ya muda wako. Kujua thamani kutakusaidia zaidi kuwekeza nguvu zako kwenye kufanya kazi na majukumu ambayo ni ya muhimu, huku ukiachana na majukumu ambayo siyo ya muhimu

Ili tujue thamani ya muda wako, kwanza unapaswa kujua kiasi gani unataka kuingiza kwa mwaka mmoja ujao. Ebu kwa mfano tuseme kwamba una mpango wa kuingiza milionoi 100. (Hiki kitu tukiite A)

Kitu cha pili cha kujiuliza ni muda kiasi gani ambao uko tayari kufanya kazi kwa wiki? Kama kwa siku unafanya kazi kwa saa 15 na kwa wiki unafanya kazi kwa siku sita. Maana yake kwa wiki unafanya kazi kwa saa 90 (Hiki kitu tukiite B).

Na kitu cha tatu ambacho tunataka tujue ni je, kwa mwaka utakuwa tayari kufanya kazi kwa wiki ngapi? Kwa kawaida mwaka una wiki 52. Sasa ni wiki ngapi utakuwa tayari kufanya kazi ukiondoa wiki za mapumziko. Kama unapumzika kwa mwezi mzima kwa mwaka, maana yake unafanya kazi kwa wiki 48 tu kwa mwaka (hiki kitu tukiite C).

Sasa kifuatacho, ngoja tuone thamani ya muda wako kwa kutumia vipengele hivyo hapo juu. Kujua thamani ya muda wako utachukua.

Thamani ya saa lako moja= (A÷B÷C)

Kwa hiyo kama una mpango wa kuingiza milioni 100 (100,000,000) kwa mwaka na upo tayari kufanya kazi kwa saa 90 kwa wiki kwa wiki 48. Hivyo,

Thamani ya saa lako moja=(100,000,000÷90÷48)=23,146

Kwa hiyo wewe thamani ya saa moja kwako ni sawa na 23,148. Ukifanya kazi yoyote ambayo ni ya chini ya hivyo viwango, basi unakuwa umejishusha.

Kama ulikuwa hujawahi kupima thamani ya muda wako, Ebu fanya hivyo siku ya leo. Utajifunza vitu vingi na kikubwa zaidi ni kwenye utunzaji mzuri wa muda wako ili kazi unazofanyaa ziendane na viwango vya thamani yako.

Lakini ubora ni kwamba unaweza kuongeza thamani ya saa lako moja kutoka kiwango cha chini na kukipandisha juu kabisa.

Hakuna kiwango cha ukomo wa thamani ya muda wako unachoweza kutengeneza

Sasa wacha tuzame ndani zaidi kwenye hiki kitabu ili uweze kuona ni kwa namna gani unaweza kuongeza thamani yako hatua kwa hatua. Mbinu unazoenda kujifunza kwenye hiki kitabu ni mbinu ambazo wanatumia watu wanaolipwa kiwango kikubwa cha fedha kwa siku, wiki na mwezi. Ubora ni kuwa mbinu hizi ukizitumia wewe mwenyewe unaenda kupata matokeo makubwa ambayo hata hapo awali ulikuwa hujafikiria kuwa unaweza kuyapata.

Miaka kadhaa iliyopita nilikuwa namsikiliza Les Brown, kwenye yale maongezi akawa anasema kwamba alipokuwa anaitwa kwenye semina alikuwa analipwa dola elfu moja kwa kila maongezi. Ila sasa siku moja katika kuongea na baadhi ya watu waliokuwa wanatengeneza kiasi kikubwa zaidi ya hapo, walimwambia kuwa unaweza kulipwa zaidi ya hapo. Wakamwambia kuwa badala ya kulipwa dola elfu moja unaweza kulipwa mpaka dola elfu tano kwa saa moja. Les Brwon anasema kwamba hiki kitu kilimpa hofu kwanza, lakini baadaye alipoanza kukifanyia kazi, kitu hiki kikaleta matokeo makubwa akawa ameanza kulipwa hicho kiasi na baadaye akaweza kulipwa zaidi ya hapo.

Ninachotaka kukwambia ni kuwa, unaweza kulipwa zaidi ya unavyolipwa sasa hivi. na mbinu zilizoainishwa kwenye hiki kitabu zinajieleza waziwazi tu.

Wasalaam,

Godius Rweyongeza

0755848391

Morogoro-Tz

24 Agosti, 2022.

Gharama ya kitabu hiki ni 20,000/- hardcopy.

Kitabu hiki ni 20,000/-. li kupata kitabu hiki, wasiliana nami kwa 0755848391 sasa ili nikutumie popote pale ulipo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X