Ushauri Muhimu Kwa Mtu Yeyote Ambaye Ana Lengo La Kuweka Akiba 2023


Hivi ulivyo mwanzo wa mwaka najua kuna watu wengi ambao wameweka lengo la kuweka akiba. Watu wanataka waweke akiba ili waweze kupata uhuru wa kifedha. Sasa siku ya leo ningependa kukwambia kitu kimoja muhimu sana, wewe ambaye umeweka lengo la kuweka akiba

KABLA sijakwambia hiki kitu naomba kujua ni wapi utakuwa unaweka fedha zako za akiba. Je, fedha hizi utakuwa unaziweka benki, au fedha hizi utakuwa ukiziweka chini ya godoro?

Kitu kimoja kikubwa ambacho ningependa kukwambia siku ya leo ni kwamba mwaka huu FUNGUA AKAUNTI YA UTT na fedha yako ya akiba uwe unaiweka huku.

Pengine unajiuliza UTT amis ni nini?

UTT ni mfuko wa uwekezaji wa pamoja ulio chini ya wizara ya fedha. Ambao wenyewe kazi ni kukusanya mitaji kutoka kwa watu na kuiwekeza kwa niaba ya watu.

Kwenye hii makala sitaeleza kwa undani zaidi kuhusiana na UTT. Kama utapenda kujifunza zaidi kuhusiana na UTT nashauri sana usome kitabu changu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. Hiki kitabu kina kila kitu unachohitaji kujua kuhusu uwekezaji kwenye UTT.

Humu kwenye blogu pia kuna makala nyingi kuhusiana na uwekezaji huu. ila kikubwa ninachotaka kusisitiza kwenye makala ya leo ni kuhusu mrejesho pale unapoweka hela yako.

BENKI nyingi hazitoi riba kubwa kama ilivyo UTT. Na UTT imedhihirisha kuwapa mrejesho mzuri wawekezaji wake kwa muda mrefu zaidi.

Hivyo kama kuna kitu ambacho nakushauri rafiki yangu ni kimoja tu. mwaka huu akiba yako iweke UTT badala ya kuiweka sehemu nyingine.

Kila la kheri.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

Baadhi ya vitabu vyangu vimesomwa kwa mfumo wa sauti yaani, audiobook. Na mojawapo ya kitabu ha aina hiyo ni kitabu hiki CHA NGUVU YA VITU VIDOGO KUELELEA MAFANIKIO MAKUBWA. Hakikisha unapata kitabu hiki mapema iwezekanavyo. Tuwasiliane kwa 0755848391

Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X