Kama Kuna Kitu Unataka Kufanya Kifanye


Badala ya kukaa na kusubiri MTU au watu fulani waje wakusaidie kufanya na kukamilisha kitu au jambo fulani, nakushauri kwamba Kama Kuna Kitu unataka kufanya. Kifanye. Ukiendelea kumsubiri mtu au watu fulani waje wakusaidie kukifanya ukweli Ni kwamba utasubiri sana na hawa watu unaweza usije kuwaona maisha yako yote.

Kwenye hii dunia kuna watu wa aina tatu.
Kuna wale ambao huwa wanatamani vitu, Ila huwa hawachukui hatua na kuvifanya.

Kuna wale ambao huwa wanaona vitu vinafanyika na kuishia kuangalia na namna vinavyofanyika

Mwisho Ni wale wanaochukua hatua kuhakikisha kwamba wamefanyia kazi vile wanavyotamani kufanya.
Wewe unapaswa kuwa kwenye Aina ya tatu.
Hawa ndio wale watu ambao huwa wakiamua jambo huwa wanalifanya bila kusita.
Hawa ndio wale watu ambao huwa wapo tayari kuweka kazi inapohitajika ili waweze kupata matokeo wanayotaka.

Dunia imekuwa hivi ilivyo Leo hii kwa sababu ya watu wanaochukua hatua.
Leo hii naandika makala hii kwa kutumia simu simu ambayo imetengenezwa na watu wanaochukua hatua. Leo hii napanda gari lililotengenezwa na watu wanaochukua hatua.
Hata Kama ukisikiliza muziki jua kuwa umetengenezwa na watu wanaochukua hatua.
Kama unapendelea kuangalia tamthiliya, jua wazi kuwa zimetengenezwa na watu wanaochukua hatua.
Na wewe kuwa tayari kuchukua hatua.
Hakuna namna ambavyo unaweza kupata matokeo ya tofauti kama hutachukua hatua.

Kama Kuna kitu ungependa kufanya Leo hii, Basi uchukue hatua na uanze kukifanya rafiki yangu.

Naomba siku ya leo tukubaliane kitu kimoja tu. Na kitu hiki Ni wewe kufanya kile unachotamani kufanya bila kurudi nyuma kuanzia leo hii.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X